The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 8,551
- 20,346
Kisa cha kweli Mwajili Tapel kuweni Makini sana.
Katika Ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa adimu kuna matapeli wengi wanaoliza watu tuwe makini, Hiki ni Kisa cha kweli kabisa kanisimulia rafiki yangu kiilimpata last week.
Iko hivi huyu jamaa alipigiwa simu na baba yake mdogo Kwamba kuna mtu kampigia simu aliwahi kumsaidia kimasomo alikuwa yatima sasa kashapata kazi ya HR mahali na ananafasi ya kazi hivyo angependa ampatie mtu awe ni mwanafamalia kama kurudisha fadhila.
Huyu baba mtu ni mtu wa kanisa hivyo alitumia baadhi ya michango ya waumini kumsomesha huyu bwana HR maana alikuwa yatima na aliletwa kwake na waumini kwa hiyo uaminifu ulikuwa ni mkubwa hata baada ya kuombwa alipwe fadhila.
Sasa huyu ndugu aliyetapeliwa hakuwa na wasiwasi kwa sababu kaambiwa na ndugu yake tena baba mdogo mtumishi wa kanisa. Basi huyu ndugu alipewa namba na baba yake ili amtafute huyo HR Yatima mrudisha fadhila.
Waliweza kuongea na huyu HR wakatambulishana kwenye simu. HR akiwa anaongea kwa sauti ya upole na yenye huruma alikiri kusaidiwa kweli kimasomo na baba mtu maana yeye hakuwa na chochote ila sasa maisha yamemnyokea anamliki gari nzuri, nyumba, mshahara mnono pamoja na nafasi kubwa ya HR katika Kampuni (X) kubwa hapa Tanzania.
Basi huyu ndugu hakuwa na wasiwasi tofauti na kufurahi kupatiwa hilo dili lenye mshahara mnono bila kikwazo maana alitajiwa mshahara mnono sana na huyu HR kama fadhila kwa familia baada ya kusaidiwa kimasomo na baba mtu.
Picha linaanza majira ya saa sita mchana HR anasema sasa tuna kikao leo saa kumi kamili jioni kwa ajili ya kupitia jina lako ambayo ni nafasi niliyoomba mimi binafsi kama HR kwa hiyo lazima upate, ila sasa inahitajika barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa, kama una jamaa yako yupo karibu hapa mpe details zako alafu atanipatia niwasilishe kwa wakubwa waidhinishe jina lako .
Option ya pili akamwambia kama huna jamaa hapa mkoani wenye viti wa serikali za mtaa huwa wanatoa hizo barua kwa gaharama ya 50K tu maana hii ni kampuni kubwa sana Kwa sababu ya uharaka jamaa hakuona tabu kutoa 50k akiwa na imani kabisa na mtu aliyeunganishwa na baba yake mdogo tena mtumishi wa kanisa.
Basi aliahadiwa jioni mida ya saa moja atapigiwa simu kwa maelezo zaidi baada ya kujadili jina lake na wakubwa wenzake kweli saa moja inafika simu inaita na maelezo yakawa hivi kwa sauti ya upole kabisa.
" Tumepitia jina lako mambo yameenda vizuri tu na jina lako limepitishwa sasa kinachofuta ni kusaini mkataba tu. Utachagua Mwenyewe uje usainie huku au tukutumie kwa njia ya email, Tahadhari ukija huku utafanyiwa interview upya kitu ambacho mimi sitaki maana ni issue ya kifamilia. Interview inaweza kuwa mgumu na msaada wangu huenda usifaanye kazi kwa sababu 95% wanaofanyiwa interview hapa hufail"
"Lakini nikikutumia mkataba kwa email itakuwa vizuri ila itabidi tuwapoze kidogo hawa jamaa wa mikataba ili wafanye haraka, nimeomba umepewa mkataba wa miaka mitatu Mshahara utaanzia 3.5M na utapanda hadi 5M kutegemeana na juhudi zako Mwenyewe"
Uoga wa interview ulamfanya huyu jamaa akubali tu atumiwe mkataba na akapewa maelekezo atoe hela kidogo 150K ili watu wanaohusika na mikataba wapozwe hata kama hiyo 150k ingepungua basi huyo HR angeongezea maana ni issue ya kifamilia zaidi.
Sasa huyu bwana hicho ndicho kilichomshitua na kuamua kumrudia tena baba yake mdogo kumuuliza kulikoni mbona tena huyu HR Mrudidha fadhila anaomba hela ili kufanikisha baadhi ya mambo.?
Alimtajia ile 50K ya serikali za mitaa na hii 150K kwa ajili ya kutumiwa mkataba. Baba yake alishituka sana na kumwambia hata ile 50K usingemtumia ungeniambia kwanza ili tupate uhakika.
Mzee alikiri kumsaidia kimasomo mtu huyo, lakini alishindwa kuelewa ni nini kilimpata hadi kuwa tapeli au pengine. Simu yake illibiwa na kuanza kufanyiwa utapeli
Kwa hiyo ndugu zangu tuwe makini sana katika utafutaji.