Kwa CV hii kuna pointi kweli huko Arumeru

Kwa CV hii kuna pointi kweli huko Arumeru

Wazaz hii nchi ni domo tu linatakiwa hata waliosoma nao hawana la maana zaidi ya kuiba kama Mkapa.kusafiri kama JK,waoga kama Pinda .....................kuna nini wamefanya?
 
Kweli kazi tunayo!
Ndugu zangu kama kweli tungekuwa na wasomi ambao ni viongozi (Maana kuna wasomi ambao sio viongozi) tusingekuwa na mikataba mibovu hivi! Tusingekuwa tunauza nchi hovyo hovyo hivi! Watoto wetu wasingekuwa wanakaa chini ya mwembe hadi leo! Tusingekuwa tunauana kama leo! Tusingekuwa na waropokaji kama leo.
Hatuna viongozi wasomi hapa na hata kama tunao wamemezwa na nyangumi wasomi wasokuwa viongozi. Wameingia huko kwenye uongozi kujaza matumbo yao!
Manyangumi hawa hawataki Viongozi waliozaliwa kuwa vingozi!
Wale waliozaliwa viongozi wakitaka kusema ukweli hawa nyanguma wanawaangamiza!
Angalia wakoloni walichotaka kumfanyia JK Nyerere
Angalia Kilichompata Edward Sokoine
Angalia Horace Kolimba
Angalia Mwakyembe
Na sasa angalia kumbe naye JK Nyerere
Mifano ipo lakini hamwoni.
Mnaona lakini mnaishi kama hamwoni!
Hapa nafikiri tujadili uwezo wa mtu na sio elimu ya mtu.
Fungukeni sasa hasa kwa kipindi hiki. Hatma ya Watanzania ipo mikononi mwenu!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Je chadema na CCM ni chama kimoja? ungependa vifanane kwa mabaya na mazuri?
Vile vile Vuta nikuvute anapaswa kujua kwamba CCM hawawezi kmsimamisha kampeni meneja wa shule ya aina hiyo.
 
Ndugu zangu wana JF. Kwa muda mrefu sana jukwaa letu hili linazidi kupoteza mvuto siku hata siku, kisa hasa ni ushabiki. Kama Jambo likianzishwa la kuisifu au kuikosoa CCM au CHADEMA basi tegemea mada hiyo kuishia watu kuvaana maungoni. Mimi siamini kwamba hiyo inatokana na uelewa mdogo tulio nao wachangiaji bali ni kutokana na ushabiki uliotopea kwenye mbongo zetu.

Hoja ya Elimu ina mashiko lakini na kwa upande mwingine tunashindwa kutofautisha kati ya Elimu na usomi. Usomi ni hali ya mtu kufaulu mitihani na kuthibitishwa kufaulu kwake na mabingwa wa ufundishaji kwenye fani husika. Inawezekana kabisa mfundishaji huyo wa fani husika asiwe kabisa na elimu ya kile anachokifundisha. Hapa inahusika na uwezo binafsi wa mtu katika kukariri mambo.

Lakini hapo hapo kuna baadhi ya wasomi ambao pia ni watu wenye elimu pia. Watu wa aina hii ndiyo wale wanaotumia usomi wao kutatua matatizo ya watu wanaowazunguka badala ya kuwa wakaririfu. Hebu tujiulize ni kwa nini wasomi wanapotaka kufanya utafiti wa jambo lolote lile hawaendi kuwahoji wale wenye elimu wenzao kwa lengo la kuandika andiko lao badala yake wanakwenda kuwahoji watu wasio na elimu kama yao?

Tanzania tunahitaji sana wasomi lakini tunahitaji zaidi watu wenye elimu. Na kama mchangiaji mmoja alivyoeleza kupatikana kwa elimu hakutegemei peke yake kwenda kukaa darasani na kufundishwa na mwalimu jambo fulani, kuna aina nyingi sana za jinsi ya kupata elimu. Hivi magari yetu yakiharibika huwa yanatengenezwa na nani, suti tunazovaa hushonwa na nani, nyumba tunazoishi zimejengwa nanani au hata wasusi na vinyozi wa nywele zetu ni Maprofesa. Au tunadhani fani hizi hazihitaji elimu ya jinsi ya kuzifanya?
 
