Kuzorota kwa Huduma/Shirika gani litakufanya usiipigie tena kura CCM?

Black Opal

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
201
263
Wakuu swalama?

Kuzorota kwa huduma gani au shirika gani kutafanya usiipigie tena kura CCM ikafie mbele?

1. Kwakweli kwangu TANESCO ni namba moja, naashum TANESCO ni mbunge, anafanana na yule aliyeimbwa na Nakasya Sumari, yaani TANESCO ni zaidi ya garasa, halifai kwa lolote.

2. Ya pili ni huduma ya Intaneti, 1000 unapata MB 450 kwa siku, yaani ukikohoa tu hata hujafungua simu zimeisha! Tupo kwenye ulimwengu ambao bila internet michongo haiendi, halafu tunapata huduma hii kwa gharama kubwa hivi ni kweli mnataka Tanzania ipige hatua? CCM ikikosa kura bwana Nape Nnauye jua na wewe umesababisha chama chako kuangukia pua.

3. Suala la miundombinu hasa barabara, jamani jamani, hapa ndio kichomi kabisa. Barabara zinajengwa kwa kiwango kibovu sababu rushwa zimejaa kwenye tenda lakini pia ni makusudi ili kuwe na matengenezo ya mara kwa mara watu wajipigie hela.

4. Huduma ya maji, hapo kwanza ncheke! Kama hujabambikiwa bili basi maji hakuna, ukibahatisha yamemetoka linakuja vumbi la maana ambalo nalo sio kwamba hulilipii! Yaani ukisimama nchale, ukigeuka nchale ukilala nchale na ukikaa nchake, piga pigo zote mwisho wa siku unaambulia kibuyu.

Je, wewe ni shirika/huduma gani ambayo kila ukiifikiria unasema hapa CCM lazima niile kichwa?
 
B.O.T >>Wameshindwa kuja na sera ya kuzuia thamani Tsh kuporomoka
>>wameshindwa dhibiti mashirika yenye kutoa mikopo umizi/firisi

CMSA>>Wameshindwa weka sera ya kushawishi makampuni mengi yawe Public kwenye DSE

NHC>>>>wameshindwa kuja na mradi wa makazi wenye kujenga Vijana Maskini wanaonza maisha.
>>Kujenga nyumba za makazi Packers,badala ya ukumbuke za matamasha.
 
Alternative ya kutoipigia kura ccm iko wapi? Kutokwenda kupiga kura?
Kutokwenda kupiga kura unaweza kujikuta kichaa kachaguliwa na vichaa wenzie kuwa rais, utamlaumu nani?
 
Hata ukienda kupiga kura ni kupoteza muda maana kura haziheshimiwi. Labda machafuko au mapinduzi ya kijeshi, lakini kupiga kura kwa tume na katiba hii, ni matumizi mabaya ya raslimali muda.
 
Nitajie shirika au taasisi yoyote chini ya serikali ya ccm ambayo haijazorota!!
 
Tatizo sio TANESCO, ni Sheria za umeme Tanzania, ni kama mpaka Leo TTCL ingekuwa ndio kampuni inayoruhusiwa kufanya bishara ya simu Tanzania na hakuna nyingine,unazuia investment wakati huna hela ya kuwekeza, umaskini mwingine ni wa kujitakia tuu, serikali ya CCM imejaza wajinga watupu
 
Kwani huko upinzani wanafanya nini cha maana cha kutufanya tusiwaone nao siyo wapumbavu watupu?
Tatizo la Tanzania siyo tatizo la kiitikadi au kichama, ni tatizo la kijamii. Lingekuwa ni tatizo la kiitikadi basi wapinzani wangeshajipambanua na kufanya mambo kwa ufanisi ili kujitofautisha na ccm. Lakini sasa, watanzania ni wale wale!
 
pamoja na matatizo ya kijamii mengine ya uoinzani,vyombo vya dola kupendelea upande kwenye uchaguzi nalo ni tatizo la kijamii,mnasemaje hapo?
 
Wakuu swalama?

Kuzorota kwa huduma gani au shirika gani kutafanya usiipigie tena kura CCM ikafie mbele?

1. Kwakweli kwangu TANESCO ni namba moja, naashum TANESCO ni mbunge, anafanana na yule aliyeimbwa na Nakasya Sumari, yaani TANESCO ni zaidi ya garasa, halifai kwa lolote.

2. Ya pili ni huduma ya Intaneti, 1000 unapata MB 450 kwa siku, yaani ukikohoa tu hata hujafungua simu zimeisha! Tupo kwenye ulimwengu ambao bila internet michongo haiendi, halafu tunapata huduma hii kwa gharama kubwa hivi ni kweli mnataka Tanzania ipige hatua? CCM ikikosa kura bwana Nape Nnauye jua na wewe umesababisha chama chako kuangukia pua.

