Kwa hija hizi CHADEMA ni afadhali msishiriki Uchaguzi Mkuu 2020

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Vitus Nkuna: Tumepata Shida Sana.

Jibu: Hizi ni kelele na wala sio hoja. Hujasema wazi ni shida zipi, kwani zipo shida za uvivu, shida za ndoa n.k. Muungwana hasemi kama hana ushahidi wa kusema wazi. Mjinga anasema kwa kuwa ni kawaida kusemasema ovyo ovyo!

Vitus Nkuna: Ndugu zetu wamepotezwa.

Jibu: Hujasema hao ndugu zako wamepotezwa na nani, na katika mazingira gani. Na kwa bahati mbaya hujasema kama uliwahi kwenda kutoa taarifa mahala husika. Ni dhahiri kuwa huna ushahidi. Narudia tena, mtu muungwana hasemi pasipo ushahidi!

Vitus Nkuna: Ndugu Zetu wameuliwa

Jibu: Huu ni sawa sawa kabisa na ujinga wa hapo juu, et ndugu zetu wamepotezwa! Siwezi kuusemea kwa mara ya pili.

Vitus Nkuna: Biashara Zetu Zimefungwa

Jibu: Si rahisi ukafungiwa biashara yako ikiwa unafanya kazi rasmi na kwa uadilifu bila ukanjanja. Jifunze kuwa muadilifu hutafungiwa biashara yako. Na kama walikuonea ni ujinga wako kama hukwenda kuitafuta haki yako mahala husika.

Vitus Nkuna: Ajira Hakuna

Jibu: Katika karne ya sasa na karne nyingine nyingi zijazo ajira itaendelea kuwa ni tatizo kwa watu wavivu wa kufikiri na wachaguzi.

Vitus Nkuna: Uhuru wa habari Umezimwa

Jibu: Huu nao ni ujinga. Kwani nikikuuliza, umewezaje kufahamu hali ya siasa ya nchi, uchumi pamoja na hali ya watu kwenye jamii! Bila shaka jibu lako la kimyakimya unakubali kuwa ni kutokana na uwepo wa uhuru kwa vyombo vya habari makini, na wala sio wale wanasiasa katika jukwaa la vyombo vya habari.

Vitus Nkuna: Udikteta Umetawala

Jibu: Tanzania hatukuwahi kutawaliwa na dikteta isipokuwa na viongozi wazalendo kwa misingi ya katiba ya nchi. Labda kama utakuwa unafasiri uadilifu, uzalendo na usimamizi mzuri wa maliasili za nchi kuwa ndio udikteta. Ila ninakuapia hatutakuja kutawaliwa na dalali la nchi ambaye kwa njaa zake likotayari kuiuza nchi na kutanga hadharani kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Vitus Nkuna: Afu leo Mtu anajichekesha kwetu Apoteleee Mbali

Jibu: Hapa umejikwaa kidogo ndugu yangu. Huwezi kumuita mtu mwenye cheko la furaha kuwa anajichekesha kwa tafsiri yako mbovu. Watanzania wengi ni wenye furaha sasa, kwa kuwa wanaona nchi inaenda na kwamba wanaona matumaini yapo, watanzania wanafahamu kuwa kwa sasa serikali yetu chini ya ilani ya CCM inafanya kazi ya ujenzi wa nchi kwa maslahi mapana ya taifa na kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Mtu akicheka akiwa mbele yako, ama nyuma yako ni haki yake kufanya hivyo ikiwa tu aiingilii uhuru wako ndugu.

Mwisho.
 
Ngojeni kipenga kipulizwe mbona mna kiherehere kama kuku anayetaka kutaga? Ile siyo ilani wala sera ilikuwa kutest mitambo tu. Mbona CCM mna hofu sana usiku kucha mchana kutwa mnashindana kuanzisha nyuzi za Lissu na Chadema hadi mnatia huruma.
 
Tulia dada muandalie mumeo chakula cha usiku ale ashibe akukojoleshe.
Mambo ya siasa yanakuzeesha bure.))
 
Chaguzi zote Tanzania zimefanyika kwa uwazi na Uhuru kabisa.
 
Back
Top Bottom