Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, May 21, 2018.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
  [​IMG]
  LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

  Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
  Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

  Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

  Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
  Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

  Mchanganuo Wa 69500 ni:-
  Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

  Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
  Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
  layer's consetraite

  Kilo 25 kifuko. = 21500.

  Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

  Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

  Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
  Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
  Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

  TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
  Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

  Jogoo 1 = 20000
  Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
  Itakuwa imebaki shs. 60500

  -Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

  Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
  Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

  Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

  Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

  Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
   
 2. APEFACE

  APEFACE JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2018
  Joined: Oct 1, 2016
  Messages: 2,200
  Likes Received: 2,170
  Trophy Points: 280
  Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
   
 3. Norshad

  Norshad JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2018
  Joined: Jun 3, 2013
  Messages: 3,114
  Likes Received: 5,541
  Trophy Points: 280
  nyumba za kupanga mtihani kweli kweli, shamba kuku ni elfu 6 tu
   
 4. Sir_Mimi

  Sir_Mimi JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2018
  Joined: Jun 21, 2013
  Messages: 3,907
  Likes Received: 4,660
  Trophy Points: 280
  Wakuu fursa kama hizi inahitaji kujiongeza kidogo,hapo unapotafutia ridhiki tafuta wenzako mmoja au wawili mtafute kiwanja kikubwa kidogo nje ya mji mchangishane kisha mkinunue mgawane.

  Let's say kipo sehemu kina miguu 50×50 kinauzwa mill5 na wewe hunayo hiyo pesa yote,mkiwa wawili mkakinunua mkagawana pasu utaweza kutekeleza azma yako.

  Muhimu we jichangishe tu na uzima uwepo.
   
 5. Karne

  Karne JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2018
  Joined: Jun 13, 2016
  Messages: 1,768
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Hii michanganua kwa kuisoma hivi tu inaonekana ni simple ila ukienda field sasa.
   
 6. Tajiri Kichwa

  Tajiri Kichwa JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2018
  Joined: Apr 2, 2017
  Messages: 1,024
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Vipi huyo jogoo mmoja... ikatokea hapandi mtungi si bajeti inaharibika maana hakutakuwa na watoto wa kuku wapya
   
 7. 13 mega pixel

  13 mega pixel JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2018
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 4,291
  Likes Received: 4,040
  Trophy Points: 280
  Safi mkuu, kwangu nina banda nilijenga vyumba viwili vikibwa tuu, sikumalizia nitalimalizia kisha nijaribu kufanya hivi
   
 8. k

  kyata JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2018
  Joined: Jun 20, 2015
  Messages: 372
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Hii Mie naifanyia kazi kuanzia wk hii, Naomba kuelekezwa sehemu y'a kupata Mbegu nzuri y'a kuku. Maana banda ninalo tayari. Mungu ibariki hili wazo n'a mleta wazo pia.
   
 9. mjr95

  mjr95 JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2018
  Joined: Oct 10, 2016
  Messages: 5,325
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Hapa ndio watu hufikia tunaanguka katika mambo mengi. Badala ya kufanya jambo kwa moyo mmoja eti unajaribu. Ufanye kwa kupenda kabisa sio eti nitajaribu.
   
 10. n

  ngonyango JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2018
  Joined: Aug 7, 2017
  Messages: 470
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  yaani kusoma maelezo kama haya utaona ni kazi rahisi kweli lakini duh ingiza timu uone kimbembe chake...
   
 11. peterchoka

  peterchoka JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2018
  Joined: Oct 12, 2014
  Messages: 6,880
  Likes Received: 6,238
  Trophy Points: 280
  Ukishafanya hayo, umemaliza kazi yako imebaki ya Mungu tu
   
 12. m

  miki123 Member

  #12
  May 22, 2018
  Joined: Apr 27, 2018
  Messages: 60
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Uzuri mada imekopiwa toka mtandaoni na sijui uzoefu wa mtoa na huko mada alikoitoa kwenye ufugaji wa kuku, inahitaji ujipange kuanzia ufugaji wenyewe + magonjwa ya kuku na baada ya hapo ulishafikiria kuhusu soko la kuku na changamoto zake? yote yanawezekana ila si kwa kirahisi kihivyo.
   
 13. 13 mega pixel

  13 mega pixel JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2018
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 4,291
  Likes Received: 4,040
  Trophy Points: 280
  Mkuu nia ya kujenga ilikuwa kufuga kuku, lakini siyo kwa namna hii aliyosema mdau, hivyo nitajaribu kufanya namna yake
   
 14. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2018
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,293
  Likes Received: 8,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

  Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
   
 15. m

  mob JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2018
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,131
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  mkuu kuna uzi kama huu niliupitiaga nikakaa chini nikaufanyia kazi mkuu umelipa sana.Kuliko kujenga nyumba ambayo utapangisha watu chumba elfu 30-60 chumba kwa mwezi ni bora kufuga kuku mia kwenye hicho chumba nikiwa na maana kuwa ukiwa na ukuku mia una uhakika wa mayai 20 kila siku sasa yai moja la kienyeji ni 500 * 20= 10,000 so kwa mwezi una uhakika wa laki tatu ukitoa matunzo na usimamizi unabakiwa na 150,000( makadirio ya juu sana) sasa hapa hujapigiana kelele na mtu kachafua nyumba kabomoa mlango sijui umeme sijui kuvuta uchafu NK.Hii salio linatosha kabisa kwa familia ya kawaida kulipia bili ya umeme na maji kwa mwezi na kusukuma angalau kwa mboga kwa siku mbili tatu huku pia cku moja moja na wewe mfugaji kula mayai mara moja moja.

  Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds!
   
 16. Inna

  Inna JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2018
  Joined: Jan 13, 2017
  Messages: 6,438
  Likes Received: 14,770
  Trophy Points: 280
  ngoja nijaribuu..
   
 17. GoPPiii.

  GoPPiii. JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2018
  Joined: Oct 6, 2014
  Messages: 1,203
  Likes Received: 1,576
  Trophy Points: 280
  Shukrani kwa Bandiko nimepata kitu hapa...
   
 18. mjr95

  mjr95 JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2018
  Joined: Oct 10, 2016
  Messages: 5,325
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Jaribu na dingimtoto, mm nitafanya na mumu na si kujaribu kama ww.
   
 19. dingimtoto

  dingimtoto JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2018
  Joined: Jan 9, 2016
  Messages: 4,022
  Likes Received: 8,304
  Trophy Points: 280
  Asante comrade, huu Mchanganuo mzuri ngoja nitaufanyia kazi
   
 20. devor

  devor Senior Member

  #20
  May 23, 2018
  Joined: Oct 15, 2017
  Messages: 158
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hiv kuku wa kienyej unaweza uka wafuga kwa Ku wafungia ndan kama hawa kuku wa kizungu" maana Nina vyumba viwili dabo vipo tupu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...