Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Jamani ni kweli kupeana ujuzi wa kuwa wajasiliamali. Kwa kifupi nianze hivi.
tunapo taka kufanya jambo haijarishi lina faida ndogo au kubwa lazima kwanza tuishirikishe mioyo yetu. Waweza pewa detail za kutosha jinsi ya kuanza mradi wa kuku na faida ikawa kubwa kwa kusoma makaratasi au makara mbalimbali. Hivyo unavyo soma au unavyo ambiwa sivyo ilivyo kwako au itakavyo kuwa kwako. Wewe itakuwa tofauti. Na kama hujawahi kufuga hata kuku mmoja ukamtunza usilaumu hayo makaratasi au maneno. Wanao paswa kutumia hayo makaratasi ni waliothubutu kwa kiasi fulani na sasa wanapanda nngazi. Si kwa wewe unaye fikiri iwe hivyo.
aksanteni nitarudi kwa somo dogo.
 
ufugaji wa kuku hasa kienyeji.kiuhalisia haikupi faida haraka,chukulia kama unahifadh fedha yako baada ya muda utapata faida.AU ni kama umenunua hisa,baada ya muda fulan utapata mgao. Kuku faida yake ni baada ya miezi 5 - 6, hapo ndo unaeza ona matunda ya kile ulichopanda kwa miez 6. Nadhan ndio katika ufugaj invist ya mda mfupi.
 
Wakuu fursa kama hizi inahitaji kujiongeza kidogo,hapo unapotafutia ridhiki tafuta wenzako mmoja au wawili mtafute kiwanja kikubwa kidogo nje ya mji mchangishane kisha mkinunue mgawane.

Let's say kipo sehemu kina miguu 50×50 kinauzwa mill5 na wewe hunayo hiyo pesa yote,mkiwa wawili mkakinunua mkagawana pasu utaweza kutekeleza azma yako.

Muhimu we jichangishe tu na uzima uwepo.
Mkuu miguu 50×50 ni sawa na mita ngapi kwa ngapi?
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
nadhani anachofanya kuwawekea mayai 15 and probly watatotoa 14hadi 12 inategemea hali ya hewa mm nimefanya na naendelea kufanya huwa wanatoto hadi 14 ,then unawaacha na mama zao kwa wiki 3 watarudia tena kutaga baada ya wiki moja then siku 21 ya kutaatamia
 
Inawezekana, ila ndio gharama. Mfano una matetea 10 yakitaga kwa pamoja Na kuku wa kienyeji anataga mayai 15-20 maana yake unaokota mayai 150 -200 na mayai yanayofaa kutotoleshwa hayatakiwi kuvuka siku 12. Hivyo Siku 12 Za kwanza Mara mayai 10 kila siku ni mayai 120 unapeleka kwa mtotoleshaji Mwenye incubator. Usipomuatamisha kuku ndani ya wiki mbili mpaka tatu anaanza tena kutaga. Hivyo katika miezi mitatu unaweza kufikisha vifaranga 300.
msada zaidi hapa,umesema mayai ya kwenda kutotolesha yasikae zaidi ya siku 12?
 
hatukatai kwamba kuna chalenges kwa kila mwanadamu afanyalo, my point is - anza business with low expectation. mtu akisoma bandiko hapo juu hakawii kukimbia benki kukopa pesa illi awahi kupata nyingi zaidi.

Ufugaji wa kuku umeaza kitambo sana miaka ya 60's - fanya upelelezi ni matajiri wangapi wamepitia ufugaji huu wa kuku?
mkuu usisahahu kuwa kila zama na kitabu chake.
 
Mkuu ukifuga kisayansi hiyo hesabu itafika. Tatizo lako wewe unafuga kwa mazoea.
Ha ha ha...
Hivi nani alitunga hii hadithi aiseeh?
Kwanza, Kuku wa kienyeji huwa hawatagi kwa pamoja, na hawatagi mfululizo... Ukianza na Kuku 11 na ukienda vizuri inaweza fikisha Kuku 100 ndani ya mwaka mmoja ukijitahidi na uwe na Bahati kweli kweli...
Utajiri sio kama kucheza draft kwamba unaweka hapa na kupata pale...
Naongea kama mfugaji mzoefu na mbobevu, hii hesabu ya mada hii field HAIWEZEKANI
 
Back
Top Bottom