Kuzaa mtoto mmoja

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
15,819
22,920
Wana JF

Mimi mwenzenu nina mtoto mmoja tu, na huu ulikuwa ni mpango wa mimi na mke wangu kabla hata hatujaoana. Mtoto wetu sasa ni mkubwa ana miaka 14, I am not regreting for that and we are all quite happy.

Sasa kinachonishangaza mimi ni kuwa inakuwa kama kero, yaani nikutana na ndugu, marafiki, ninapokuwa kazini na hata watu wangine tu nisio na uhusiano nao wa karibu wamekuwa wakinilaumu mimi hata mke wangu "kwanini mmezaa mtoto mmoja tu si muongeze angalau mwingine"!

Hili neno kwangu sasa naona ni kama kero. Hebu nishaurini jamani, hawa watu niwape majibu gani ili niwaridhishe?
 
Waeleze kua ressources zenu (time, emotional, financial, supervison, quality time etc) zinawaruhusu ku-focus vipaswavo kwa mtoto mmoja tu. Maybe ukumbuke kwa nini mliamua hivo in the first place and share that with them. but all in all the easiest way ni kuwaambia: haya masuali yamekua kero sasa (as you have expressed it).
 
hahahaa, mimi kabla sijaolewa nilikuwa nawaambia kwamba nataka zaa watoto sita, hadi leo nina mmoja na wamesema hawajachoka na wanaendelea kusema.
 
Jibu liko kwenye thread yako tayari yaani wewe wajibu:- "huu ulikuwa ni mpango wa mimi na mke wangu kabla hata hatujaoana. Am not regretting for that and we are all quite happy". Ila kusema ukweli sidhani kama haya maneno uliyoandika kwa kiingereza yana ukweli sana ndani yake. Yangekuwa kweli usingepata shida kuwaelimisha hao wanaokuuliza na wala isingekuwa kero kwako kuulizwa mara kwa mara.
 
Wana JF mimi mwenzenu nina mtoto mmoja tu,na huu ulikuwa ni mpango wa mimi na mke wangu kabla hata hatujaoana,mtoto wetu sasa ni mkubwa ana miaka 14,am not regreting for that and we are all quite happy,sasa kinachonishangaza mimi ni kuwa inakuwa kama kero,yaani nikutana na ndugu,marafiki,ninapokuwa kazini na hata watu wangine tu nisio na uhushiani nao wa karibu wamekuwa wakinilaumu mimi hata mke wangu "kwanini mmezaa mtoto mmoja tu si muongeze angalau mwingine",hili neno kwangu sasa naona ni kama kero kwangu,hebu nishaurini jamani hawa watu niwape majibu gani ili niwaridhishe.


Haya maneno ya kizungu haya!!!!!! Sidanganyiki. Kama hujutii jambo hauhitaji vuvuzela kuwajulisha watu kuwa hujutii. Watu wataona tu kwa vitendo vyako. Nadhani wanaokuuliza wanahisi ama kwa maneno au vitendo vyako kuwa una regret kuwa na mtoto mmoja pekee.
 
Nadhani utaelewa tu siku moja kwanini wanakwambia hivo, yaweke haya maneno yangu.

Acha uchuro mkuu, ni uamuzi wa mtu/watu kuwa na idadi ya watoto kulingana na uwezo wa kutunza....sisi Waafrika/ Wabongo tunang'ang'ania kuwa na timu ya watoto matokeo yake ndio mara unakuta huyu katiwa mimba, kaka yake katia mimba mke wa mtu, mwingine sijui anavuta kitu ya Arusha halafu yule wa mwisho saa hizo yupo sijui Segerea.
 
Haya maneno ya kizungu haya!!!!!! Sidanganyiki. Kama hujutii jambo hauhitaji vuvuzela kuwajulisha watu kuwa hujutii. Watu wataona tu kwa vitendo vyako. Nadhani wanaokuuliza wanahisi ama kwa maneno au vitendo vyako kuwa una regret kuwa na mtoto mmoja pekee.
Na bado kila siku zikienda atalia kupoteza wakati wake kuzaa katoto kamoja tu...Wengine wanataka kushindana kupanga maisha wakati Mungu ndo anawapangia.
 
Kwanza tuambie sababu ya kuzaa mmoja halafu tukushauri cha kuwaambia waridhike
 
Kosa kubwa sana kuzaa mtoto mmoja sababu hatakuwa na mtu wa kumsupport siku za mbele...Hakuna kitu kama damu.

Wacheni kuwainga wahindi na wazungu wale kule njaa zinawasumbua.
"Fazaa, if you have a good pension scheme and if you have prepared you retreat you won't need to be a burden for your kids in your old age.
 
Acha uchuro mkuu, ni uamuzi wa mtu/watu kuwa na idadi ya watoto kulingana na uwezo wa kutunza....sisi Waafrika/ Wabongo tunang'ang'ania kuwa na timu ya watoto matokeo yake ndio mara unakuta huyu katiwa mimba, kaka yake katia mimba mke wa mtu, mwingine sijui anavuta kitu ya Arusha halafu yule wa mwisho saa hizo yupo sijui Segerea.

Aliweka thread watu wachangie, nimesema yaliyo moyoni mwangu, usinilazimishe niseme unayoyataka wewe, hakuna uchuro wala nini, kama haregret kwanini ameweka humu? si anataka jibu? na kila mmoja atampa jibu analoona linafaa , namshauri kama ana uwezo wa kuzaa basi na aongeze wa pili, si vibaya . na asiwajibu watu vibaya kama nyie mnavomshauri maana mnataka kama awajibu vibaya flani vile au awadharau hao watu wanaomwambia, yeye kama ameamua hivo basi na akae kimya, kwanini atafute ushauri? sasa kama ameamua kutafuta ushauri basi na akubali mawazo ya watu tofauti wanasema nini!
 
Back
Top Bottom