Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Hesabu za kwenye makatasi ni rahisi mno, ukifanya practical si jambo jepesi kama unavyoandika hapo!! usidanganye watu wakaingia wakakuta mambo ni tofauti kabisa.
 
Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Kuku-kupatana.jpg

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
Utajiri huwa hautangazwi hadharani hivi..!
 
Unaendelea vizuri ila nilishauachia mtu mwingine - wife; mimi huwa napenda kutengeneza sehemu za kufundishia jamaa zangu. Kwa sasa nimeanza wa nguruwe .. naona hata soko la ndani halijitoshelezi.
Soko la nguruwe likoje mkuu, nataman nianze huu mradi mwezi wa 12,.
 
Hesabu za kwenye makatasi ni rahisi mno, ukifanya practical si jambo jepesi kama unavyoandika hapo!! usidanganye watu wakaingia wakakuta mambo ni tofauti kabisa.
Hakuna mishe inayokosa challenge mkuu, hata ukiajiriwa tu zipo sembuse biz yako mwenyewe
 
Mbona mpo Negative hivo? Ni shughuli gani ya ujasiriamali haina changamoto?
kila kazi ina changamoto na ili itoboe inahitaji uvumilivu sana tu, ninachokosoa ni mtu kuipamba kazi flani kama vile ni rahisi mno.
Unakumbuka forex ilivyotambulishwa na watu wengi wakakimbilia wakijua ni kudownload pesa tu.
 
Hapo nimekusoma mkuu
 
Hakuna mishe inayokosa challenge mkuu, hata ukiajiriwa tu zipo sembuse biz yako mwenyewe
hatukatai kwamba kuna chalenges kwa kila mwanadamu afanyalo, my point is - anza business with low expectation. mtu akisoma bandiko hapo juu hakawii kukimbia benki kukopa pesa illi awahi kupata nyingi zaidi.

Ufugaji wa kuku umeaza kitambo sana miaka ya 60's - fanya upelelezi ni matajiri wangapi wamepitia ufugaji huu wa kuku?
 
Najarbu Mungu anismamie 🙏
Kila la kheli.
"Angalizo" tafuta jogoo mzuri anayepanda sana asiwe mnene sana wala asiwe chotara,baada ya hapo jifunze namna nzuri ya kutunza vifaranga hapo utatoboa hata kama kwa miaka miwili au mitatu utatoboa..
 
nyumba za kupanga mtihani kweli kweli, shamba kuku ni elfu 6 tu
Ndugu tena hizi nyumba za kupanga ndio nzuri,binafsi nafuga kuku kwenye nyumba ya kupanga,naitumia kodi yangu vizuri,siwezi kuliacha eneo bure ilhali naweza kulitumia kwa shughuli za kuniingizia pesa,shtuka,tumia fursa..
 
Hii michanganua kwa kuisoma hivi tu inaonekana ni simple ila ukienda field sasa.
ni simple kulingana na eneo husika mfano iringa upatikanaji wa maeneo ni rahisi unaweza pata hata ekari 1 kwa 250,000 na karib na mjini pia materials kama mabanzi ni sawana bure tuu!! Kwa sehem nyingine ni tofauti so inayofautiana kulingana na sehem uliyopo!
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
Ni. Kweli mkuu jamaa ameshindwa kuchanganua labda kacopy sehem ukiwa na kuku 10 mitetea na jogoo 1 ukawalisha vizuri chakula chenye mchanganyiko wa
Mashudu
Damu
Chokaa
Mfupa
Pumba
Kwa muda wa week 2 wataanza kutaga lets say kila kuku akitamia mayai 100
Baada ya kutotoa week 1 baadae unawanyanganya vifaranga kwa mama zao. Hao vifaranga unawapa chakula cha vifaranga huwa kinauzwa maduka y vyakula kilo moja sh 1500 huku ukiwapatia joto kwa taa ya umeme au chemli!
Hao mitetea uliowanyanganya vifaranga wakila vizuri chakula chenye mchanganyiko maalum nilioelezea hapo juu ndani ya week 2-3 wataanza kutaga tena na kuatamia wakitotoa baada ya wee1 unawanyanganya Tena vifaranga!
Fanya hivyo kwa miez 6 utakua na kuku wenhi
 
Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Kuku-kupatana.jpg

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.

Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
Shukran
 
Ni idea sahihi na ina ukweli unaowezekana ndani yake...

Binaafsi pia ni mfugaji... Alichosahau ni suala la magonjwa na urahisi wa kufa kwa mifugo.... Izo kinga alizozisem mazee zinatibu kibahat bahat unaweza ukawapa na ukakuta woote wamekufa asubuh.....

Alafu karahisisha saaana..... Lazima upambane sio simple kama unavyosoma.

Changamoto ya kuku ni hapo tu..... Kwingine koote hakuna tatizo kabiisa. Na inawezkan...
Bro upo mkoa gan
 
Back
Top Bottom