SoC04 Kutungwa sheria kwa viongozi watakaoshindwa kutatua matatizo walioahidi kwa wananchi awamu iliyopita kutopata nafasi ya kugombea katika awamu zijazo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Littledidah

New Member
May 13, 2024
3
3
TANZANIA TUITAKAYO

Nchini Tanzania wananchi uingia mkataba na viongozi kwa muda wa miaka mitano kwa lengo la kuboresha sehemu zenye mapungufu na kutatua kero na changamoto za wananchi katika nyanja mbalimbali. Swali ni kwamba ndani ya hiyo miaka mitano hadi kukamilika miaka hiyo, viongozi hutimiza yale waliyoahidi kwa wananchi? na kama hawajatimiza wala kutatua changamoto za wananchi kuna sheria yoyote inayowabana viongozi kwa kutotimiza wajibu wao?.

UTANGULIZI

Uongozi ni uadilifu na utendaji kazi kwa kutimiza matakwa ya wananchi katika sehemu husika, uongozi ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa katika uangalifu mkubwa nchini, kwasababu kila Nyanja inahitaji kiongozi atakae simamia kwa kuboresha na kutatua matatizo yanayokumba nyanja husika ndio maaana kwenye elimu, afya, miundombinu, sanaa, habari, michezo na yyanja nyingine zote zina viongozi. Linapokuja suala la watu kupewa usukani wa kuongoza nchi, mikoa, wilaya na vijiji au kata ni suala la mkataba baina ya viongozi na wananchi kwa ujumla, na mkataba unapokamilika kila mtu katika mkataba huo anapaswa kutimiza wajibu wake kulingana na muda waliokubaliana na kama upande mmoja ukishindwa kutimiza wajibu wake lazima hatua za kisheria zifuatwe kulingana na wananchi na viongozi walivyokubaliana.

HALI HALISI NCHINI TANZANIA

Nchini Tanzania wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kwa watu wanaowaamini kwa kuwapa kura za ndio na kuweka imani kwa viongozi hao kwa kuamini kuwa watatatua changamoto na kutimiza matakwa ya wananchi, kitendo cha kupiga kura moja kwa moja huwaingiza wananchi kwenye mkataba na viongozi kwa muda wa miaka mitano kwa lengo la kuboresha sehemu zenye mapungufu na kutatua kero na changamoto za wananchi katika nyanja mbalimbali. Swali ni kwamba ndani ya hiyo miaka mitano hadi kukamilika miaka hiyo, viongozi hutimiza yale waliyoahidi kwa wananchi? na kama hawajatimiza wala kutatua changamoto za wananchi kuna sheria yoyote inayowabana viongozi kwa kutotimiza wajibu wao?.

Uhalisia nchini Tanzania viongozi wengi wanamaliza miaka yao mitano wakiwa madarakani bila kutoa matunda kwa wananchi waliowaamini viongozi hao kwa kuwapigia kura, lakini bado viongozi hao walioshindwa kutatua changamoto za wananchi hupewa nafasi za kugombea tena ilihali hawakufanya kitu cha msingi katika muda waliokuwa madarakani. Tanzania tuitakayo inahitaji sheria zaidi zinazowabana viongozi ili kutimiza majukumu yao na wajibu wao kwa wananchi, wananchi wanaweza kutoa maoni yao kwa viongozi kuhusu matakwa yao lakini kama hamna sheria inayowabana viongozi katika kutimiza matakwa ya wananchi itakuwa ni kazi bure kwani viongozi watafanya yale yanayo wanufaisha wao zaidi ya wananchi. Sheria ni muhimu sana katika kuweka watu mahala salama. Mfano mzuri ni shuleni, sheria zipo na wanafunzi wanaadhibiwa kutokana na makosa yao. Kwanini isitungwe sheria kwa viongozi wanaoshindwa kutimiza matakwa ya wananchi wa muda wa miaka mitano waliyokuwa madarakani?

UMUHIMU WA KUTUNGWA SHERIA KWA VIONGOZI WATAOSHINDWA KUTATUA MATATIZO WALIOAHIDI KWA WANANCHI.

Nchi ni hakuna sheria amabayo inawafunga viongozi kwa kushindwa kutatua changamoto za wananchi na kushindwa kuboresha sehemu zenye mapungufu kwa muda waliopo madarakani hadi kuisha kwa muda huo. Kuwepo na sheria inayowafunga viongozi wataoshindwa kutatua matatizo walioahidi kwa wananchi kutopewa nafasi ya kugombea tena. Kuna umuhimu wa kuongezwa kwa kifungu hicho kama ifuatavyo:

1. Sheria itachochea viongozi kuwa wa wajibikaji

Watu wengi siku hizi hutaka kuwa viongozi kwasababu ya uchu wa madaraka na wapo tayari kufanya lolote ili wasitoke madarakani, endapo ikitungwa sheria kwa viongozi wataoshindwa kutatua matatizo ya wananchi wao kutopewa nafasi ya kugombea kuwa viongozi, viongozi watakuwa wa wajibikaji katika sehemu wanazoongoza

