Kuzaa mtoto mmoja

Kwa raha zenu! As long as mko na furaha no problem..hao wanaokusumbua kwa kauli zao wapotezee..
 
Sioni shida kama mtaongeza mtoto mwingine. Hawa wanaokushauri kuwa usiwasikilize watu wanapokushauri kitu kwenye ndoa wanakupoteza tu, mbona uliwashirikisha ulipofunga.Leo wanapokuja kukushauri unakuwa mkali?. Tusidanganyane hapa kama sio sababu za 'magonjwa' na 'kipato' hakuna sababu zinginezo zinazokufanya usiongeze idadi provided Mungu ameruhusu.
Na kwa sababu umesema umekosa la kuwaambia hadi umekuja hapa JF, obvious hauathiriwi na hayo matatizo niliyoyataja hapo juu, na kwa vyovyote nao pia wangeona na wasingerudia kukuambia hii habari. Ushauri wangu..go for another child buddy!!
 
Mimi nina mtoto wa 3month but nishatamani kuwa na mwengine. Hivi akifika mwaka tu nabeba nyingine.
Sishauri hata kidogo mtu kuzaa mtoto mmoja. Km Mungu amekujalia uzazi hata wawili jamani.
 
mi sioni kwanini ukwazike kwa jambo ambalo wewe na mkeo mko comfortable nalo,ningeelewa kama ni otherwise. In your case hutakiwi kuliweka akilini ama hata kulitafutia ushauri kwa sababu halikusumbui. Wapotezee tu ndo dawa yao,na likiendelea kukusumbua sana bana itabiri urevisit maamuzi yako,itakuwa ni dalili ya uhitaji.
 
Kwa kuwa mlipanga tangia hapo awali yawezekana pia mkeo alisha funga kizazi na au kuondolewa kabisa kizazi hivyo hawezi kuzaa tena! Pole. Basi ushauri wangu waambie kila mtu na mipango yake ya maisha. Else ongeza mtoto my friend mtoto ni baraka kwenye familia.
 
huko uingereza kuna mama ana watoto 15 na anadai anataka wafikie 20.
Anadai yeye alizaliwa peke yake hivyo akawa mpweke wakati wa utoto hana hata mtu wa kucheza naye.Pia anadai alivyokuwa msichana alitegemea company ya marafiki na ikitokea yeye na best friend wake wamegombana anaishia kuwa mpweke sababu mama yake sio wa rika lake hivyo.
Anyway ni maisha yako mkuu,unaweza kuzaa wengi Mungu akawaita wote akabakia mmoja tu.
Mimi binafsi ningependa japo wawili watoto wangu wawe na mtu wakumuita dada au kaka,ndugu wa kuzaliwa naye tumbo moja hawezi kulingana na mpwa wala binamu.
 
For NO.1 am sorry that's too private,for NO.2 yaani kwa mapenzi tuliyonayo kwa mtoto wetu hakuna anaefikiria kuongeza mwingine kwani ni mambo ambayo huwa tunayaongea na hakuna anayejilaumu pia financially tunaona tunachokipata kinatosha kabisa kumtunza yeye (sasa na baadaye) na kuongeza mwingine ni kama kuharibu trend ambayo tumemuandalia,tuanapoona mtu ana kichanga tunaona tu ni wa-kwake kwani kwetu sisi ni stage ambayo tumeshaipitia na hatuhitaji tena kuirudia.for NO.3 wazo la kuwa na mtoto moja lilikuwa ni la kwangu na sukujali atakuwa wa jinsia gani,kwa mke wangu yeye alikuwa na option ya jinsia,kama angezaliwa wa jinsia hii.... itabidi tuongeze ili tupate wa jinsia anayoitaka ,ila kama takuwa wa jinsia ile aliyoitaka yeye alisema hatahitaji mwingine,luck enough akazaliwa wa jinsia aliyokuwa anaitaka na hapo ndio tukamaliza mchezo.

hapo kwenye namba moja ndio tatizo,mimi nilivyokusoma(nisamehe kama nimekosea) kwamba kuna kitu kinaendana na namba moja ambacho labda ulikifanya sasa unashindwa kujua kama ulikuwa sahihi au la!
 
