Mara ya mwisho kusindikizwa na familia yako yote kwa safari, ilikuwa lini?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,174
39,934
Kuna siku nilikuwa nasafiri, natokea Arusha kuja Dar kwa usafiri wa basi.

Nimefika kituo cha basi asubuhi kama saa 11.45; pembeni ya basi niliona vijana wakihindi kama saba hivi; wakiume na wakike.

Mi nikapanda kwenye basi na kukaa kwenye siti niliyopangiwa.

Nilipokuwa ndani, nikawa nawaangalia wale wahindi; nikawa najiuliza wanasubiri nini hapo chini?

Nilipoangalia vizuri ndani ya basi, ndipo nikamuona mzee mmoja wa kihindi.

Baada ya kudadisi; nikagundua wale vijana ni watoto wa yule mzee; na wamekuja kumsindikiza mzee wao kwa safari.

Basi lilipoanza kuondoka, wakapungiana mikono na watoto wakaondoka.

Ule ukarimu wa namna hiyo, ulinifikirisha sana; kwa sababu huo ukarimu ulishaisha tangu miaka ya 90 kwa waafrika walio wengi.

Wakuu nawauliza; mara ya mwisho kusindikizwa na familia yako yote kwa safari, ilikuwa lini?
 
Kwa Kweli Mimi mwisho ilikuwa mwaka jana tukiwa wote nyumbani kwa Mzee
Wote walitoka nje na gari lilipokuja tukaagana nikapanda huyooooo
Au lazima Basi
Popote pale, iwe uwanja wa ndege, kituo cha basi n.k...yaani waache mambo yao yote na wafuatane na wewe mpaka kituo husika, na sio dereva akupeleke yeye mwenyewe kwenye kituo cha usafiri
 
Popote pale, iwe uwanja wa ndege, kituo cha basi n.k...yaani waache mambo yao yote na wafuatane na wewe mpaka kituo husika, na sio dereva akupeleke yeye mwenyewe kwenye kituo cha usafiri

Sisi home bado tunasindikizana
Hata kama ni wawili au watatu lakini hatuwezi kumuacha mtu aende peke yake

Najua ni old fashioned kama wengine wanavyoona lakini bado tunatumia njia hiyo na ni heshima pia kumbukumbu na furaha iliyochanganyika na huzuni maana hujui mtaonana lini tena

Na Ndio maana kila mmoja anataka kusindikiza
 
Daah hi kwetu tofauti.. labda ila kwangu mimi naondokaga man alone an tunaagana usiku asubuhi nikiamka ni mi mwenyewe tu.. au na mtu mmja bhasi wengine tulishamalizana usiku na huyo mmoja ananifikisha stendi alafu huyo anaweza ondoka na mi ndo nishazoea an
 
Sisi wanafamilia owte lazma waamke siku ya asubuhi ya safari inaombwa dua/ sala ya pamoja ya kumuombea anayesafiri afike salama bada ya hapo mmoja tu ndio amasindikiza hadi stand kama kuna mizigo mingi ka hakuna unasepa one man army
 
Kuna siku nilikuwa nasafiri, natokea Arusha kuja Dar kwa usafiri wa basi.

Nimefika kituo cha basi asubuhi kama saa 11.45; pembeni ya basi niliona vijana wakihindi kama saba hivi; wakiume na wakike.

Mi nikapanda kwenye basi na kukaa kwenye siti niliyopangiwa.

Nilipokuwa ndani, nikawa nawaangalia wale wahindi; nikawa najiuliza wanasubiri nini hapo chini?

Nilipoangalia vizuri ndani ya basi, ndipo nikamuona mzee mmoja wa kihindi.

Baada ya kudadisi; nikagundua wale vijana ni watoto wa yule mzee; na wamekuja kumsindikiza mzee wao kwa safari.

Basi lilipoanza kuondoka, wakapungiana mikono na watoto wakaondoka.

Ule ukarimu wa namna hiyo, ulinifikirisha sana; kwa sababu huo ukarimu ulishaisha tangu miaka ya 90 kwa waafrika walio wengi.

Wakuu nawauliza; mara ya mwisho kusindikizwa na familia yako yote kwa safari, ilikuwa lini?
Umasikini huindoa ukarimu wa kweli.
Familia zenye pesa hasa baba mshikamano bado upo. Ukikohoa tu umezungukwa na familia.
 
Mwisho kipindi naishi kwetu ila tokea baba yangu afe hakuna mtu anayefuata tena utaratibu huo .
Ila ilikuwa mnaamka baba anaomba nakuhakikisha kumuombea muhusika na badhi wanamsindikiza aendako.
 
Back
Top Bottom