Tutegemee matusi matupu sikujua kama jamaa ana elimu ya form 4 alikuwa wapi kujiendeleza
Haya ndiyo waliyofanya wasomi wa Tanzania.
1. JAKAYA MRISHO KIKWETE (PHD)
- Alipoulizwa kwa nini Tanzania ni Maskini akajibu hata yeye hajui (ndiye RAHISI wetu!)
- ameiongoza nchi kwenye mdororo wa uchumi kiasi kwamba mfumuko wa bei haukamatiki.
- Ni muongo! aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania na akaleta bora maisha kwa kila mtanzania
- Alikubali kutumia 60 billion kwa kusherehekea sikuu ya uhuru huku akishindwa kuwalipa posho madaktari hadi kusababisha mgomo wa madaktari ulioletea vifo vingi vya wananchi wasio na hatia. (PHD ilisaidia nini?)
2. ANDREW CHENGE - (majority mnajua kwamba kwenye eneo la sheria kwa usomi huyu jamaa yuko juu sana hasa sheria za kimataifa.
- Alisababisha tukashikishwa rada kwa bei ya kutupwa
- Alisimamia mikataba mibovu
- alishindwa kuishauri serikali kwa manufaa ya Taifa.
3. Mungai(PHD)
- alichezea elimu ya Tanzania akibadilisha sylabus kila mwaka hivyo kuwafanya watoto wetu kuchanganyikiwa wakati wa kwake wanasoma international schools.
- Alifuta Michezo mashuleni (kwa elimu yake aliona michezo ni kupoteza muda)
- Alilazimisha masomo ya kifaransa wakati anajua hana walimu!
4. Professor Juma kapuya
- Hapa nimepanic naana kila nikiangalia ni bogus tu hata sijui niandike lipi!
5. Shukuru kawambwa (PHD)
- yaani kikwete anambeba na kumbadilisha wizara kwa sababu ya undugu lakini hata sikumbuki zuri alilofanya!
6. Professor Kigoma Ali Malima
- Akiwa waziri wa fedha ndipo shillingi ya Tanzania ilizidi kuporomoka! Aliishia kujenga misikiti wizarani!
7. Proffesor Ibrahim Lipumba
- Cuf imemshinda!
N.B huu wote ulikuwa ni uchokozi tu lakini nilichokuwa na maanisha wasomi wetu ndio wanaotupeleka kubaya! Ndio wanatuingiza kwenye mikataba feki! Ni msomi gani ambaye haoni ufisadi wa kubadili jina la kampuni kila baada ya miaka mitano ili wakwepe kodi? Ni msomi gani ambaye haoni kwamba POMBE inalipa sana kodi KULIKO DHAHABU! wasomi wetu wengi ni wajinga ELIMU HAIJAWAHI KUWASAIDIA!