Tunaomba Serikali iwasimamishe kazi Kamishna Mkuu TRA, Kamishna Kodi za ndani na Meneja wa kodi Kariakoo TRA

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,218
39,052
Wakubwa habari zenu.

Kamishna mkuu wa sasa Kidata toka apewe hii ofisi kumekua na ongezeko la kodi zisizo na tija kwa walipa kodi. Ameleta sheria nyingi ambazo zimeshindwa kuwasaidia walipa Kodi bali zinawakandamiza.

Nikiangalia uongozi wa Mhede na kidata Mhede yuko mbele sana aliweza kuwabana walipakodi wakubwa sisi wadogo tulifanya biashara vizuri na tulikua tunalipa kodi wala hakukua na manung’uniko. Mhede alitumia “Progressive Tax system” lakin kwa sasa hawa walipa kodi wakubwa ndo wakwepaji tunakuja kamatwa sisi vidagaa.

Nikiangalia uongozi wa Mapembe aliyekua kamishna kodi za ndani huwezi fananisha na Kyabemela huyu jamaa sioni impact yake kwenye kusaidia walipa kodi. Mapembe alikua kichwa sna na tumeona impact yake kwenye DRD, Domestic Revenue.

Meneja Kariakoo ameshindwa kukaa na sisi wafanyabiashara na kutusikiliza kero zetu ila amekua akiwatuma vijana mtaani kukamata mizigo hovyo na sio waelewa kabisa. Wameweka maslah mbele kuliko utu imagine huna kosa na mtu anataka uumpe Million 2 kweli hii haki??. Biashara zimekua ngumu mtu anataka hiyo amount ni sawa? Afu ukicheki ni kijana mdogo sana hata maisha hajajua hapo anataka gari kali, madem wazuri na pombe.

Hawa vijana ni wadogo kama mmewaajir bhs mmeajiri majambazi na wala rushwa hawana utu kabisa. TRA tafuteni mbadala wa kuajiri sio unamchukua mtu kakaa kitaa muda mrefu unampa kazi ya kukusanya kodi unategemea nini? TRA Kariakoo wale vijana mliowaajiri mwaka 2019 wako wapi?

Nilipataga habari walikua intern. Hawa vijana walikua wazuri sana walikua na utu, na walitupa sana elimu ya kodi. Bora hata mngeajir hawa kuliko haya majizi hasa pale Karikaoo bila kutoa hela hupati huduma utawekwa weeh mbaka kero.

Mama yetu kipenzi Samia tunaomba uwaondoe hao watu juu hawana msaada kwako. TRA ya sasa imejaa Rushwa na uonevu mkubwa pamoja na kukomoana.

.
IMG_0868.jpg
 
Hao ndio watu wanaotamba awamu hii, serikali hii ni zaidi ya dhaifu!

We subiri muda sio mrefu WATAOMBWA watupishe...fanyamasihara na mswahili wewe!!.
 
Poleni wafanyabiashara ndio nchi ilivyo hii hawajali mfanyabiashara ataumia au laa
 
Back
Top Bottom