Honestly...na mimi nimepata mwanga wa haswa kwanini alikuwa na audacity ya kutoa 'fact' (kwangu ni fallacy) zisizo na research nyuma yake...sijui kwa nn but ile statement kuhusu ex-Police Oficcers na u-DC ilinikera..na mimi ni mwanachadema whatever that means!!!!
 
mh! Mbona mnatuvua nguo watu wa msoma na kama jina linavyojieleza?
 
Inamaana huyu bwana hajawahi kufanya kazi yeyote? hata ku volunteer?
 
Vicent kaonekana hana elimu kwakuwa kasema ukweli, je kapa alipo tukana mbona hamjataja elimu yake.Elimu inampelekea matusi,wizi na uuaji hiyo ndo elimu.Kipaji kina zaliwa vicent pia amezaliwa na kipaji.mbona ccm kuna mbungee wa rolya ni std vii Mzee amejiumbua mwenyewe kwa kupayuka wacha wampe vidonge vyake.
Lakini usisahau kuwa Mhessgimiwa Rais Jk alimtimua marehemu Balali kwa kutokufanya kazi sivyo pamoja na elimu yake
 
Siasa ni jinsi unavyozipanga karata zako na uwezo wa kutoa hoja zako kwa wapiga kura. Si unamjua Profesa Maji Marefu mbunge wa jimbo mojawapo kule Tanga, yeye ni darasa la saba tu lakini anaongoza jimbo la uchaguzi.
 
Kwa hiyo waliomchagua wote ni wajinga?
Wakati wa uchaguzi CCM ilimsimamisha msomi yupo wapi leo?
Hapa ukisema mtoa mada ni Mpumbavu unaweza kula ban. Lakini nimemaanisha hivyo
 
Ukimuona mtu ana elimu ya Msingi lakini amepata madaraka makubwa kuliko wewe unayejiita msomi. UJUE KAMA WEWE UNGEISHIA FORM FOUR hakika hata kazi ya house boy/girl usingepata
 
Ni ajabu sana kulinganisha cv na uelewa wa mtu, kwa elimu ya tz cv za kukalili darasani, nashukuru siku hizi ukitaka kuajiriwa kama professional yako ni computer, waajiri hawaangalii cv yako ila wanakukabidhi computer wanakwambia haya fanya kile unachokiombea kazi, wanaangalia kama kweli kina relevant na cv yako. Najua wengi humu jf wana cv nzuri lakini ni za kukariri au kununua au kupewa kama baba mwanaasha, au hata waliiba cv za watu na ndizo zilizowaweka mjini mida hii
 
Siasa ni jinsi unavyozipanga karata zako na uwezo wa kutoa hoja zako kwa wapiga kura. Si unamjua Profesa Maji Marefu mbunge wa jimbo mojawapo kule Tanga, yeye ni darasa la saba tu lakini anaongoza jimbo la uchaguzi.
"Jambo moja ambalo ni la msingi ni kwamba elimu ya darasani kwa tulipofikia na dunia tuliyo nayo leo ni ya msingi hata tufanyeje.Lakini la pili ambalo ni hakika,unatumiaje hiyo elimu yako uliyoipata.unaweza ukawa na elimu na uelewa mdogo lakini ukautumia vizuri kwa asilimia 100% na kuleta matunda kuliko kuwa na PHD ambayo hata haitumiki.Kwanza huko ni kupoteza rasilimali,kwa muda ulioutumia kuitafuta ,ungefanya jambo ambalo ni productive ungelichangia taifa.
Lakini pia tuangalie lengo la elimu ni nini?
Nikutusaidia kutambua mazingira yanayotuzunguka, na hivyo kuweza kutatua matatizo tuliyo nayo.kama una PHD ya sheria,Uhandisi,Udaktari na fani nyinginezo na huwezi kututatulia matatizo yetu ni kazi bure.
Tukumbuke pia ,wale wote tunaowaita great thinkers ,wengine wakati huo hata hawakua na elimu ya darasani lakini waliweza kutufanyia mambo makubwa.
Suala lililopo hapa ni kutatua matatizo tuliyo nayo.Tuna wasomi ambao hata wameshindwa kutusaidia kwenye mikataba ya madini.tunapata 4% instead of 50/50 halafu ndio hao tunakaa kuwatetea hapa,huu ni upuuzi wa hali ya juu.Tuna wasomi wanaoshindwa kuhakikisha watu waliotufikisha hapa,kwa ufisadi wanaondolewa madarakani, wao ndio wanawatetea,I will opt for Vicent kwani na elimu yake ndogo anaweza akasimamia anchokiamini.tunahitaji mtu mwenye Common sense as "Common sense is not common to common people like you"
 