huko uingereza kuna mama ana watoto 15 na anadai anataka wafikie 20.
Anadai yeye alizaliwa peke yake hivyo akawa mpweke wakati wa utoto hana hata mtu wa kucheza naye.Pia anadai alivyokuwa msichana alitegemea company ya marafiki na ikitokea yeye na best friend wake wamegombana anaishia kuwa mpweke sababu mama yake sio wa rika lake hivyo.
Anyway ni maisha yako mkuu,unaweza kuzaa wengi Mungu akawaita wote akabakia mmoja tu.
Mimi binafsi ningependa japo wawili watoto wangu wawe na mtu wakumuita dada au kaka,ndugu wa kuzaliwa naye tumbo moja hawezi kulingana na mpwa wala binamu.
queenkami tena asikudanganye mtu kuna mama yangu mkubwa alikuwa amezaa watoto wengi, sa kila aliye kuwa akizaa watu wakija muona anasema huyu atakuwa doctor, huyu pilot huyu mwalimu na Masha Allah wote wamekuwa vile.
 
queenkami tena asikudanganye mtu kuna mama yangu mkubwa alikuwa amezaa watoto wengi, sa kila aliye kuwa akizaa watu wakija muona anasema huyu atakuwa doctor, huyu pilot huyu mwalimu na Masha Allah wote wamekuwa vile.
FAZA mama yako ana bahati.
maana hapo juu kuna mtu nimeona kasema ukizaa wengi wanaishia kuwa majambazi na kuzalishwa hovyo.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa la wabongo ni life expectancy iko chini mno, yaani wanakuonea huruma in case of anything!

ni kweli huwez kujua mtt wenu mtaish nae had lini..also u never knw if atakua profesa au mvuta bng.so it's beta to have more children.
 
FAZA mama yako ana bahati.
maana hapo juu kuna mtu nimeona kasema ukizaa wengi wanaishia kuwa majambazi na kuzalishwa hovyo.
queenkami Inategemea unalea vipi watoto zako, kama uanwalea kwa ujambazi yataishia kuwa majambazi...ukiwalea kielimu wataishia kuwa wana elimu..Ikiwalea ki dini watakuwa wafata dini, ukiwalea kama wanavyo lea wahuni wataishia kuwa wahuni.
 
Wana JF mimi mwenzenu nina mtoto mmoja tu,na huu ulikuwa ni mpango wa mimi na mke wangu kabla hata hatujaoana,mtoto wetu sasa ni mkubwa ana miaka 14,am not regreting for that and we are all quite happy,sasa kinachonishangaza mimi ni kuwa inakuwa kama kero,yaani nikutana na ndugu,marafiki,ninapokuwa kazini na hata watu wangine tu nisio na uhushiani nao wa karibu wamekuwa wakinilaumu mimi hata mke wangu "kwanini mmezaa mtoto mmoja tu si muongeze angalau mwingine",hili neno kwangu sasa naona ni kama kero kwangu,hebu nishaurini jamani hawa watu niwape majibu gani ili niwaridhishe.

Watolee nje tu na wala wasiwakoseshe raha katika maisha yenu kwa kuwasakama na uamuzi wenu wa kuwa na mtoto mmoja. Hongereni kwa kutobadilisha maamuzi yenu.
 
Hivi mambo ya kuingilia maisha ya watu yanatoka wapi? watu ni mashuhuri sana kusema mtoto wa pili lini? ukipata wa pili wanauliza wa tatu, ukipata wa tatu wanauliza wa nne. Ukizaa mmoja tabu ukizaa wengi tabu. Hebu jamani maisha ya wanandoa wawaachie wanandoa.
 
I've born alone and I'm supporting myself and my family, I'm also happy to be alone.

Ungetumia tu lugha yetu adhimu ya kiswahili kumjibu ndugu fadhaa ambaye alijenga hoja kwa kiswahili. Ila kama uliona ni vyema kumjibu kwa hii lugha ya waingereza, ili kuonesha msisitizo, basi unngejaribu kuwaiga wenyewe wanavyoandika kwa ufasaha zaidi.
 
Nina hakika hata huyo mwanenu atakuwa ameanza kuwaomba apate ndugu yake wa damu,kama hajaanza pengine anachelea kuwaudhi akidhani hiyo imetokana na matatizo ya kizazi! Binafsi nnapenda niwe na ndugu yangu, na ndilo hilo watoto wengi wanapenda pia (huenda mwanenu akiwemo)!
 
Back
Top Bottom