Kuwa baba, kuwa mama, kuwa mzazi katika karne hii ya 21 .Tulonge maujuzi na changamoto

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,124
56,554
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza.Awali ya yote hakuna mzazi yeyote mwenye akili timamu anaependa mwanae aharibikiwe,hivyo atafanya lolote liwezekanalo katika kumsaidia mwanae akue na kuwa mtu mzima atakaeweza kumudu mahitaji yake.

Wewe kama mzazi unafanya nini ili kumuandaa mwanao asije kuja marioo au mdangaji?
Kulea siyo lelemama kwa kweli.

Kwa mfano mimi kwangu hakuna kuangalia tv siku za wiki.TV ni week end peke yake.

Homeworks tunafanya wote yaani mambo ya makumi na mamoja ukiwa mzazi kwenye karne hii ya 21 unarudishwa hadi kwenye Sentensi ni nini.

Haya hebu naomba mtiririke mnavyofanya kuwa mzazi katika karne hii ya 21.
 
Asante mkuu mleta mada. Mimi tukishamaliza makumi na mamoja na ajue na namba aliyoshika kichwani...basi tunawekeana ahadi nataka 90-100 ili nitoe 200 ya Sambusa kinyume na hapo Sina hela

Nimepanga nianze kwenda nao kucheza mpira jumamosi wakilala wakiamka ile saa 10-10:30 tukawe mafutibola ( footballers)
 
Hii ni mada kubwa sana mm,hongera mtoa mada,,Kwakweli mimi niko makini sana kwa upande wa marafiki wa mwanangu,watoto wadogo wanaanza kuharibika kwa marafiki wanaocheza nao na wanaoshinda nao wakiwa rikizo..Tuweni makini sana kuwachagulia marafiki,,pia tuwape nafasi watoto,tuwasikilize matatizo yao wanavyojaribu kujieleza,mtoto anaweza kupata tatizo kubwa akashindwa kukueleza mzazi kwasababu humpi nafasi,umetanguliza ubabe,MTOTO ANAWEZA AKANYANYASWA KIJINSIA NA ASIKWAMBIE,AKIZOEA BASI UJUE NDO IMEKUWA TABIA YAKE..
 
Najitahidi sana kuwa rafiki wa wanangu ili wawe huru kwa kila jambo ni rahisi kumsoma mtoto, urafiki huo hauniwekei mipaka ya kuwachapa bakora pia kama sehemu ya onyo.........marafiki na mazingira wanayocheza watoto ni muhimu kuvifuatilia ivo vitu
 
Kuna vitu huwa navizingatia sana kwa watoto

1. Afya yao- usafi wao huwa nazingatia saana.

2. Nawajengea kujiamini

3. Marafiki wa wanangu huwa nakuwa nao makini

4. Nakwepa kuwabagua kwa namna yoyote, hapa wazazi tunafeli sana, ukiona mtoto ni mzembe au mkorofi, au mtundu au unamuona si mwenye uelewa sana huwa tunawatenga haswa wazazi wa kiume hivyo tunasababisha wamama kuwapenda saana watoto hawa hivyo huharibika saaana .

5. Nawasisititiza sana kuhusu kujisomea vitabu, kutumia muda vizuri !

6. TV siruhusu sana matumizi yake.

7. Nina mpango wa kuwafundisha computer katika umri wao mdogo najua uhitaji wa kompyuta kwa sasa .

8. Nawafundisha sana kuhusu kujitegemea, bajeti na uchumi kwa ufupi !

9. Naandaa utaratibu wa kuwafundisha kuhusu kutoa, nataka wajua kutoa ni bora kuliko kupokea
 
Mimi nawaamini,nawaweka huru,lakini nahakikisha wanatumia muda vizuri kwa maana baada ya kurudi kutoka shuleni mchana,jioni wanarudi tution,toka walipokuwa chekechea,napenda wajichanganye na wenzao kwenye michezo mbalimbali,nafuatilia sana ili nijue uwezo wa kila mmoja kipaji chake ni nini?sijawahi kupiga hata kofi watoto wangu toka wazaliwe mpaka sasa,wakikosea huwa nawaeleza tu kwa upole namna iliwapasa wafanye,wananipenda hatari,wamenizoea kama babu yao,kwenye mapungufu yangu ya malezi mama yao hunisaidia, hasa upande wa (vipigo).nawaombea mwisho mwema,bado safari ndefu,mambo hubadilika.
 
