Uchaguzi 2020 Takwimu hazidanganyi: CCM wameshashinda Uchaguzi kwa Idadi ya Kura za Kanda ya Ziwa

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Ni kama ambavyo wakati wote nimesisitiza kuwa Uchaguzi ni maarifa, mipango na akili, hakuna kitu kina guarantee ushindi katika mpambano wa kisiasa kama kuchanga karata zako vyema, na kwa kuitazama CCM chama changu, ni wazi kuwa Viongozi wake na Mgombea mwenyewe amejipanga vyema sana. Leo nitafafanua eneo moja tu la RATIBA ya Mgombea na namna inavyomsaidia kumaliza hii game mapema.

Mikoa ambayo Mgombea wa CCM aliyokwishapita na kupata mapokezi ya kuridhisha ni pamoja na Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mara, Mwanza na leo anapokelewa nyumbani Geita. Ratiba hii inamkutanisha Mgombea na takribani wapiga kura 11.2 M ambapo Dom (1.33 M) Singida (0.85M) Tabora (1.5M) Shinyanga (1M) Simiyu (0.9) Mara (1.1) Mwanza (1.9) Geita (1.21) Kagera (1.4M).

Based on voters behaviour katika ya wananchi 29M waliojiandikisha, ni wananchi kati ya 12 - 16M watajitokeza kupiga kura mwaka huu, Ikiwa magufuli tayari anakura takribani 11M, ni wazi kuwa tayari Ndugu Magufuli ni Rais anayesubiri kuapishwa.

Mapokezi yanayoonekana kimsingi yana reflect uhalisia wa watu wa jamii ile wanapompenda mtu huwa hawawezi kujificha, ukweli ni kuwa MAGUFULI anapendwa sanaaaa na jamii ya watu wa Kanda ya Ziwa, utetezi kuwa watu wanabebwa na malori na kulazimishwa kuhudhuria mikutano ya Mgombea Urais huyo ni Upuuzi unaopaswa kupuuzwa, U can't stage watu vijijini wanaojaza umati kwenye mabarabara., ingekuwa ni Rais hivyo basi na Upinzani wangeweza kufanya tu, badala ya kupata aibu wanayokutana nayo akina Lissu huko Dodoma na KibandaMaiti ama Aibu anayokutana nayo Mzee wangu Membe.

data.JPG

Takwimu zinaonyesha kuwa voters behaviour katika chaguzi ambazo Mgombea wa CCM anaendelea (Kwa maana ya Mgombea ambae ni Rais) hamasa ya wapiga kura inapungua na kwa mwaka 2010 ambapo Mheshimiwa Jakaya Kikwete alikuwa anaendelea na awamu yake ya pili waliojiandikisha walikuwa 20.1M na waliopiga kura ni 8.6M tu sawa na 42%, mwaka 2015 waliojiandikisha walikuwa 24.6 M waliopiga kura ni 15M tu. Kwa behaviour hiyo tunategemea kuwa mwaka huu pia ni kati ya asilimia 40%- 50% watajitokeza kupiga kura.

Tabia ya wapiga kura wa kanda ya ziwa ni kuwa wana msimamo, mwaka 2015 Mikoa ambayo Ndugu Magufuli alipata kura nyingi ukiacha Dodoma mingine yote ni mikoa ya Kanda ya Ziwa (Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga n.k) na kutokana na tabia ya jamii hiyo kutobadilika ni wazi mwaka huu pia watamchagua tena Magufuli.

Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na Ahadi za Rais katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ni kielelezo kingine cha wazi kabisa kuwa Wananchi wa Kanda hiyo wameuona na kushuhudia WEMA wa Rais Magufuli kwao, amejenga miundombinu na huduma za kutosha mpaka wapinzani wakaona waitumie propaganda kuwa Kanda hiyo inapendelewa na kuonyesha choyo kwa watu hao (Hoja nyingine ya kuwanyima Kura) na kwa kweli jamii hiyo ya watu wanajua kukirimu mtu aliyewafanyia wema. Magufuli ni mwema sana kwao, watampa kura nyingi.

