Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Shukrani mleta mada, jamani hebu punguzeni upinzani, mleta mada katoa mwanga na Alama za mlango hivyo wewe unaweza kutafuta njia, si lazima ufuate hatua kama alivyo eleza lakini kupitia maelezo yake unaweza kufanya kitu.
 
Hii michanganuo kwa kuisoma hivi tu inaonekana ni simple ila ukienda field sasa.

Inafurahisha kuisoma na kuchangia tu lakini ukithubutu ukaingia kwenye utekelezaji utajutia..
 
Ufugaji wa online simple sana
tia chuma physical uone kama dunia ijakutenga

bora kuku wa kisasa bei ndogo na ata consuption yake kubwa hasa maeneo ya Dar es salaam

kuku wa kienyeji ni wazuri
lkn sokoni bei yake ni juu
kwaiyo walaji wapo lkn kwa namba sio kubwa sana kulinganisha na wa kisasa
 
Hivi wanaoandikaga hii michanganuo wanakuwa washawahi kufuga walau kwa mwaka mmoja au ndio wanaanza au pengine hawana hata kifaranga?

Sitaki kusema kufuga kuku au mnyama mwingine hakulipi lakini sio rahisi kama ambavyo watu huwasilishaga hizi mada humu.
 
Ni. Kweli mkuu jamaa ameshindwa kuchanganua labda kacopy sehem ukiwa na kuku 10 mitetea na jogoo 1 ukawalisha vizuri chakula chenye mchanganyiko wa
Mashudu
Damu
Chokaa
Mfupa
Pumba
Kwa muda wa week 2 wataanza kutaga lets say kila kuku akitamia mayai 100
Baada ya kutotoa week 1 baadae unawanyanganya vifaranga kwa mama zao. Hao vifaranga unawapa chakula cha vifaranga huwa kinauzwa maduka y vyakula kilo moja sh 1500 huku ukiwapatia joto kwa taa ya umeme au chemli!
Hao mitetea uliowanyanganya vifaranga wakila vizuri chakula chenye mchanganyiko maalum nilioelezea hapo juu ndani ya week 2-3 wataanza kutaga tena na kuatamia wakitotoa baada ya wee1 unawanyanganya Tena vifaranga!
Fanya hivyo kwa miez 6 utakua na kuku wenhi
Mkuu huoni kama unaingilia haki ya kikatiba ya wanyama kwa kumpora kuku uzao wake kila mara, ulaya unafungwa kwahio kesi!
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
Inawezekana, ila ndio gharama. Mfano una matetea 10 yakitaga kwa pamoja Na kuku wa kienyeji anataga mayai 15-20 maana yake unaokota mayai 150 -200 na mayai yanayofaa kutotoleshwa hayatakiwi kuvuka siku 12. Hivyo Siku 12 Za kwanza Mara mayai 10 kila siku ni mayai 120 unapeleka kwa mtotoleshaji Mwenye incubator. Usipomuatamisha kuku ndani ya wiki mbili mpaka tatu anaanza tena kutaga. Hivyo katika miezi mitatu unaweza kufikisha vifaranga 300.
 
Hiv kuku wa kienyej unaweza uka wafuga kwa Ku wafungia ndan kama hawa kuku wa kizungu" maana Nina vyumba viwili dabo vipo tupu
Inawezekana lakini ni vizuri zaidi wakapata kaeneo ka kukimbia Kimbia na kuoga mchanga. Unaweza kuzungushia nyavu kidogo
 
Kuku 11 (wa kienyeji)wazalishe kuku 300 in 3 months ni impossible labda uwe unafuga panya. Kifaranga kinachukuwa miezi 3 hadi miezi 6 kukuwa na kuanza kutaga mayai. Tuwe tunaandika vitu vya ukweli sio kudanganyana kama wanasiasa wa hiki chama wanavyofanya
Hapo ndipo mlipochanganyana hilo linawezekana kifaranga mpaka kianze kutaga ni miezi sita hivyo ni obviously hakumaanisha utakuwa na kuku Mwenye uwezo wa kutaga bali utakuwa na kuku (vifaranga) 300+
 
ukitaka faida katika ufugaji wa kuku wa kienyeji. Bas wafuge kienyeji.
Kumbuka wanauza madawa ni wafanyabiasha, na wanaouza chakula pia. Haya madawa ya kuku ndio chanzo kikubwa cha magonjwa kwa kuku, fanya nawe research, watenge kuku ambao utawapa aloevera na mwarobaini pekee, alaf wengne wape hayo madawa ya minyoo,antibiotic,chanjo nk. Alafu uone banda la kuku wasiopewa madawa hawatasumbuliwa na maradh pia utagaj wao unaongezeka. Lakin wale wa madawa kila muda utakumbana na magonjwa. Jiulize kuku wanaopatikana vijijini kabisa wanapewa dawa zipi.
 
Back
Top Bottom