Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,619
- 46,259
Silaha za laser "Laser weapons" ndio silaha zinazotegemewa kuwa silaha za viwango vya juu zaidi duniani kuyasaidia majeshi dhidi ya makombora yote katika karne ya 21.
Silaha za laser ni silaha za aina gani?
Silaha za laser ni silaha zitakazokuwa zinatumia nguvu za miale ya laser kuharibu mifumo ya vifaa vya kijeshi kama maroketi, helicopters, ndege, rada, makombora n.k ishindwe kufanya kazi zake, kutembea au ishindwe kulipuka kama ilivyokusidwa kwenye target yake pale miale hiyo ya laser inapoelekezwa katika vifaa hivyo.
Hizi ni silaha mojawapo katika kundi la silaha zinazoitwa Directed Energy Weapons (DEW), nyingine ya silaha katika kundi hili zitakuwa ni za microwaves, particle beams na sound beams.
Jinsi gani silaha za laser zitabadilisha sanaa ya vita?
Ikiwa zitafanikiwa kwa kiwango kikubwa wale watakaokua wanazimiliki watapata faida kubwa katika vita kwa sababu watakuwa wana uwezo wa kuharibu ufanyaji kazi wa silaha, nyenzo na vifaa vingi muhimu vya kijeshi vya kisasa vinavyowasaidia wanajeshi katika mapambano, hii ina maana kitisho cha silaha kama za roketi na makombora kitapunguzwa sana na hivyo matokeo ya vita yataamuliwa zaidi na silaha za karibu kama bunduki na mapambano ya karibu ya moja kwa moja ya wanajeshi katika uwanja wa vita.
Nani anaongoza mbio za kuzipata silaha hizi?
Tangu mwaka 1999 Marekani walizitizama silaha za DEW kama teknolojia ya juu zaidi ya silaha katika karne ya 21 na Pentagon wakaanza kutengewa bajeti ya kufanya utafiti na kuanza kutengeneza silaha za aina hiyo za majaribio madogo madogo.
Baada ya majaribio madogo ya muda mrefu hatimaye Pentagon waliwapa kandarasi ya kutengeneza silaha kubwa makampuni mawili ya silaha ya Boeing na General Atomics Aeronautical Systems(GA-ASI). Majaribio ya kwanza ya silaha kubwa za kilowat 300 za laser yanatarajiwa kufanyika kuanzia mwaka 2022.
Matokeo yoyote ya majaribio hayo utakuwa mwanzo mwingine wa mchuano mkali wa mashindano ya silaha "arm race". Teknolojia inazidi kuwalipa walioamua kufikiri na kutazama mbele ya wakati siku zote.