Hoja ya Uzawa bado ina nguvu katika Siasa za Nchi yetu, pamoja na ukweli kuwa hatuchaguani kwa UKABILA lakini hoja ya Uzawa na Uenyeji ni kigezo tosha cha kupata kura katika maeneo mengi nchini, wale waliokuwa watia nia wanalijua hili kwa uhalisia baada ya kukutana na hasira za wajumbe ambao waliwaona kuwa wao ni wageni kwani wengi walitoka Dar kwenda kugombea Vijijini, WALIKATALIWA kwa hoja ya Uenyeji na Uzawa, magufuli ni Mzawa na mwenyeji wa Kanda ya Ziwa, ni mtoto wao...na mcheza kwao hutuzwa.

Pamoja na takwimu kuonyesha kuwa watanznaia katika kipindi cha uchaguzi wa marudio na ule wa Mgombea akiwa Rais hawajitokezi sana kupiga kura kwa maana hamasa yao ya kushiriki siasa iko chini sana, imeonyesha tofauti kwa wapiga kura wa Kanda ya Ziwa, Mwaka 2015 takwimu zimeonyesha asilimia 86.7% ya waliojiandikisha walipiga kura, wakati maeneo mengine yakionyesha asilimia kati ya 50% na 60% ndio waliojitokeza kupiga kura.

RATIBA ya WAGOMBEA wa UPINZANI
Lissu alianza Vibaya sana DAR (wakafukuza wanahabari), akaenda kuharibu ARUSHA (wakasingizia mechi ya Simba) akaenda kupata mapokezi hafifu MWANZA (comparing to Magufuli) akaenda kujiliza SHINYANGA, akanyanyapaliwa TABORA na akapata aibu ya mwaka DODOMA, akafutwa machozi MBEYA na baadae akachungulia Kaburi KIBANDA MAITI - ZANZIBAR ambapo ilibidi aombe msaaad wa ACT kuita watu na kukaribisha Viongozi wao kuhutubia na akaishia kumuombea kura Maalim.... Katika mikoa takribani 10 aliyotembelea Lisu amepata mapokezi ya kuridhisha MBEYA tu.
1599552018530.png


Mbobezi naona amekata moto kabisa, ratiba yao ilionyesha Uzinduzi LINDI, walipaswa kuwa MTWARA baada ya hapo, Kisha RUVUMA na baadae NJOMBE. Kimsingi huyu Mzee hajatoka nje ya LINDI, yupo anapiga kampeni za Kata za Lindi ambazo mahudhurio yake yanachekesha na kimsingi anajutia maamumzi yake, BIG TIME..yaani nimemuona ametoka Nje ya Lindi kituo kilichofuata ilikuwa ni kipindi cha Dakika 45 cha ITV....Aibu.
IMG-20200908-WA0054.jpg



Narudia tena Kampeni ni maarifa, mipango na akili na wapinzani wamepungukiwa na vyote...!!
 
Wapinzani wanajua kabisa hawapiti isipokua sasa zile pesa walizopata kupitia ruzuku zinakaguliwa na CAG lazima zionekane zimetumikaje. Hapo ndipo watu wanapopiga pesa sasa mwisho wa siku wewe mlala hoi unaenda kupigwa kwenye maandamano unapigwa na jua mchana ili yaonekane mafuriko lakini wengine wameishavuta mipigo yao wametulia kimya. Wanapiga kwenye utengenezaji wa tshirt, kofia, kuandaa magri ya muziki, kupamba jukwaa nk
 
Usijidanganye kuwa Magufuli anakubalika kanda ya ziwa kwa lile tamasha. Mkoa wa mara ni nusu kwa nusu, Mkoa wa Kagera hawataki kumsikia kwa matusi yake wakati wa tetemeko.