Ni heri V. Nyerere mwenye elimu ndogo mzalendo kwa watanzania,kuliko Mkapa mwenye
elimu kubwa,aneyewafanya watanzania wanasafa kwa sera yake ya ubinafshaji na uwekezaji
na kutuibia Kiwira na kufanyia bioashara kwenye ikulu yetu.
 
ni bora yeye amesema ukweli kuhusu elimu yake,hao unaoona wana madegree ni ya uongo hamna kitu huenda huyu anawazidi mbali sana
 
bunge letu linabakwa na wabunge wenye degree,masters,phd tukiangalia kweli bunge letu linahitaji viwango hivyo vya elimu ili watu wakasinzie,kuzomea,kupiga makofi bungeni darasa la saba wanafaa pia kuwa wabunge siyo ishuuu kabisa elimu bungeni
 
Member Type:Constituency Member

[TD="bgcolor: #b1c3d9, colspan: 3"] GENERAL [/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Salutation [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Honourable[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] First Name: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Vincent[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Middle Name :[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Josephat Kiboko[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Last Name: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Nyerere[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Constituent: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Musoma Mjini[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Political Party: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]CHADEMA[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Office Location: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Box 557, Musoma[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Office Phone: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]+255 28 2620610/+255 713 275804[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Ext.: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Office Fax: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Office E-mail: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Member Status: [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"] Date of Birth [/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd Date

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 5"] EDUCATIONS [/TD]

[TD="width: 10%, bgcolor: #b4c6db"] Level [/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Mukendo Primary School[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Primary Education[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1983[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1985[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]PRIMARY[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Mwere Primary School[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Primary Education[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1985[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1988[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]PRIMARY[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Iringo Primary School[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Primary Education[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1988[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1989[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]PRIMARY[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Ikizu Secondary School[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]O-Level Education[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1992[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]1995[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]SECONDARY[/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 4"] CERTIFICATIONS [/TD]

[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"] Certification Name or Type [/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"] Certification No. [/TD]
[TD="bgcolor: #b4c6db"] Issued [/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"] Expires [/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 4"] EMPLOYMENT HISTORY [/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db"] Company Name [/TD]
[TD="bgcolor: #b4c6db"] Position [/TD]
[TD="bgcolor: #b4c6db"] From Date [/TD]
[TD="bgcolor: #b4c6db"] To Date [/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 4"] POLITICAL EXPERIENCE [/TD]

[TD="class: text_menu"]Ministry/Political Party/Location[/TD]
[TD="class: text_menu"]Position[/TD]
[TD="class: text_menu"]From[/TD]
[TD="class: text_menu"]To[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"]CHADEMA[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]Member - District Management Committee[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"]2007[/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 2"] PUBLICATIONS [/TD]

[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Description[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Published Date[/TD]

[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]
[TD="bgcolor: #e9f0f0"][/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 4"] SPECIAL SKILLS [/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db"]Skill Name or Description[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Years Experience[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Acquired Through[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Skill Level[/TD]

[TD="bgcolor: #edeeee"][/TD]
[TD="bgcolor: #edeeee"][/TD]
[TD="bgcolor: #edeeee"][/TD]
[TD="bgcolor: #edeeee"][/TD]

[TD="bgcolor: #b4c6db, colspan: 5"] RECOGNITIONS [/TD]

[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Recognition Type[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Recognition Date[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Reason[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Action Taken[/TD]
[TD="class: text_menu, bgcolor: #b4c6db"]Issued by[/TD]

[TD="colspan: 7"] No items on list [/TD]

Usiache kupitia na hapa gamba.........
Parliament of Tanzania

http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcvs.php?vpkey=179

http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcvs.php?vpkey=228

[url]http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcvs.php?vpkey=228

[/URL]
 
Vicent amenajisi elimu kumpa ukampeni meneja Arumeru kama chadema watashinda wategemee CCM kukata rufaa kwa maneno yake likiwemo la Mkapa alimuua Nyerere.

likiwemo la mkapa aliimua nyerere!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom