Mimi nawaamini,nawaweka huru,lakini nahakikisha wanatumia muda vizuri kwa maana baada ya kurudi kutoka shuleni mchana,jioni wanarudi tution,toka walipokuwa chekechea,napenda wajichanganye na wenzao kwenye michezo mbalimbali,nafuatilia sana ili nijue uwezo wa kila mmoja kipaji chake ni nini?sijawahi kupiga hata kofi watoto wangu toka wazaliwe mpaka sasa,wakikosea huwa nawaeleza tu kwa upole namna iliwapasa wafanye,wananipenda hatari,wamenizoea kama babu yao,kwenye mapungufu yangu ya malezi mama yao hunisaidia, hasa upande wa (vipigo).nawaombea mwisho mwema,bado safari ndefu,mambo hubadilika.