ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,064
- 49,751
Naona banks zimeingia kwenye ushindani wa bonds Kufuatia kuimarika Kwa Biashara ya mikopo yaani watu na kampuni za biashara zinamiminika sana kukopa hivyo banks zinalazimika kutafuta pesa Kwa Ajili ya kukidhi soko la mikopo.
Baada ya CRDB kuzindua Kijani Bond yenye thamani ya Dola za Marekani 300 sawa na zaidi ya bil.700 za Madafu,NMB nao wamekuja na kubwa kuliko inaitwa Jamii Bond ya Trilioni Moja.
Haya kwenu wenye mapesa Yao kama Wastaafu na wengine mnaofikitia muwekeze nini na wapi ,katunzeni mapesa yenu huko kwenye banks.
Kwa hatua hizi ni wazi Uchumi unazidi kufunguka na Biashara zimerejea Kwa Kasi sana.
======
Benki ya NMB hii leo imezindua na kutangaza rasmi dirisha la uwekezaji wa toleo la kwanza la kuuzwa kwa hati fungani iliyopewa jina la hati fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond) yenye lengo la kukusanya fedha ambazo zitawezesha utolewaji wa mikopo yenye kuleta matokeo chanya kwenye jamii kupitia miradi ya mazingira, afya, elimu, wanawake na vijana, pamoja na miradi inayolenga kuhakikisha usalama wa chakula.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akiongea katika halfa ya uzinduzi huo amesema “Lengo letu ni kukusanya Tsh. bilioni 75, tunaishukuru Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kwa kuruhusu ongezeko la mpaka Tsh. bilioni 25, pia idhinisho la USD million 10 limetolewa, na kuruhusu ongezeko la mpaka USD milioni 5, ambapo jumla inafikia USD milioni 15, itakayouzwa kwa Mashirika na Wawekezaji walioko nje ya Tanzania"
Hati hii fungani ya NMB Jamii imepewa muda wa uwekezaji wa miaka mitatu ambapo Wawekezaji watapata riba ya asilimia 9.5 kwa mwaka na kulipwa mara nne huku kiwango cha chini cha uwekezaji kikiwa ni Shilingi laki tano (500,000) ambapo dirisha hilo la Uwekezaji likitegemewa kufungwa Octoer 27, 2023.
Benki ya NMB pia imezindua programu ya muda wa kati (Multicurrency Medium Term Note – MTN) ya miaka kumi yenye jumla ya Tsh. trilioni moja iliyopewa idhini na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kwa muda wa miaka 10.
Hafla hiyo imefanyika Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi Nehemiah Mchechu ambaye ni Msajili Mkuu wa Hazina akiambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.