Asante
nundu-, kwa andiko zuri lenye kufikirisha.
Maisha yanatawaliwa na
Uwepo.
Bila Uwepo hakuna maisha, ndio maana huyu Mungu wa Ibrahim Issaka na Yakobo ailiyeumba Uwepo yeye ndiye asili ya Uwepo.
Musa alipomwuliza
" Wewe unayejiita Mungu Jina lako unaitwa Nani kwa Jina ? "
Akajibu Mimi naitwa
NIKO AMBAYO NIKO.
Sehemu nyingine anajitambulisha Kama
MIMI NDIYE,
KABLA YA IBRAHIMU MIMI NIKO,
ALFA NA OMEGA yaani mwanzo na Mwisho.
BWANA WA MILELE
NK.
Nirudi kwa sisi Binadamu,
Binadamu pia wamerithishwa tabia ya ya UWEPO na Mungu.
Ila wao sio Alfa kwakuwa Wana mwanzo pale walipoumbwa.
Nikianza na kimwili hasa kwa sisi Waafrika, toka Adamu wetu azaliwe pale na kuishia pale Oduvai Gorge, ameendelaea kuishia hadi leo kwani bado damu yake unaishi hadi sasa ambayo ndio sisi.
Ni kosa Mwanadamu kujibu SIPO, au HATUPO.
Mtu anakuuliza kwenye simu uko wapi unajibu SIPO, hili nikosa.
Ukiulizwa uko wapi jibu
Niko Mjini au Kazini au Shambani au Nyumbani au sema ukweli nipo Guest House. NK.
Nirudi Kiroho, tunasoma Mungu alipomwumba Mwanadamu akampukizia Pumzi ya Uhai.
Hii Pumzi ya Mungu ya Uhai ni kitu cha thamani Sana sana kuliko MWILI. Hii ndiyo inayoitwa Roho inayojitambulisha Kama Nafsi.
Ukisikia watu wanasafiri kwa kumeditate ndiyo wanaitumia hii Pumzi ambayo ndo Uhai wenyewe kimwili wanauacha kitandani.
Yesu Kristo alipata kuwaambia wafuasi wake
"Msiwaogope wanawaua mwili bali mwogopeni mwenye uwezo wa kuiua Roho.
Na anasema pia
" Mtu aniaminiye Mimi hata akifa ataishi "
"Asiyeniamini hakika atakufa"
yaani Roho yake itauwawa na aliyeitengeneza.
Hapa analenga maisha ya umilele ya Kiroho.
Sehemu nyingine Yesu anasema,
"Waacheni Wafu wakawazike Wafu wao"
Kwani hao maisha yao yanakikomo pale wanapozikwa na kufa Kiroho.
Na akajitapa mahali kwa kusema,
Mimi NDIYE,
NJIA, KWELI NA UZIMA.
Hili pia ni Jina la Mungu.
Na hakuna kiumbe kilichokanusha hii sifa aliyojitapa Yesu Kristo, wala kuiga kujiita hivyo hadi hii leo.
ASANTE SANA.
Hivyo mleta
nundu, mada hongera Sana kwa kuleta mada very Philosophic and Real.