2. Viongozi watafanya yale yanayoleta maendeleo

Viongozi wengi wanao wawakilisha wananchi katika majimbo mbalimbali nchini Tanzania wanaonekana wakifanya vitu ambavyo vipo nje na uongozi wao. Mfano mzuri ni bungeni siku hizi wabunge wamekuwa wakiongea vitu ambavyo havina manufaa katika maendeleo ya taifa kwa ujumla

MAPENDOKEZO

1. Baada ya uchaguzi na viongozi kupatikana, kila wilaya kuwe na mkataba baina ya wananchi na viongozi wao kwa kukubaliana baadhi ya vitu vya kutimiza kwa wananchi kama matakwa yao na pia kutatua changamoto za wananchi. Suala hili litampa chachu kiongozi kufikiria na kutendea kazi yale waliokubaliana na wananchi wao ( kwenye suala la mkataba hapa maoni ya wananchi yatachukuliwa na yale maoni yatayotolewa na wengi ndio yatakayo wekwa kwenye mkataba)

2. Katika ibala ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaonesha sifa ya mtu kuwa mgombea ubunge. ibala hiyo iongeze sheria ya kutowaruhusu viongozi walioshindwa kutatua changamoto za wananchi awamu iliyopita kugombea tena katika awamu zijayo. Kama mtu kashindwa kutatua matatizo za wananchi ndani ya miaka mitano kuna haja gani ya kumpa kijiti mtu huyo kugombea tena?

3. Sheria hiyo itayoongezwa katika ibala ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inabidi iwahusu viongozi wote ambao hawajakamilisha asilimia 80% ya ahadi zao kwa wananchi. Sheria hii ya kutowaruhusu viongozi walioshindwa kutimiza yale walio ahidi kwa wananchi wao haitawahusu viongozi waliojitahid kutimiza matakwa ya wananchi kwa 80%.

4. Kila baada ya mwaka mmoja kuwa na tathmini ya utekelezaji wa mkataba baina ya viongozi na wananchi. Suala hili litasaidia katika kutimiza yale waliokubaliana kati ya viongozi na wananchi kuliko kusubiri tathmini baada ya kuisha kwa miaka mitano

HITIMISHO

Ili yote haya yaweze kufanyiwa kazi, maoni ya wananchi yanabidi yapewe kipaumbele kwani wao ndio waliowaweka hao viongozi madarakani, wananchi pia washiriki katika kutoa maoni yao na kujua haki na wajibu wao kama wananchi, wananchi wajue pia sheria za nchi yao kwa ujumla. Mtu akiwa anajua sheria hata ujasiri wa kutoa maoni unakuwepo na hapo tutatokomeza wananchi wasiojiamini. Vilevile viongozi wafuate sheria na wajikite katika kutekeleza yale waliokubaliana na wananchi.
 
ni suala la mkataba baina ya viongozi na wananchi kwa ujumla, na mkataba unapokamilika kila mtu katika mkataba huo anapaswa kutimiza wajibu wake kulingana na muda waliokubaliana na kama upande mmoja ukishindwa kutimiza wajibu wake lazima hatua za kisheria zifuatwe kulingana na wananchi na viongozi walivyokubaliana.
Enhee, kimsingi hivi ndivyo ilivyo.

na kama hawajatimiza wala kutatua changamoto za wananchi kuna sheria yoyote inayowabana viongozi kwa kutotimiza wajibu wao?.
Nadhani katika demokrasia inayofanya kazi vema watahukumiwa na wananchi wao katika sanduku la kura.

Kila baada ya mwaka mmoja kuwa na tathmini ya utekelezaji wa mkataba baina ya viongozi na wananchi. Suala hili litasaidia katika kutimiza yale waliokubaliana kati ya viongozi na wananchi kuliko kusubiri tathmini baada ya kuisha kwa miaka mitano
Hii nzuri ndiyo maana kila projekt za kizungu zina kipengele cha monitoring and evaluation

. Vilevile viongozi wafuate sheria na wajikite katika kutekeleza yale waliokubaliana na wananchi.
Nao wananchi watimize wanachopaswa kufanya kama mtu hafai kura wasimpe. Itategemea pia tume ya uchaguzi itimize majukumu yake.
 
Enhee, kimsingi hivi ndivyo ilivyo.


Nadhani katika demokrasia inayofanya kazi vema watahukumiwa na wananchi wao katika sanduku la kura.


Hii nzuri ndiyo maana kila projekt za kizungu zina kipengele cha monitoring and evaluation


Nao wananchi watimize wanachopaswa kufanya kama mtu hafai kura wasimpe. Itategemea pia tume ya uchaguzi itimize majukumu yake.
Hakika, wananchi ndio wenye maamuzi ya kupata kiongoz bora.
 
Back
Top Bottom