Nimejifunza na naendelea kujifunza
Uko sahihi lkn pia watoto wanarthi baathi ya tabia na marathi kutoka kwa wazazi hivyo ukitaka kizazi bora na ww mwenyewe uwe bora mtu chapombe lkn ambiwa hataki mwanawe anywe changudoa lkn bint akileta wanaume anavimba
 
Najaribu sana kuangalia vipaji walivyonavyo kwa sababu naamini vipaji vinalipa zaidi.....kuhusu kielimu najitahidi waende shule,na kuusu kiimani na maadili huwa wanaenda kanisani.Na pia najitahidi wanielewe tabia zangu halisi
 
Bado niko najifunza Niko kwenye kulea na kichanga cha mwezi huwa na muomba Mungu amkinge mwanangu hatari zote za kiroho na mwili huwa najitahd kumnenea mema à
 
Hata sifuri ni hasi ikilinganishwa na chanya. Hata sifuri ni chanya ikilinganishwa na hasi. Hata chanya ni sifuri ikilinganishwa na chanya na ni hasi ikilinganishwa na chanya zaidi yake. Mama mdangaji, baba mario wazazi hawa wanapigaa ili mtoto aje awe nani wakati asipokuwa katika kundi lao ni sawa na wameharibikiwa
Tafsiri ya kuharibikiwa ni pana sana. Maana ni kinyume cha marengo bila kujari uzuri ama ubaya wa lengo. Kule msoma mtoto anaenda kuiba ng'ombe akizileta ni kidume wakati usukumani ukileta ng'ombe ya wizi myumbani hata baba anaweza kukuchoma moto.
 
Kama kuna matabia ya kurithi basi kuna vitu sitaki wavibebe kutoka kwangu(wazee wangu), kutoka kwao(wazee wake). Nafanyaje hapo?

Muda ni changamoto kubwa, mostly saa moja na nusu ndio natia mguu home, najuaje wameshindaje kwa mda mfupi tunaokaa na kuongea?

Naweza kuwachagulia marafiki?

Jinsi gani kuwa-intergrate na teknohama bila kuathiri makuzi yao?

Vipi nawasaidia kumfahamu Mungu wakati siendi kanisani, je nyumbani tu kunatosha kutoa elimu ya kimungu?

Aah mambo ni mengi!!
 
Mnasaidiana majukumu na mkeo weekend unakaa na wanao kwa ukaribu
Kama kuna matabia ya kurithi basi kuna vitu sitaki wavibebe kutoka kwangu(wazee wangu), kutoka kwao(wazee wake). Nafanyaje hapo?

Muda ni changamoto kubwa, mostly saa moja na nusu ndio natia mguu home, najuaje wameshindaje kwa mda mfupi tunaokaa na kuongea?

Naweza kuwachagulia marafiki?

Jinsi gani kuwa-intergrate na teknohama bila kuathiri makuzi yao?

Vipi nawasaidia kumfahamu Mungu wakati siendi kanisani, je nyumbani tu kunatosha kutoa elimu ya kimungu?

Aah mambo ni mengi!!
 
Wazazi wengi tumesahau wajibu wetu kama wazazi badala yake tumewaachia waalimu na wasaidizi wa kazi watulelee watoto.
Tuko busy sana hatujui hata kama mtoto kaoga.

Nionavyo mimi, si sahihi mtoto kuzurula kwenye nyumba za watu. Kuwa na marafiki.

Mnunulie mtoto michezo kama baiskeli ili apotezee muda wake hapo kuliko kwenda nyumba za watu...

Fatilia sana wasaidizi wa kazi kama hauna muda wa kumlea mtoto.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom