Kuwa mkweli, mara yako ya mwisho kwenda nyumba ya ibada ilikuwa lini

jokotinda_Jr

JF-Expert Member
Apr 9, 2022
882
1,521
Naamini kila moja Ana kile anacho kiamini lakini hiyo bado haikufungi wewe kwenda kwenye nyumba ya ibada ...ijapokuwa enzi za mqbabu zetu cjui kama kulikuwa kama ivi sasa utandawazi umekuwa mwingi sana

Imefika kipindi watu wana hoji baadhi ya maswali ambayo zamani yalokuwa nadra sana mfano .. sahvi watu wanahiji uwepo wa MUNGU nakadhalika ... japo hili halikuwa mada yangu kwa Leo..... sasa basi naomba kukuliza mara yako ya mwisho kwenda NYUMBA YA IBADA ILIKUWA LINI?
42359-church-ThinkstockPhotos-139605937.1200w.tn.jpg
nft.jpg
 
Niliacha kwenda tangu walipo ongeza michango ya kanisani.
1.Sadaka ya Zaka.
2.Sadaka ya jumapili.
3.Sadaka ya mavuno.
4.Sadaka ya jumuiya.
5.Michango ya harusi.
6.Michango ya misiba.
7.Michango ya viti vya jumuiya.
8.Michango ya kigango.
9.Michango ya jengo la paroko.
10.Michango ya ukarabati wa kanisa.
 
Toka mwaka 2017.

nilienda.kuombewa maana mchungaji alisifika sana kusaidia vijana kupata ajira.

nilienda kwa kulazimishwa na shemeji yangu, nikaona nitafute siku tulivu tu, katikati ya wiki.

nikaenda kweli bwana, nikamkuta mchungaji hapo.

tukapiga story za hapa na pale, akaniuliza mengi kuhusu.mimi, nikamueleza tu wazi wazi.

Kuna kipengele alisikia kwenye mazungumzo, kwamba nina laptop.

Cha ajabu akaitaka ile Pc kwa nguvu niipeleke kanisani kama sadaka ili nifanyiwe maombi nizidi kufanikiwa😂😂😅😅😅

Yule mwamba sitamsahau, nilimkubalia tu ili niweze kuondoka kiroho safi, baada ya hapo hakuniona tena.

Pc ya laki 5, nilitaka kuiuza nifanye biashara niendeshe maisha, mara pastor kaitaka.

Dah, niliendapo baada ya miezi miwili nikaambiwa kanisa lilishakufaga😂😂

Sadaka ni nyingi sana makanisani..tunaandikwa hadi majina yetu kwenye bahasha na Hela tulizotoa.

miujiza feki ni mingi sana..

hivyo vigezo vinatukimbiza sana kwenye nyumba za ibada.
 
Naamini kila moja Ana kile anacho kiamini lakini hiyo bado haikufungi wewe kwenda kwenye nyumba ya ibada ...ijapokuwa enzi za mqbabu zetu cjui kama kulikuwa kama ivi sasa utandawazi umekuwa mwingi sana

Imefika kipindi watu wana hoji baadhi ya maswali ambayo zamani yalokuwa nadra sana mfano .. sahvi watu wanahiji uwepo wa MUNGU nakadhalika ... japo hili halikuwa mada yangu kwa Leo..... sasa basi naomba kukuliza mara yako ya mwisho kwenda NYUMBA YA IBADA ILIKUWA LINI? View attachment 2182463View attachment 2182464
ilikuwa ni tar 15.5.1995 ilikuwa ndio siku nimepata komunio..
 
Niliacha kwenda tangu walipo ongeza michango ya kanisani.
1.Sadaka ya Zaka.
2.Sadaka ya jumapili.
3.Sadaka ya mavuno.
4.Sadaka ya jumuiya.
5.Michango ya harusi.
6.Michango ya misiba.
7.Michango ya viti vya jumuiya.
8.Michango ya kigango.
9.Michango ya jengo la paroko.
10.Michango ya ukarabati wa kanisa.
Mi nimechelewa sana Ila nimeshaungana nawe bro.
 
Niliacha kwenda tangu walipo ongeza michango ya kanisani.
1.Sadaka ya Zaka.
2.Sadaka ya jumapili.
3.Sadaka ya mavuno.
4.Sadaka ya jumuiya.
5.Michango ya harusi.
6.Michango ya misiba.
7.Michango ya viti vya jumuiya.
8.Michango ya kigango.
9.Michango ya jengo la paroko.
10.Michango ya ukarabati wa kanisa.
Lakini kanuni ya kupokea ni kutoa mkuu
 
Dah! Umejuaje mzee, baada ya kama miaka miwili na kitu hiviii leo ndio nimeenda kanisani. Nimejisikia amani na raha japo mwishoni nilikerwa kidogo na ratiba.
Kwenye kibao kinachoonesha mpangilio wa ibada kinasema ibada inaanza saa nne kamili asbuhi hadi saa saba kamili mchana, lakini hadi saa tisa kasoro bado mambo yanaendelea nikaamua kusepa.
Nimeamua kuanza kuhudhuria kanisani tena
 
Niliacha kwenda tangu walipo ongeza michango ya kanisani.
1.Sadaka ya Zaka.
2.Sadaka ya jumapili.
3.Sadaka ya mavuno.
4.Sadaka ya jumuiya.
5.Michango ya harusi.
6.Michango ya misiba.
7.Michango ya viti vya jumuiya.
8.Michango ya kigango.
9.Michango ya jengo la paroko.
10.Michango ya ukarabati wa kanisa.
Sasa hivi tunachangia parokia aisee. Ndo tunamalizia madeni ya kiwanja. Tunemegwa parokia ya kimara. Hapa korogwe kigango ni parokia teule. Tunasubiria michago ya ujenzi. Hapa tunaendelea na mingine kama kawa

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom