Kwa bei hizi za korosho 2019 / 2020 tutarajie lolote kutoka kwa Rais Magufuli?

Amani kwetu,

Leo kumefanyika mnada wa kwanza wa korosho huko Masasi na Newala. Huu ukiwa ni mnada wa kwanza kabisa tangu uamuzi wa serikali kununua korosho mwaka jana kufuatia bei hafifu.

Msimu huu bei zimeanzia 2,100 hadi 2,500. Bei hizi kwa kweli bado sio rafiki kwa mkulima kwa ntazamo wa rais wetu.

Wakulima hawa wanyonge kwa utaratibu wa sasa watakumbwa na makato kadhaa hivyo kupunguza mapato tarajio.

Nimeuombe mh Rais Magufuli arudi tena kuwatazama wakulima hawa,ikiwezekana asitishe ama afute kabisa makato haya kwa mkulima.

Kwa msimu huu wa korosho bado mambo yatakuwa kwa wastani..

Tunawatakia heri wakulima wote wa korosho pamoja na vyombo vyote vinavyosimamia na kuunga mkono juhudi za wakulima wa korosho.
Mmekwishaanza kupanga mipango ya dhuluma kudadeki ! wakulima siyo wajinga sana !
 
Mkuu acha tu huo mzimu wa koro show, hawatausahau wao walidhania ni kitu rahisi tu!!! Bado kuna watu hadi leo nimeangalia kwenye tv, kuna watu hawajalipwa pesa zao!!
Kangomba ndio wamekua wa mwisho kulipwa ila wakulima wa kawaida walishalipwa siku nyingi tu
 
Amani kwetu,

Leo kumefanyika mnada wa kwanza wa korosho huko Masasi na Newala. Huu ukiwa ni mnada wa kwanza kabisa tangu uamuzi wa serikali kununua korosho mwaka jana kufuatia bei hafifu.

Msimu huu bei zimeanzia 2,100 hadi 2,500. Bei hizi kwa kweli bado sio rafiki kwa mkulima kwa ntazamo wa rais wetu.

Wakulima hawa wanyonge kwa utaratibu wa sasa watakumbwa na makato kadhaa hivyo kupunguza mapato tarajio.

Nimeuombe mh Rais Magufuli arudi tena kuwatazama wakulima hawa,ikiwezekana asitishe ama afute kabisa makato haya kwa mkulima.

Kwa msimu huu wa korosho bado mambo yatakuwa kwa wastani..

Tunawatakia heri wakulima wote wa korosho pamoja na vyombo vyote vinavyosimamia na kuunga mkono juhudi za wakulima wa korosho.
Tunaenda hatua 8 mbele na kurudi 10 nyuma alafu tu ajipongeza.Kiukweli amefeli kwenye hili zao.
 
Mwaka Huu hawezi Kufanya huo upuuzi, kwa Kilicho mkuta msimu uliopita ndio maana Akatangaza mapema kwamba mwaka huu Hatanunua ila atasimamia tu.
Yaani kutoka kupewa bei ya kilanguzi 1900 mpaka kupewa 3500 unauita upuuzi? Au wewe Kangomba?
 
Mi nadiriki kusema biashara ya korosho ndo kiboko ya jeuri na ngebe za Jiwe. Alidhani angejipatia mtaji wa kisiasa wa "mtetezi wa wanyonge" kupitia korosho "alipojishebedua" kuwazuia wafanyabiashara kununua zao hilo kwa bei ya chini ya sh.3000 kwa kilo.

Alipiga marufuku na kuharamisha biashara ya korosho kwa mtindo wa kangomba. Zaidi alchofanya ni kuzuia malipo kwa wote waliojikusanyia korosho kwa "njia haramu" ya kangomba.

Bali katika kuonesha msisitizo wa "uharamu" wa biashara ya kangomba, alipozuri mkoani Mtwara mwezi April mwaka huu, Jiwe aliwataka wafanyabiashara wa kangomba, ili wapate malipo yao, "watubu" kwa maandishi kuwa walijipatia korosho kwa njia haramu na kwamba hawatarudia tena .

Nasema biashara ya korosho ni "mbabe" wa Jiwe kwasababu imemtoa "ngeu" na sasa anaiogopa. Serikali yake "imegwaya" na imekiri haitathubutu tena "mziki" wa korosho. Matokeo yake ndo kama hivi; bei imeshuka kutoka sh. 3300 anayoipenda Jiwe na biashara ya kangomba inaendelea kama kawa. Ile toba kwa maandishi ya kutokurudia biashara ya kangomba si chochote si lolote kwa msimu huu bali serikali inaogopa kuwapiga marufuku.
Lengo la Rais lilikua maslahi bora kwa wakulima, kwani yeye ni mfanya biashara wa korosho mpaka uliweke hili soo personal? Mbona kama unafikiri ikinunuliwa pungufu ya 3k ni Rais anaumia sana? Yeye mshahara wake mbona upo pale pale tu

