Baada ya matukio ya MO29 (Oktoba 29) na sasa tukiwa tunaelekea kwenye maandamano ya D9 (Desemba 9), hali ya taharuki imeongezeka sana. Yale tuliyoyaona MO29—ambayo hata hayafikii robo ya hali ya vita yamenifanya kuwa makini sana.
Mijini hali ni ngumu. Huwezi kutulia wakati mambo yanapowaka, isipokuwa kama unaishi maeneo yenye ulinzi na watu walio ndani ya mifumo ya usalama. Kwingineko, hatuko salama kabisa.
Wakati wa MO29 hatukuweza kutoka nje. Watu wengine walijikuta wahanga bila hata kushiriki maandamano. Kupata huduma za kijamii ilikuwa changamoto kubwa. Na bado, hali ile haijafikia hata sehemu ndogo ya kile kinachoweza kutokea kwenye vita.
Ukifikiria kama hali ingeendelea kuwa mbaya zaidi, ni rahisi kuona jinsi watu wangekimbilia misituni bila makazi maalum, wengine wakitafuta hifadhi kwenye kambi za wakimbizi na kulala kwenye mahema.
Sehemu ambazo zilionekana kuwa salama zaidi ni vijijini. Watu waliendelea na shughuli zao, walienda kusali, wakafanya ibada zao, na kuishi maisha yao kwa uhuru zaidi.
Kwa jinsi mambo yanavyoendelea na vijana wanavyozidi kupoteza uoga tuliokuwaga nao vizazi vya kabla ya miaka ya 90, kuna hatari ya waandamaji kujilinda kwa njia ambazo zinaweza kuongeza machafuko. Hali kama hiyo inaweza kupelekea mazingira yanayokaribisha vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo mara nyingi huanzia mijini, kwenye majiji au makutano ya mkoa.
Kwa yote haya, kujenga maisha na makazi ya kudumu vijijini ni muhimu sana. Sio kwamba familia nzima inategemea nyumba moja tu ipindi cha sherehe au misiba bali kila mtu kuwa na nafasi yake ya kujitegemea na usalama wake.