Kuwepo au Kutokuwepo; wote wapo

N

Nundu_Tanzania

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
23
Points
45
N

Nundu_Tanzania

Member
Joined Apr 19, 2019
23 45
Huyu aliyepo hii leo ndiye asiye kuwepo badae na asiye kuwepo ndiye aliyepo. Hiki unachokiona leo siyo hicho walichokiona waliokuwepo, lakini ndiyo hicho kilichopo, ambacho kila aliyekuwepo, anayekuwepo na atakaye kuwepo anacho.

Wewe upo kwasababu wao walikuwepo na kwasababu walikuwepo na wewe upo na hivyo wote mpo.

Ukisema kwa sababu walikuwepo hivyo hawapo sasa maana yake na wewe haukuwepo na haupo sasa. Kama unasema walikuwepo, lakini sasa hawapo maana yake wewe pia hukuwepo ndiyo sababu unaona hawapo.

Ukiwa mwanadamu tayari umekuwepo na hivyo haiwezekani kwamba hautakuwepo.

Mtu aliyepo anawezaje kusema hayupo angali yupo? Vivyohivyo kwa aliyekuwepo atawezaje kutokuwepo? Aliyekuwepo ndiye aliyepo nae atakuwepo. Vivyohivyo kwa aliyepo ndiye yupo na atakuwepo.

Kama huyo hayupo maana yake na wewe haupo, lakini kama wewe upo na yeye yupo. Unawezaje kusema, yeye hayupo, lakini wewe upo?

Kama mtu huzaliwa na aliye kuwepo na yeye huyo anaezaliwa huwapo nae akisha kuwapo huzaa atakae kuwepo. Sasa ni nani kati hawa anaeweza kudai huyu hayupo?

Hivyo hakuna awezae kuwepo kama aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuwepo hajaweza kuwepo na hivyo aliyekuwepo yupo, atakuwepo na kwasababu yupo nasi tupo.
 
Use brain Heriel

Use brain Heriel

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2017
Messages
1,728
Points
2,000
Use brain Heriel

Use brain Heriel

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2017
1,728 2,000
nimesoma 6 times sijaelewa mtoa mada embu toa hint ya hii puzzle.

La sivyo saa nne kamili nachoma jani nameditate nakuja na lugha nyepesi ya fumbo lako.
 
E=mcsquared

E=mcsquared

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2009
Messages
224
Points
195
E=mcsquared

E=mcsquared

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2009
224 195
Kawaida, watu hawawezi kusema kuwa haupo wakati hukuwahi kuwepo! Maana yake ni kwamba ili uwe haupo, lazima uwe uliwahi kuwepo. Kwa hiyo huwezi kuwa haupo bila kuwa uliwahi kuwepo, au huwezi kutokuwepo bila kuwepo!
 
N

Nundu_Tanzania

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
23
Points
45
N

Nundu_Tanzania

Member
Joined Apr 19, 2019
23 45
Mkorea, hapo ulipo sasa, huyo ambae alikuwepo nae alipata kuwapo hapo. Kwasababu yeye aliyekuwepo alikuwepo hapo ulipo ndiyo maana na wewe upo hapo. Kumbe basi, aliyekuwepo kabla yako haiwezekani asiwepo wakati wako. Hii ni kwa sababu bila ya uwepo wake kwanza hakuna uwepo wako baadae.
 
N

Nundu_Tanzania

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
23
Points
45
N

Nundu_Tanzania

Member
Joined Apr 19, 2019
23 45
Jambo likiwa kawaida ndivyo lilivyo. Hivyo kama lilivyo kawaida ndiyo hivyohivyo nasi tupo.
Yaani hivi: huyo aliyekuwepo kwanza na kwa yeye huyo wewe ukawa badae, ndani yake ndiye yeye huyohuyo, ambae kwake wewe uliyepo wakati wako, umepata kuwepo. Na kwa ajili hiyo, kwa sababu yeye alikuwepo kwanza kabla yako na kwake yeye wewe ndiyo ukawepo, inawezekanaje kudai kwamba, huyo ambae wewe kwake ndiyo umetoka na kisha ukawepo asiwepo?
 
BabaMorgan

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Messages
471
Points
1,000
BabaMorgan

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2017
471 1,000
Jambo likiwa kawaida ndivyo lilivyo. Hivyo kama lilivyo kawaida ndiyo hivyohivyo nasi tupo.
Yaani hivi: huyo aliyekuwepo kwanza na kwa yeye huyo wewe ukawa badae, ndani yake ndiye yeye huyohuyo, ambae kwake wewe uliyepo wakati wako, umepata kuwepo. Na kwa ajili hiyo, kwa sababu yeye alikuwepo kwanza kabla yako na kwake yeye wewe ndiyo ukawepo, inawezekanaje kudai kwamba, huyo ambae wewe kwake ndiyo umetoka na kisha ukawepo asiwepo?
Ulipo nipo na kwa sababu nipo ulipo inamaanisha kuwa wote tupo tunapokuwa tupo wote uwepo unakuwa unatokea kwa wote tuliopo ndo maana hadi vivuli vinakuwepo maana vinathibitisha uwepo wetu na hii haitokei kwetu tu Bali kwa wale wote ambao wapo duniani.
 
joanah

joanah

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
9,285
Points
2,000
joanah

joanah

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
9,285 2,000
Naona nyota nyota mpaka muda huu

Ngoja nirudie. Au sio kila kitu lazima tuelewe
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Kwa mazingira niliyopo hapa huu uzi ni wa kusoma kesho labda ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Sihitaji mambo magumu hivi

Jaribu kusoma tena labda unaweza kupata kitu...tunashindwaje wote aseee ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 

Forum statistics

Threads 1,304,164
Members 501,290
Posts 31,505,016
Top