Rais alitaka wakulima wapate maslahi mazuri na alifanikiwa kwenye hilo na kwa taarifa yako tu ni kwamba suluhu ya hili ni kuwa na kiwanda kikubwa cha kubangua korosho zote zinazozalishwa Tanzania, kama mambo yataenda sawa 2022 kitakua tayari kinafanya kazi
 
Kama rais alilazimika kuingiza serikali kwenye biashara ya korosho ili kulinda maslahi ya mkulima, kwanini msimu huu imejitoa na imeshindwa hata kutoa bei elekezi? Je, kwanini serikali ilitangaza kuwa biashara ya kangomba ni haramu na bado msimu huu inafanyika? Je, serikali inasimammiaje maslahi ya mkulima?
 
Mi nadiriki kusema biashara ya korosho ndo kiboko ya jeuri na ngebe za Jiwe. Alidhani angejipatia mtaji wa kisiasa wa "mtetezi wa wanyonge" kupitia korosho "alipojishebedua" kuwazuia wafanyabiashara kununua zao hilo kwa bei ya chini ya sh.3000 kwa kilo.

Alipiga marufuku na kuharamisha biashara ya korosho kwa mtindo wa kangomba. Zaidi alchofanya ni kuzuia malipo kwa wote waliojikusanyia korosho kwa "njia haramu" ya kangomba.

Bali katika kuonesha msisitizo wa "uharamu" wa biashara ya kangomba, alipozuri mkoani Mtwara mwezi April mwaka huu, Jiwe aliwataka wafanyabiashara wa kangomba, ili wapate malipo yao, "watubu" kwa maandishi kuwa walijipatia korosho kwa njia haramu na kwamba hawatarudia tena .

Nasema biashara ya korosho ni "mbabe" wa Jiwe kwasababu imemtoa "ngeu" na sasa anaiogopa. Serikali yake "imegwaya" na imekiri haitathubutu tena "mziki" wa korosho. Matokeo yake ndo kama hivi; bei imeshuka kutoka sh. 3300 anayoipenda Jiwe na biashara ya kangomba inaendelea kama kawa. Ile toba kwa maandishi ya kutokurudia biashara ya kangomba si chochote si lolote kwa msimu huu bali serikali inaogopa kuwapiga marufuku.
Hawana nguvu ya kuwapiga marufuku kwanza wakulima wengi bado awajalipwa 70% japo naskia wanalipa kwa speed ndogo.
 
Kama rais alilazimika kuingiza serikali kwenye biashara ya korosho ili kulinda maslahi ya mkulima, kwanini msimu huu imejitoa na imeshindwa hata kutoa bei elekezi? Je, kwanini serikali ilitangaza kuwa biashara ya kangomba ni haramu na bado msimu huu inafanyika? Je, serikali inasimammiaje maslahi ya mkulima?
Kwa upande wa maslai wakulima bd awajalipwa n bora wangekubali mnada.
 
Kama rais alilazimika kuingiza serikali kwenye biashara ya korosho ili kulinda maslahi ya mkulima, kwanini msimu huu imejitoa na imeshindwa hata kutoa bei elekezi? Je, kwanini serikali ilitangaza kuwa biashara ya kangomba ni haramu na bado msimu huu inafanyika? Je, serikali inasimammiaje maslahi ya mkulima?
Serikali inajua jinsi wakulima wanavyodhulumiwa na walanguzi na ipo kwenye UTEKELEZAJI wa kudumu kwenye kuondoa hii kero, kiwanda ndio jawabu tosha na hilo lipo kwenye hatua nzuri.
 
aingilie kati kwani hajipendi,watu wamechafukwa na waliofanyiwa msimu uliopita,madeni hajamaliza.
 
Mwaka huu machale yakinicheza Mapema ndiyo maana nilikacha kununua Kwa kangomba.
Jamaa zangu wamenunua tsh 2000/= Kwa kangomba moja wakitegemea kuuza Kwa tsh 3000/= sasa Kwa style hii naona hasara inaanza mapema
Kangomba moja Ina ujazo wa kilo 2 mkuu,.. Hapo kwao ni kicheko tu
 
Serikali inajua jinsi wakulima wanavyodhulumiwa na walanguzi na ipo kwenye UTEKELEZAJI wa kudumu kwenye kuondoa hii kero, kiwanda ndio jawabu tosha na hilo lipo kwenye hatua nzuri.
Kwahiyo kwa mwaka huu mkulima ataendelea kunyonywa kwa bei ndogo za minada na kangomba kama kawaida hadi hapo hicho kiwanda kitakapo kamilika. Jebu tuambie hicho kiwanda kitakamilika lini? Lakini kwanini msimu wa mwaka juzi korosho ilinunuliwa kwa zaidi ya sh 4000 kwa kilo bila kuwepo kwa hicho kiwanda?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom