Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dr. Edwin Mhede ndiye pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB.
TRA ndiye mkusanya kodi na mapato wa nchi hii wakati NMB ni mmoja wa walipakodi. Bodi ya Wakurugenzi ndiyo itoayo maamuzi makubwa ya kikampuni ikiwemo kuteua, kukopa na kadhalika.
Kutokana na uelewa wangu huo wa TRA na Bodi ya Wakurugenzi, ni sawa/sahihi kwa Kamishna Mkuu wa TRA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, mmoja wa walipakodi? Hakuna mgongano wowote wa kimaslahi katika utendaji kazi wake?