Whitesmith
JF-Expert Member
- Aug 12, 2017
- 454
- 635
Habari ya Leo GT.
Kwa hili CHADEMA CHUKUENI HATUA;
1: Kesi hizi zilitengenezwa ili muanze kuhangaika na muhimili wa mahakama, Je nia yao ni nini?
a: Kupunguza pressure mtaani
b: Kupunguza mzigo kwa CCM
c: CCM na watu wao kujificha katika muhimili mwingine, ionekane ya kwamba suala liko mahakamani na huku wao wakichezesha mhimili wa mahakama kwa mlango wa nyuma.
2: Nini kifanyike?
a: Chama kianze harakati zake kama kawaida.
b: Chama kiandae wapambanaji mbadala Kila hatua, ili wakiwakamata waliopo wengine waendelee.
c: Tuwe tayari wote kwenda gerezani, isiwe suala la Lissu peke yake kuwa gerezani, kama mikoa yote tuna Kesi mahakamani hii itasaidia siyo tu kuonesha ukatili wa CCM kupitia mahakama Bali itasaidia kuhuisha Ari na mapambano ya kweli, Africa kusini hakwenda Mandela peke yake. Mapambano lazima yaendelee NRNE.
d: Tupunguze kulia lia, ndo Maana Lissu anatuuliza Kila siku "Mimi sijachoka nyinyi mmechoka?" anaona kabisa hatuna Ari ya mapambano, nani aliwaambia vitani akifa kamanda Ari ya mapambano inakufa? Ari ndo inazidi kuongezeka! Ndg Heche toa mwongozo kwenye mabaraza yote ya Chama, VIONGOZI wa Kanda na wote katika mikoa Yao mashambulizi yaendelee, acha kulia lia na mahakama.
e: Punguza mahudhurio ya Mahakama! anza kuchora ramani ya mapambano kuna kina Heche wa Tarime, tuna wapambanaji wa songea kule, tuna wapambanaji wa Arusha, Dodoma, tuna wakiki Matata, Lema arudi field nk, haki haiombwi inapambaniwa.
f: Tusiwafundishe wanachama unyoge na kulia lia, ndo maana Lissu alitamka wazi mahakamani mjiandae nikitoka tunarudi barabarani. Mlisema mtafanya siasa ngumu, inawezekanaje kiongozi katekwa hakuna amsha amsha? mnalia Lia kama uongozi uliopita? Tunataka nchi yote iwe kama Wamasai, huwaoni wakilalamika mtandaoni ila wako organized unawakuta wamekusanyika elfu 40 wanadai haki Yao.
Sasa tunatakiwa tumdai Lissu aachiwe kwa maandamano nchi nzima na mikoa yote, tunataka reform kwa maandamano yasiyokama huku wanachama wakishikilia majani mikononi na sime kiunoni kama ishara yakuwa tayari kwa mapambano. Kama kweli viongozi wa serikali ya mitaa hawakuchaguliwa basi wananchi wawe tayari kuwaotoa madarakani wakakusanyike Dodoma huko.
g: Ni muda wakuchagua mitume nakuwaosha miguu. nimemtumia huo mfano wa alichofanya Yesu, sasa basi mpaka muda huu tunawajua wapambanaji gani wawe front line na field wawe kina nani. Waite mikoa yote au pita Kanda zote waoshe miguu yaani wape mamlaka na wawe tayari kwa utii na wawe tayari kwa kiapo kuwa kwa damu ya wapambanaji wenzao walioanguka udongoni ( Ali Kibao, na wenzake, ) hawatasaliti mapambano iwe ni kiapo.
h: Viongozi wa matawi na shina hadi ngazi watengeneze mtandao wa mawasiliano wawe wanaweza kuwasiliana nakukusanyika kwa ghafla na very surprised, ili watesi wakute nchi nzima tumekutana na tunadai kitu kimoja, fikiria kina Bibi Titi waliwezaje kuwa organize watu na mikutano ikafanyika kipindi ambacho barabara ni mbovu mitaa iko mbali mbali, hakuna simu.
Je, nyinyi mnashindwa nini kuorganize wafuasi? Acheni kulia lia na mahakama ni upbavu kwenda kulia lia kwa CCM. wewe unajua kabisa huyu jaji ni WA Mchongo, wachieni nawakili waendelee naye sisi huku field kiwake yaani hamasa iwe kubwa. Yaani sasa hivi ni kama tunamsuburi Lissu atoke ndo vibration ianze!
Na shuka Jukwaani, nimekosa usingizi harakati zinachemka kifuani....