Hata kwao geita hakubaliki kivile, turufu yake iko Mwanza na anatumia mbinu ya kuongea kisukuma mikutanoni wakati ye kazaliwa Chato, wilaya Biharamulo, mkoa wa Kagera, kabila msubi. Aliileta Chato geita kimkakati baada ya kuwa apendwi kule Biharamulo
 
Ni kama ambavyo wakati wote nimesisitiza kuwa Uchaguzi ni maarifa, mipango na akili, hakuna kitu kina guarantee ushindi katika mpambano wa kisiasa kama kuchanga karata zako vyema, na kwa kuitazama CCM chama changu, ni wazi kuwa Viongozi wake na Mgombea mwenyewe amejipanga vyema sana. Leo nitafafanua eneo moja tu la RATIBA ya Mgombea na namna inavyomsaidia kumaliza hii game mapema...
Kweli Tundu Lissu kawashika MATAGA kunako....

Lissu shikilia hapo hapo usilegeze baba - imeisha hiyo!
 
Kumekucha.. kwa siku zinavyokwenda.. mbili nane.. atashangaza sana..

Kwa utulivu wa mikutano ya uchaguzi.. na wapinzani kuwa wanafanya wanachotaka.. Hakika Magufuli ni chaguo la Mungu kwa nchi yetu hii pendwa..

Tunasukuma siku.. huko mbeleni hadi mbili saba.. kutakucha zaidi.. 💃🏽💃🏽💃🏽💃🏽 💯
 
Ni kama ambavyo wakati wote nimesisitiza kuwa Uchaguzi ni maarifa, mipango na akili, hakuna kitu kina guarantee ushindi katika mpambano wa kisiasa kama kuchanga karata zako vyema, na kwa kuitazama CCM chama changu, ni wazi kuwa Viongozi wake na Mgombea mwenyewe amejipanga vyema sana. Leo nitafafanua eneo moja tu la RATIBA ya Mgombea na namna inavyomsaidia kumaliza hii game mapema...
Umeelezea vizuri sana ndugu, Hakika Namba hazidanganyi
 
Usijidanganye kuwa magufuli anakubalika kanda ya ziwa kwa lile tamasha.mkoa wa mara ni nusu kwa nusu.mkoa wa kagera hawataki kumsikia kwa matusi yake wakati wa tetemeko.hata kwao geita hakubaliki kivile,turufu yake iko mwanza .na anatumia mbinu ya kuongea kisukuma mikutanoni wakati ye kazaliwa chato,wilaya biharamulo,mkoa wa kagera,kabila msubi .aliileta chato geita kimkakati baada ya kuwa apendwi kule biharamulo
Mwenzako kaleta takwimu,naww leta takwimu hapo tuone.
Tunasema"NAMBA HAZIDANGANYI"
 
Bila NEC na Polisi, Sisiemu ni sawa na "Kondomu" iliyotumika!
Kama mtu anajua hilo kwanini ushiriki uchaguzi ukijua fika hupati kitu?

Uroho ,ujinga na tamaa za kula bila kunawa ndio mtaji wa wale wanaotegemea miujiza.

Je kwanini vyama visisusie uchaguzi, huku wakijua wataambulia sifuri katika mazingira yasio na usawa?

Kama kutokea 1995 hadi 2020,bado tunategemea huruma badala ya Tume huru na katiba ya Warioba,kuna haja gani ya kuendelea kujidanganya na wagombea wa upinzani kuwa watashinda?
 
Usijidanganye kuwa magufuli anakubalika kanda ya ziwa kwa lile tamasha.mkoa wa mara ni nusu kwa nusu.mkoa wa kagera hawataki kumsikia kwa matusi yake wakati wa tetemeko.hata kwao geita hakubaliki kivile,turufu yake iko mwanza .na anatumia mbinu ya kuongea kisukuma mikutanoni wakati ye kazaliwa chato,wilaya biharamulo,mkoa wa kagera,kabila msubi .aliileta chato geita kimkakati baada ya kuwa apendwi kule biharamulo
hahahha........
Magufuli kawashika Pabaya aseh naona hali tete
 
Back
Top Bottom