Kuwa wapenzi wa muda mrefu na hadi kufunga ndoa ni kitu kinavutia sana

Iam Lupa

Member
Sep 22, 2023
37
75
Nakumbuka mwaka jana nilihudhuria harusi ya rafiki wangu (wa kike),asee was very impressed kwa kweli. Si unajua pale tena harusi za siku hizi wale maharusi wanachukua time ya kuelezea familia zao na kujuana ndugu wa pande zote.

Basi kwenye maelezo yule jamaa akasema alikutana na huyu manzi miaka 9 nyuma,na tokea hapo wakawa wapenzi na hadi inafika time wanafunga ndoa. Inapendeza sana

Katika hili nikaja kugundua mambo matatu, kuwa ili upate kuwa pamoja na mwenzi wako kwa kipindi kirefu basi lazima yafanyike haya.

1.Lazima mmoja awe mjinga kwa mwenzie - kusikilizana sawa ila kuna baadhi ya mambo ya mambo unayaona ila unajifanya hauyaoni (special kwa mwanaume)hawa ladies wana mambo mengi sana ya kukera na ukichukulia serious kwa kila kitu basi mapema tu munamwagana.

2.Upendo - lazima kuwe na true love hata ya upande mmoja (special kwa mwanamke)kama mamaa amekuelewa atleast 95% basi gentle upo kwenye njia nzuri ya kuwa na mahusiano ya muda mrefu.

3.Kujali - kila mmoja we tayari kujali haja na shida za mwenzie(kama nyege unachukulia kitu simpo kwa mwenzako io safari yenu haina umbali) na hata kwenye misaada ya kifedha na mawazo pia ni muhimu kuzingatia.

Mwisho: zingatieni afya zenu
 
Hakuna kitu bora katika maisha kama kumpata wa kuendana nae, na ukimpata kila kitu kinakaa ktk nafasi yake.
Huo upendo, kujali vyote vinakuja bila kutumia nguvu.

Mimi nitaendelea kumshukuru Mungu, nimeyaona na kuyaishi mapenzi ya kweli kwa neema zake.
 
Ngoja niendelee kumvumilia huyu wangu japo tumetoka mbali toka yupo form 3 mimi nipo form 5 mbaka nimemaliza chuo yeye now yupo second year siku zilizopita tulikuwa tunaongelea swala la ndoa japo nilitaka akimaliza tu nimuoe ila ameniomba sana mbaka leo anazidi kuniomba et aingie kwanza masters akimaliza ndo tuonae nikamkatalia nikamwambia kwani kuna ubaya gani ukisoma huku nimke wa mtu akalia sana kuwa nisifanye hivyo now anasema bas aingie masters mwaka wa kwanza ukiisha tu tunaoana huku anaendelea kusoma kiukweli mbaka leo sijajua ni nini anakitengeneza au ni nini anakitafuta japo ndio najua kuwa ni ndoto zake na siwez kumzuia kusoma ila ngoja tuone itakuaje mungu ndo anajua
 
Na wa kwangu nimeanza ukaribu nae nikiwa form five yeye yuko form three ila tumeanza mahusiano akiwa Diploma 2. Sasa anaingia Degree.
 
Ngoja niendelee kumvumilia huyu wangu japo tumetoka mbali toka yupo form 3 mimi nipo form 5 mbaka nimemaliza chuo yeye now yupo second year siku zilizopita tulikuwa tunaongelea swala la ndoa japo nilitaka akimaliza tu nimuoe ila ameniomba sana mbaka leo anazidi kuniomba et aingie kwanza masters akimaliza ndo tuonae nikamkatalia nikamwambia kwani kuna ubaya gani ukisoma huku nimke wa mtu akalia sana kuwa nisifanye hivyo now anasema bas aingie masters mwaka wa kwanza ukiisha tu tunaoana huku anaendelea kusoma kiukweli mbaka leo sijajua ni nini anakitengeneza au ni nini anakitafuta japo ndio najua kuwa ni ndoto zake na siwez kumzuia kusoma ila ngoja tuone itakuaje mungu ndo anajua
Kwani 'mbaka' sasa hivi umeshahitimu au ulidisco?
 
Nili date na mwanamke miaka saba mpaka tukafanana ,tulipewa majina kwamba sisi ni mapacha ila nilicho ambulia ni kadi yake ya send off pamoja na fedheha kibao,

Mimi kama mwanaume nilisononeka sana ila hakuna jinsi nimejifunza sana mwanamke siyo kiumbe kizuri ni hatari mno na hupaswi kumuweka akilini.

Mlio weza kudate muda mrefu na mkaoana na kuolewa nendeni mkatoe sadaka ya shukrani sawa sawa na imani zenu.
 
Raha ya JF ni pale una miaka 25 ya ndoa halafu unakuja kugundua kumbe kwenye ile mada fulani ya ndoa yule jamaa aliyekuwa anakuambia hujui lolote kuhusu ndoa bora ukae kimya uache wenye ndoa wakufundishe huu ndo mwaka wake wa pili kwenye ndoa na hana mtoto bado.
 
Nili date na mwanamke miaka saba mpaka tukafanana ,tulipewa majina kwamba sisi ni mapacha ila nilicho ambulia ni kadi yake ya send off pamoja na fedheha kibao,

Mimi kama mwanaume nilisononeka sana ila hakuna jinsi nimejifunza sana mwanamke siyo kiumbe kizuri ni hatari mno na hupaswi kumuweka akilini.

Mlio weza kudate muda mrefu na mkaoana na kuolewa nendeni mkatoe sadaka ya shukrani sawa sawa na imani zenu.
Niliambulia kuambiwa nashukru kwa muda wote tuliokaa pamoja. Naomba usihangaike kunitafuta endelea na maisha yako. ! Nilimjibu H' Mbona hunashukrani.

Niliumia sana kwa sababu hakuna sababu aliyoitoa ya kuachana. Miezi 3 baadaye kaolewa. 😀

Kweli tunaowapenda ndiyo hao waletao maumivu.
Wanawake tuwape heshima yao😀
 
Ngoja niendelee kumvumilia huyu wangu japo tumetoka mbali toka yupo form 3 mimi nipo form 5 mbaka nimemaliza chuo yeye now yupo second year siku zilizopita tulikuwa tunaongelea swala la ndoa japo nilitaka akimaliza tu nimuoe ila ameniomba sana mbaka leo anazidi kuniomba et aingie kwanza masters akimaliza ndo tuonae nikamkatalia nikamwambia kwani kuna ubaya gani ukisoma huku nimke wa mtu akalia sana kuwa nisifanye hivyo now anasema bas aingie masters mwaka wa kwanza ukiisha tu tunaoana huku anaendelea kusoma kiukweli mbaka leo sijajua ni nini anakitengeneza au ni nini anakitafuta japo ndio najua kuwa ni ndoto zake na siwez kumzuia kusoma ila ngoja tuone itakuaje mungu ndo anajua
Bro jichunguzee sanaa.... Wanawake wanamambo ya chinichini Sana uenda hawaka mkweli ila jichunguzee wewe una kipato kinatosha au umesimama tayari uenda yeye anakupa mda ili aone mwelekea wako ili awe na uhakikaa na uenda mpaka Sasa Hana uhakikaa na wewe ila angekua na uhakikaa bro mademu ndio wanang'ang'ania ndoa ila wako inaonekana Hana uhakikaa
 
Back
Top Bottom