Ni lini ilikuwa mara ya mwisho kula matunda, kufanya mazoezi, kumeza dawa za minyoo na kupima afya?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,379
6,931
Wabantu wengi hatuna jadi ya kula matunda kufanya mazoezi kumeza dawa za minyoo kupima afya mara tuuguapo hadi tushauriwe na daktari ndio mtu anaanza kutafuta au kufanya mazoezi.

Mfano dawa za minyoo ni muhimu kutumia kila baada ya siku 90 au miezi mitatu hapa hadi mtu asikie tumbo linamsumbua ndio anaanza kubuni majibu yake kichwani. ..huenda ni minyoo typhoid au amoeba. Hili suala halihitaji daktari Bali jijengee mazoea.

Kupima afya ni muhimu mara uuguapo, wengi wetu hubuni na kumeza dawa za kila aina ikishindikana ndio mtu anajilazimisha kwenda hospitali kupima, wakati inawezekana ungepona mapema baada ya kugundua tatizo.

Kufanya mazoezi hasa kwa wanaotembea wakiwa wamekaa yaani wamiliki wa vyombo vya moto hadi waugue na kushauriwa kafanye mazoezi ndio anaanza kufanya mazoezi ya viungo.

Kula matunda ndio kichekesho hadi akutane nalo katika pitapita zake Tena awe na hamu nalo ndio ananunua unakuta halikuepo na kwenye akili yake na mipango yake. At least wanawake wanaenda sokoni mara kwa Mara au mtu hadi ashauriwe na daktari ndio anaanza kula.

Mwisho wako wa kufanya mazoezi au kula tunda na kumeza dawa za minyoo ilikua lini?

NB: Vitu vingine ni gharama na inategemea na uchumi wako, usiishi kwa kuiga mfano walioko mjini matunda ni bei ghali Sana lakini hata mara Moja Moja sio mbaya.

Kutokana na kazi unayofanya hauhitaji kupiga mazoezi kabisa au ni kupiga kwa kusawazisha viungo na kuweka mwili sawa, mfano kupiga zege, kulima nk.
 
Mungu ni mwema sana, jana nilipima vipimo vyote, niko salama salmini. Vijana kabla ya kuingia penzi jipya pima. Hata kama upo tu jizoeshe kupima afya. Acha Mungu aitwe Mungu 🙏🙏🙏
 
Mungu ni mwema sana, jana nilipima vipimo vyote, niko salama salmini. Vijana kabla ya kuingia penzi jipya pima. Hata kama upo tu jizoeshe kupima afya. Acha Mungu aitwe Mungu 🙏🙏🙏
Kwa hiyo yalikuwa maandalizi ya safari mpya eee😁😁
 
Back
Top Bottom