Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Nchi zote duniani zimechukua tahadhari kubwa kuhusiana na hili gonjwa la corona, kuna serikali zimefungia raia wake wasitoke nje ikiwemo nchi za Africa Isipokuwa Tanzania.

Kwa hakika hili la Rais Magufuli kuruhusu shughuli ziendelee anapaswa kupongezwa na sio kubezwa, watanzania wengi ni masikini sana kipato chao kinategemea atoke arudi na chochote kumzuia akae ndani atakufa njaa.

Kwa kweli rais wetu ameona mbali kuruhusu shughuli ziendelee, cha muhimu ni sisi watanzania kumuunga mkono kwa kuuchukua tahadhari zote tuwapo kwenye shughuli zetu, na kwa hakika baada ya hili janga Rais Magufuli ataonekana shujaa hasa katika ukanda wetu huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila nimejaribu kutembea huko mitaani Yan wananchi hawajali kabisa kuhusu huu ugonjwa. Hakuna tahadhari yoyote wanayoichukua ndio Kwanza wapo busy na mambo yao bila tahadhari yoyote,

napata shaka endapo ugonjwa huu utaingia mitaani kwa lugha nyingine uswazi tutamdisapppoint rais wetu, maana kwa mtindo huu wa maisha maambukiz yatakuwa kwa kiwango Cha juu sana ambacho akijawahi shuhudiwa tokea janga hili limeikumba Dunia hii.
 
Naunga mkono hoja, Rais Magufuli ni shujaa.

Wakati nchi za wenzetu wanaona Corona kama ugonjwa hatari hivyo kufunga mipaka, kusimamisha shughuli zote na hadi kufanya lock down kwa kutegemea nguvu za binaadam, shujaa rais Magufuli ameishtukia Corona sio ugonjwa bali ni shetani limekuja kwa mfano wa ugonjwa hivyo alichofanya ni jambo dogo tuu, kulikabidhi kwa Mungu ambaye ni kiboko ya shetani.

Mungu ameisha tukingia mkono wake, Tanzania bado hakuna kifo wala maambukizi ya ndani kwa ndani, local transmissions. Hivyo tuungane na rais wetu Magufuli, tusitishane, na Watanzania tuendelee kuchapa kazi, kwenda Kanisani, msikitini na kujichanganya na watu kama kunywa kahawa kidogo mitaani bila sanitizers kwa kukaribiana as if nothing happened huku tukichukua tahadhari kama tunavyoelekezwa na wataalamu iliwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.

P
 
Anaweza kuonekana shujaa kwa wazembe kama wewe kwa kusababisha wananchi wake wengi kufa kwa kutokuchukua tahadhari za kujikinga. siku mkianza kufa kama kuku naomba mje na mapambio haya haya.
 
Kama ulibet basi ujue UMELIWA..
HOFU HUUA.
Soon tutapoteana na huyo mjinga wako.Kaenda kujificha Chato
20200329_082740.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaweza kuonekana shujaa kwa wazembe kama wewe kwa kusababisha wananchi wake wengi kufa kwa kutokuchukua tahadhari za kujikinga. siku mkianza kufa kama kuku naomba mje na mapambio haya haya.

Hivi bro, unadhani ni tahadhari gani US, UK, Spain, Italy nk hawajachukua?

Hizi ni first world countries, kila siku watu wanaugua na wanakufa.

Sisi tuchukue tahadhari zipi ambazo wao hawakuchukua?
 
Wa kumshukuru ni Muumba mbingu na Dunia na wala sio JIWE
hata ktk vitabu vitajatifu Mungu alinena na kutenda kupitia vinywa vya manabii na wateule. sio kuonekana na kusema na wanadamu.

fungua akili. pokea huu unabii. mh. Rais ametenda jema, madhara ya kufungia watu ndani na kusimamisha shughuli za biashara yangekuwa mara 100 ya yale ya covid-19.

tungeshuhudia vifo vya njaa, wizi na unyang'anyi, vifo vya magonjwa baki, uchumi kusinyaa nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom