Kwa hiyo wananchi wa Musoma Mjini walimchagua muhuni mwenzao?
Walichuuzwa na jina la Nyerere wakafikiri kwa kuwa atakuwa anatoka katika ukoo huo atakuwa kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa hiyo wananchi wa Musoma Mjini walimchagua muhuni mwenzao?
Mbona Majimarefu naye atakuwepo?
Huyo Vicent anaonekana ni mtu wa matusi tupu kwa sababu CV yake tu inaonyesha amesoma shule tatu (3) msingi ambazo zote zipo hapo hapo Musoma Mjini inaonekana hana nidhamu.
Vipi ya profesa maji marefu na jah people aliyenazo atumwagie hapa katika huu uzi.
Alipata div ngapi form 4?
huyu jamaa pia alikuwa hajawahi kusikika katika siasa za nchi hii kwa sababu inawezekana aliamini nchi imejaa wasomi na watasaidia kutatua (au kujaribu) matatizo yaliyopo.Mi nna CV kali lakini siajwahi pewa hata uenyekiti wa kitongoji!!!
Siyo lazima awe na degree ila hii imezidi angekuwa hata vyeti vya veta angalau kuongezea ongezea. Unajua tuache ushabiki humu JF kumteua Form 4 tena ambaye hatujui kama alifaulu kidato hicho kuwa kampeni meneja ni kututukana watanzania. Lakini tusishangae MBOWE anahitaji watu wa aina hii ili iwe rahisi kumnyenyekea na kupiga magoti. Vicent, Sugu, Lema ni aina ya watu wanao mfaa sana mmafya huyu. Hivi akina Halima mdee elimu zao wanatumiwaje na Chama?mzee elimu ni vyeti au uelewa.
unaweza ukanipa elimu ya zuma
Nampenda kijana maana hajadanganya popote,hana vyeti ila ana uwezo waulize akina profesa flani nini walifanyia Taifa?zaidi ya kuiba?Wenye CV nzuri ni wepi, na wamefanya nini na hizo CV zao kama si aibu tupu na hawana michango kwa jamii ya kitanzania?
Tutegemee matusi matupu sikujua kama jamaa ana elimu ya form 4 alikuwa wapi kujiendeleza
Vicent amenajisi elimu kumpa ukampeni meneja Arumeru kama chadema watashinda wategemee CCM kukata rufaa kwa maneno yake likiwemo la Mkapa alimuua Nyerere.