Kwa bei hizi za korosho 2019 / 2020 tutarajie lolote kutoka kwa Rais Magufuli?

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Amani kwetu,

Leo kumefanyika mnada wa kwanza wa korosho huko Masasi na Newala. Huu ukiwa ni mnada wa kwanza kabisa tangu uamuzi wa serikali kununua korosho mwaka jana kufuatia bei hafifu.

Msimu huu bei zimeanzia 2,100 hadi 2,500. Bei hizi kwa kweli bado sio rafiki kwa mkulima kwa ntazamo wa rais wetu.

Wakulima hawa wanyonge kwa utaratibu wa sasa watakumbwa na makato kadhaa hivyo kupunguza mapato tarajio.

Nimeuombe mh Rais Magufuli arudi tena kuwatazama wakulima hawa,ikiwezekana asitishe ama afute kabisa makato haya kwa mkulima.

Kwa msimu huu wa korosho bado mambo yatakuwa kwa wastani..

Tunawatakia heri wakulima wote wa korosho pamoja na vyombo vyote vinavyosimamia na kuunga mkono juhudi za wakulima wa korosho.

Updates:

Wakuu wa mikoa Mtwara na lindi pamoja na wakuu wa wilaya zote waitwa dar,wafanya kikao kizito.

Hongera serikali kwa kuwakaribu na wakulima.

Acha Kulazimisha Jambo, Kwenye Biashara siku Zote Suala La Bei Kupanda Au Kushuka Ni Vitu Vya Kawaida Kutegemea Na Hali Ya Soko.

Huwezi Kumlazimisha Mfanya Biashara Anunue Bidhaa Kwa Bei Kubwa Wakati Bei Iliyopo Sokoni Sio Rafiki Kwake.

Mwaka Juzi Waliponunua Korosho Zaidi Ya 3500 Kwa Kilo Kwani Kuna Kiongozi Au Mtu Yoyote Aliwalazimisha Kufanya Hivyo?.

Nb: Ikiwa Mafuta Kuna Kipindi Yanashuka Bei Iweje Korosho Zipande Bei Siku Zote?.
 
Wanunuzi ni wahindi na Thailand ila kuanzia mwaka Jana minada yote walijipanga wahindi mpaka magufuli alipoingilia Kati akanunua mwenyewe..
Kuanzia masasi,tunduru,newala na Tandahimba wamejaa wahindi tupu wa korosho kwenye msimu huu
Wahindi sio watu.
 
Acha Kulazimisha Jambo, Kwenye Biashara siku Zote Suala La Bei Kupanda Au Kushuka Ni Vitu Vya Kawaida Kutegemea Na Hali Ya Soko.

Huwezi Kumlazimisha Mfanya Biashara Anunue Bidhaa Kwa Bei Kubwa Wakati Bei Iliyopo Sokoni Sio Rafiki Kwake.

Mwaka Juzi Waliponunua Korosho Zaidi Ya 3500 Kwa Kilo Kwani Kuna Kiongozi Au Mtu Yoyote Aliwalazimisha Kufanya Hivyo?.

Nb: Ikiwa Mafuta Kuna Kipindi Yanashuka Bei Iweje Korosho Zipande Bei Siku Zote?.
shida ni kuanza kupeleka vifaru vya jeshi katikati ya masuala ya biashara!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom