Kuyaona mawazo yetu kama 'Kelele' ni kutudharau Watanzania

N
"Tulipoamua kupandisha Tozo za Miamala tulikuwa tuna lengo zuri tu ila tulipoanza kusikia Kelele za Wananchi basi Serikali tukaona kwakuwa tunawajali Wananchi wetu tuingilie kati na sasa nimeunda Kamati ili kuliangalia hili na itakuja na majibu muda si mrefu" Rais Samia.

Hasira yangu na Uchungu wangu zaidi haipo katika Kauli nzima bali ni hilo neno tu la 'Kelele' ambalo Mimi nalitafsiri kama vile Rais 'ametudharau' mno na kwamba anataka Watanzania tuwe ni Watu wa kukubali tu kila Kitu ambacho Serikali inaamua.

Kama ni kweli Mheshimiwa Rais Samia alilisema hili neno la 'Kelele' kama alivyonukuliwa popote pale alipo ajue kuwa binafsi 'amenikera' japo huenda Watanzania wengi wakawa 'wameridhika' nalo.

Watu wa Mkoa wa Mara (Musoma) ambao ndiyo 'Mashujaa' wa nchi hii ya Tanzania kuambiwa tuna 'Kelele' ni Kosa Kubwa mno na Dharau japo kwa Watu Washamba wao neno hili huenda wakalifurahia zaidi.


Nchi yenye mtindio wa ubongo..Mzee Kenyata kauli yake ilikua na maana ,kwamba muhasisi anaongoza maiti
 
Hapo ndipo nilipochoka. Yaani wananchi kupinga unyonyaji yeye anaita kelele!!?
Kuna msemo wa wahenga unasema masikini akipata,mat..o hulia mbwata.
 
Yaani Mwanamke kabisa anatuambia Wanamume wa Kikurya, Kizanaki,Kijita na Kijaluo kutoka Mkoani Mara kuwa tuna 'Kelele' Kwake? Hivi Bi Mkubwa hapa alipitiwa tu au alidhamiria?
Tata mraaah sijui anawachukuliaje?

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Nimeandika tu hivyo Mkoa wa Mara ( Musoma ) na Kuwatania hao Watani zangu Wapendwa ( Wajomba na Mashangazi ) kama sehemu tu ya 'Kuunogesha' Uzi ili hata kama tunalijadili hili la Kuambiwa ni Wapiga 'Kelele' lakini pia 'tunapoozana' kwa Kutaniana na Kuchangamshana hapa na pale.
Nakufahamu kwa muda mrefu humu jukwaani, najua aina yako ya uandishi, imekaa kimasihara sihara but unafikisha UJUMBE, twende mbele na diskasheni kaka
 
Hili ndio neno. Na huo ndio uanaume. Kama wewe ni wa mara bila kuingia barabarani. Humu unapiga kelele tu. Mwisho ataambiwa hamia burundi kwa kelele zako
Au ataambiwa na yeye aende kitunda akauuze mayai kwenye Baiskeli Kama wa Wakulya wenzie huko kitunda!!
 
Back
Top Bottom