Kuwa baba, kuwa mama, kuwa mzazi katika karne hii ya 21 .Tulonge maujuzi na changamoto

kuna neno la kujifunza.....zuri katika yote wanao wawe ni your real friend,,, wawe huru, wacheze na marafiki,,,ila unapaswa kutambua marafiki zao ni wa aina gani.....

Watambue wewe mzazi ndio wa kwanza kujua mahitaji yao, kalamu, daftari au baiskeli imeharibika, cheza nao....wafundishe michezo mipya.....na hakikisha unawapa nafasi ya kukupenda.....watoto ni zawadi tumepewa na MUNGU.
 
Watoto hapa tunaishia umri gani..?

Kuna umri unafika unahitaji kama mzazi kumwona mwanao ana uwezo wa kujiamulia na kujisimamia, ajue muda wa homework, kucheza, kuoga, kulala na kuamka.... kwa wadogo sana ni sawa kuwafanyia yote hayo ila kuzima TV sio kitu rahisi sana.

Nina vijana wakubwa (12yrs) namshukuru Mungu wanajua kila kitu kuwahusu, kuanzia masomo na ratiba zake hadi usafi wao na hata kupika vizuri.... ratiba ya TV ni 24/7 wakitaka walale saa sita au wakeshe ila asubuhi muda wa kwenda shule nitawaamsha bila mjadala so wanajielewa.

Changamoto pekee ni kuhusu ibada na mambo za dini, mimi sio mtu wa ibada kabisa japo nilifunzwa nikiwa mdogo hivyo nimekulia kwenye misingi hiyo natambua umuhimu wake basi tu nimekengeuka.... napiga nao misele wikendi ila kuhusu ibada naishia kuwahimiza tu waende wenyewe hivyo wanaendaga wakijisikia.
 
Nitajitahidi kuwa mama mlezi hata polisi na rafiki wa karibu sana na wanangu ambapo Nitajitahidi kubalance malezi
 
Back
Top Bottom