Kwa hili la huyu mpenzi wangu acha pesa zangu ziishie kwa mama tu!

Minjingu Jingu

Senior Member
Nov 2, 2023
116
480
Iliniumiza sana msichana tumeanza naye mahusiano siku tatu tu akaniambia ana changamoto anahitaji tsh 150,000. Nikamwambia sina yote nina Tsh 100,000 nikamtumia. Hakusema hata amepokea, akanyamaza tu.

Ikabidi nimpigie simu kujua kama amepokea au laah, akapokea simu nikamuuliza "umeona kuna pesa kidogo nimekutumia Tsh. 100,000", akasema "Nimeona." Nikasubiri hata aseme asante hakusema, akaniambia, "Nipo natafuta hiyo 50,000 kwa rafiki zangu waniongezee maana nilitaka tsh 150,000 na nilikuambia hivyo."

Nikasema sawa nisamehe sikuwa nayo yote, akanijibu "Basi baadaye." Nikaingia kwenye menu yangu ya Tigo Pesa nikaomba kuirudisha ile pesa, nashukuru haikuchelewa sana ikarudishwa, nikamshukuru Mungu.

Nikamtumia mama yangu Tsh. 20,000 nikanyamaza. Akapiga simu dk hiyo hiyo akishukuru sana na kunitakia mibaraka mingi mingi, nikamwambia mama hiyo kidogo, akasema hapana hakuna pesa kidogo, akashukuru na kuniombea pale nilipopungua parudishwe.

Basi alivyokata tu simu nikammalizia na ile nyingine 80,000, akanipigia simu tena this time nikamwambia mama naingia kwenye kikao, nashukuru Mungu akubariki.

Niliona angenishukuru sana mpaka nakuwa najisikia vibaya. Siku zote mama yangu yupo hivyo umtumie 10,000 ya voucher umtumie 200,000 ya matumizi shukrani zake zipo pale pale. Nikawaza sana kuwa hawa wanawake wa sasa hivi wanakwama wapi kuwa that much cold?

Yule msichana mpumbavu akanipigia simu kuwa mbona tena ile pesa nimeichukua, nikamwambia niliona ni ndogo sana nimeichukua nimemtumia mama, yeye asubiri nikipata nyingi nitamtumia, nikakata simu.

Mpaka leo hatuna tena mawasiliano, nime-mblock.
 
Ati mama yako awe girlfriend wako?
Hiki Kizazi cha Vijana waliolelewa na SINGLE MOTHERS ni shida. Enyi kina dada ulizeni kwanza kabla ya kuingia kwenye mahusiano. Kijana wa Kiume aliyelelewa na Single Mother ni kimeo sana, wameanza ooooh kataa Ndoa ili muishi kama mama zao. Mwingine ooooh mama awe girlfriend wangu. Hiii mitoto ni shida tupu
 

Attachments

  • Screenshot_20231123-104813_Google.jpg
    Screenshot_20231123-104813_Google.jpg
    60.6 KB · Views: 18
iliniumiza sana msichana tumeanza naye mahusiano siku tatu tu akaniambia ana changamoto anahitaji tsh 150,000. nikamwambia sina yote nina tsh 100,000 nikamtumia. hakusema hata amepokea. akanyamaza tu. ikabidi nimpigie simu kujua kama amepokea au laah. akapokea simu nikamuuliza
"umeona kuna pesa kidogo nimekutumia tsh 100,000". akasema
"nimeona."
nikasubiri hata aseme asante hakusema. akaniambia
" nipo natafuta hiyo 50,000 kwa rafiki zangu waniongezee maana nilitaka tsh 150,000 na nilikuambia hivyo"

nikasema sawa nisamehe sikuwa nayo yote.akanijibu "basi baadaye"
nikaingia kwenye menu yangu ya tigo pesa nikaomba kuirudisha ile pesa. nashukuru haikuchelewa sana ikarudishwa. nikamshukuru Mungu.
nikamtumia mama yangu tsh 20,000. nikanyamaza. akapiga simu dk hiyo hiyo akishukuru sana na kunitakia mibaraka mingi mingi.....nikamwambia mama hiyo kidogo. akasema hapana. hakuna pesa kidogo. akashukuru na kuniombe pale nilipopungua parudishwe. basi alivyokata tu simu nikammalizia na ile nyingine 80,000. akanipigia simu tena this time nikamwambia mama naingia kwenye kikao. nashukuru Mungu akubariki.

niliona angenishukuru sana mpaka nakuwa najisikia vibaya. siku zote mama yangu yupo hivyo umtumie 10,000 ya voucher umtumie 200,000 ya matumizi shukrani zake zipo pale pale. nikawaza sana kuwa hawa wanawake wa sasa hivi wanakwama wapi kuwa that much cold?

yule msichana mpumbavu akanipigia simu kuwa mbona tena ile pesa nimeichukua. nikamwambia niliona ni ndogo sana nimeichukua nimemtumia mama yeye asubiri nikipata nyingi nitamtumia. nikakata simu. mpaka leo hatuna tena mawasiliano. nime mblock
Yaani ungekuwa jirani yangu ningekupa hi 10. Yaani magold digger. Tena laki hashukuru? Mungu alikulinda uachane naye mapema kabisa. Poleni Sana vijana ambao bado hamjaoa ni mtihani Sana kumpata mwenza sahihi. Ndoa changa tunaona jinsi wanasumbuana mara tu baada ya ndoa. Wazee tumebaki kuwa wasuluhishi tu. Vijana wanatuchosha Sana.
 
Back
Top Bottom