Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,380
- 6,142
Ukivuliwa tabaka zote za kumbukumbu ulizozikusanya kwa miaka mingi, ni kitu gani hasa kitabaki kukufanya uwe wewe?
Embu tafakari kwa kina hapa…
Huenda unachokiita akili si chochote zaidi ya maktaba ya mabaki ya jana iliyojificha ndani ya ubongo wako.
Maana mwanadamu haishi kwa kile anachokijua sasa, bali kwa kivuli cha yale yaliyokwisha pita.
Angalia, elimu yako ni marejeo ya kale,
Lugha yako ni mwangwi wa sauti zilizotamkwa kabla yako, Mwendo wako, maamuzi yako, hofu zako, imani zako na hata namna unavyoitazama dunia, vyote vimefungwa kwenye masanduku ya historia yaliyohifadhiwa kichwani mwako.
Ndiyo maana jamii humuita mtu huyu mwenye akili na mwingine asiye na akili kwa kupima ukubwa wa hazina ya marejeo aliyobeba.
Angalia hapa…
Daktari huitwa bingwa kwa sababu amehifadhi simulizi za magonjwa yaliyopita.
Mwanasheria hushinda kesi kwa sababu ameweza kuvuta kivuli cha hukumu za jana na kuzileta leo.
Na ushahidi wenyewe ni nini kama si mabaki ya jambo lililokwisha kufanyika muda uliopita?
Kwa kifupi ni kwamba hakuna hoja inayokubalika bila kupewa kaburi la zamani ili iweze kulalia.
Ndio maana ukisema jambo ambalo halijawahi kutokea, dunia hukutazama kama mwendawazimu. Lakini ukisema jambo ambalo lilishawahi kutokea, hata kama ni la kipuuzi, watu hulipa heshima fulani kwa sababu lina historia.
Ndiyo maana dunia yote inaonekana kana kwamba haiishi kuanzia sasa kwenda mbele, bali inaishi ndani ya makumbusho ya mambo yaliyopita na sasa. Kwasababu kila mfumo umejengwa juu ya ibada ya jana.
Leo hii mtu akikwambia ametoka sehemu unayoifahamu, hutaki kumuamini mpaka akupe alama za kale unazozijua zipo kwenye eneo hilo, akizitoa kwa namna sahihi, unaamini vinginevyo huwezi muamini.
Na hapo ndipo siri kubwa ilipojificha, ya kwamba binadamu haamini ukweli hadi uwe ule unaofanana na kumbukumbu zake au zozote zile za kale.
Na kwa sababu hiyo, sayansi nayo si kitu kingine isipokuwa historia iliyokataa kufa.
Historia ya kawaida huzikwa kwenye jana.
Lakini sayansi ni historia inayojirudia kwa nidhamu maalum hadi watu waiite sheria.
Mfano, mvua ilinyesha jana, ikarudia leo, ikitarajiwa kesho ndio tunasema kuna mfumo wa kisayansi unaoweza kuelezea mvua, kutokana na kujirudia rudia kwa tabia zile zile Kila mvua inapotaka kunyesha, lakini msingi wake bado ni ule ule, kumbukumbu ya yaliyopita.
Ila dunia ikikutana na jambo lisilo na mizizi kwenye jana. Kwa mfano, ugonjwa ambao hauna mfano wowote uliowahi kuwepo, usio na pattern, usiorudia tabia, usiokubali kuhifadhiwa kwenye rekodi.
Ndipo utaona namna akili zote zitakavyosimama pasinakujua wapi waanzie na wapi wamalizie.
Kwa sababu uwezo wa mwanadamu haujazoea kuumba kutoka mwanzo, ila umezoea kurejea kutoka kwenye kile ambacho tayari kilishakuwepo.
Hata AI mnayoihofia leo, haifanyi kazi kwa kuona kesho bali inavuta vipande vya jana na kuvipanga upya ila yenyewe hufanya kwa kasi kubwa kuliko mwanadamu.
Kwahiyo, future ndiyo eneo pekee ambalo akili hushindwa kutawala, ndiyo maana kesho hubaki kuwa fumbo na jana hubaki kuwa mwalimu na kipimo cha werevu.
Ukifaulu mtihani kwa A zote, huenda hukua na akili kuliko wengine bali huenda ulikuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kubeba mizoga ya taarifa za zamani kichwani mwako na hii ikafanya ukaitwa genius kwa sababu uliweza kukariri historia kwa usahihi mkubwa kuliko waliokaa pembeni yako.
Na hapa ndipo dunia ilipojenga mfumo wake wa ulinzi.
Kwamba, ukileta hoja isiyo na kumbukumbu ya zamani, wenye dini watakuambia unakufuru ikiwa imelenga upande huo na ukileta mbele ya wasomi, watakuambia thibitisha.
Na kuthibitisha huko maana yake ni nini?
Wanataka urudi jana ukatafute ushahidi.
Ukishindwa kufanya hivyo, hoja yako hufa kabla hata haijasikilizwa.
Ndiyo maana watu wengi hurudi kwa hiari ndani ya gereza la kawaida la fikra, gereza la historia. Kwa sababu huko hakuna pingamizi na ni sehemu salama ya akili zinazohitaji kivuli cha jana ili ziweze kupumua.
Lakini swali ambalo wengi hawathubutu kujiuliza ni hili…
Je, ni nani aliyeufuma mfumo huu wa kuabudu yaliyopita?
Kwa nini dunia inaonekana kana kwamba inaruhusu kujua kile kilichokwisha kuwepo pekee, na inazuia kufikiri kuhusu kile ambacho hakijawahi kuwepo?
Kana kwamba kuna ukuta usioonekana unaozuia akili kuvuka mipaka ya historia, na dunia pamoja na mifumo yake yote hufanya juu chini kuulinda ukuta huo usionekane.
Na huenda ndio maana hakuna jipya chini ya jua, na si kwa sababu mambo mapya hayawezi kutokea, hapana, bali kwa sababu akili nyingi zimefungwa ndani ya maktaba ya jana kiasi kwamba haziwezi kutambua kile ambacho hakina kumbukumbu.
Imani yangu inaniambia sisi ni bora ya zaidi ya hivi tulivyo, ila ni vile tumefungwa kwenye eneo ambalo halitupi mwanya wa kuona zaidi ya vile ambavyo tunalazimishwa tuvione.
Ndio maana nasema, ukifutiwa kila ulilowahi kujifunza, kila uso uliowahi kuuona, kila neno ulilowahi kusikia… usingebaki na akili bali ungebaki na utupu unaohitaji kufundishwa historia upya ili uweze kuruhusiwa kuishi tena ndani ya mfumo wa dunia kwasababu akili unayohisi uko nayo huna bali imetengenezwa na kuwa shaped kinamna ile dunia inataka iwe.