3. Suala la miundombinu hasa barabara, jamani jamani, hapa ndio kichomi kabisa. Barabara zinajengwa kwa kiwango kibovu sababu rushwa zimejaa kwenye tenda lakini pia ni makusudi ili kuwe na matengenezo ya mara kwa mara watu wajipigie hela.

4. Huduma ya maji, hapo kwanza ncheke! Kama hujabambikiwa bili basi maji hakuna, ukibahatisha yamemetoka linakuja vumbi la maana ambalo nalo sio kwamba hulilipii! Yaani ukisimama nchale, ukigeuka nchale ukilala nchale na ukikaa nchake, piga pigo zote mwisho wa siku unaambulia kibuyu.

Je, wewe ni shirika/huduma gani ambayo kila ukiifikiria unasema hapa CCM lazima niile kichwa?
Nani aliua Tanganyika Parkers?
Nani aliua Ranchi za Taifa?
Loliondo nani kaiuza?
Thanda Island kauza nani?
Hayo mashirika goigoi chini ya utawala upi?

Kinachotakiwa ni kuiondoa CCM uchaguzi ukija. Hiki chama ndicho mzizi wa uozo wote nchini
 
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA.Hii taasisi haijakidhi kabisa malengo ya uwepo wake.Ni moja ya taasisi ambayo tangu kuanzishwa kwake inaakisi matumizi mabaya ya pesa za umma.CCM hoiiii.
 
Hata ukienda kupiga kura ni kupoteza muda maana kura haziheshimiwi. Labda machafuko au mapinduzi ya kijeshi, lakini kupiga kura kwa tume na katiba hii, ni matumizi mabaya ya raslimali muda.
Si kweli, wananchi tukiungana hata jiyohiyo tume ya uchaguzi ya mchongo itadeliver tunachotaka
 
Kipi kinachowafanya msiungane, miaka zaidi ya 30 Sasa, bado chaguzi zetu haziheshimiwi kwa ridhaa ya wananchi. Au mtaungana baada ya miaka mingapi Ili tume iwajibike?
 
Wakuu swalama?

Kuzorota kwa huduma gani au shirika gani kutafanya usiipigie tena kura CCM ikafie mbele?

1. Kwakweli kwangu TANESCO ni namba moja, naashum TANESCO ni mbunge, anafanana na yule aliyeimbwa na Nakasya Sumari, yaani TANESCO ni zaidi ya garasa, halifai kwa lolote.

2. Ya pili ni huduma ya Intaneti, 1000 unapata MB 450 kwa siku, yaani ukikohoa tu hata hujafungua simu zimeisha! Tupo kwenye ulimwengu ambao bila internet michongo haiendi, halafu tunapata huduma hii kwa gharama kubwa hivi ni kweli mnataka Tanzania ipige hatua? CCM ikikosa kura bwana Nape Nnauye jua na wewe umesababisha chama chako kuangukia pua.

3. Suala la miundombinu hasa barabara, jamani jamani, hapa ndio kichomi kabisa. Barabara zinajengwa kwa kiwango kibovu sababu rushwa zimejaa kwenye tenda lakini pia ni makusudi ili kuwe na matengenezo ya mara kwa mara watu wajipigie hela.

4. Huduma ya maji, hapo kwanza ncheke! Kama hujabambikiwa bili basi maji hakuna, ukibahatisha yamemetoka linakuja vumbi la maana ambalo nalo sio kwamba hulilipii! Yaani ukisimama nchale, ukigeuka nchale ukilala nchale na ukikaa nchake, piga pigo zote mwisho wa siku unaambulia kibuyu.

Je, wewe ni shirika/huduma gani ambayo kila ukiifikiria unasema hapa CCM lazima niile kichwa?
Suala la pensheni za wazee kuwa robo
 
Kipi kinachowafanya msiungane, miaka zaidi ya 30 Sasa, bado chaguzi zetu haziheshimiwi kwa ridhaa ya wananchi. Au mtaungana baada ya miaka mingapi Ili tume iwajibike?
Idadi inabidi iwe nyingi watanzania wengi ni jau sana huku mtaani, na kundi lingine kubwa kama nyinyi mliokata tamaa kabisa na uchaguzi, ndo maana tunakwama
 
Kwa taarifa yako Mimi sijakata tamaa na uchaguzi, bali nimeupuuza. Ww ambaye bado unaamini kwenye huo upuuzi, waunganishe watu. Mimi nahamasisha watu wasipoteze muda kushiriki huo uhuni, tutapata njia nyingine ya kupata viongozi hata kama itakuwa ni kwa maumivu.
 
Back
Top Bottom