jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Wanajamvi, hivi kutumia dola dhidi ya wapinzani wako siyo dalili za kuishiwa na hoja kwenye taifa linalojinadi kufuata mfumo wa kidemokrasia?
Sidhani kama ni sahihi kumfananisha Trump na siasa zetu kwenye suala la matumizi ya dola. Hakuna usawa wa mifano hiyo hata chembe!
Mambo mengi ambayo yanafanywa na dola ya Tanzania dhidi ya upinzani yana ufanano gani na yale anayoyafanya Trump na serikali yake dhidi ya chama pinzani cha Democrats?
Hakuna kufanana hata kidogo, kwanza wagombea wote kuna wakati inafikia wanapewa ulinzi “secret services” ambao ndo wako specialized kwenye usalama wa viongozi hao bila ya kujali chama anachotokea.
Kikubwa kinachofanyika, ni kuwahakikishia ulinzi wakati wanamwaga sera zao kwa wananchi. Tena akitokea anayevuruga mkutano anabebwa juu juu kama karatasi na kutupwa nje. Sasa huku kwetu dola ndo inasimamia ukandamizwaji wa haki, uvunjifu wa sheria na ukiukwaji wa katiba ya nchi yetu halafu katibu mkuu wa ccm ambaye ni professor anaongea maneno kama vile ni mipasho?
Mbunge wa chama chochote cha upinzani marekani anaweza kupigwa risasi mahali popote pale iwe ndani ama nje ya marekani(achilia mbali kwenye maeneo ya bunge kama Lissu), na dola isitumike kufanya uchunguzi? Unaifananisha marekani na Tanzania kwenye utu wa kuthaminiana wenyewe kwa wenyewe? Au mkuu alizungumzia matumizi ya dola kivipi? Anajitia upofu? Ama ni ulevi wa madaraka?
Viongozi ump wanaweza kuthubutu kuzivamia studio za CNN pamoja na kuziita “fake news” kila uchwao? Yaliyotokea cloudsvideo si zipo? Hivyo ndivyo namna ya kutumia dola kubaki madarakani ama ni udikteta?
Mifano iko mingi sana! Lakini kwa kifupi kauli hiyo ya katibu mkuu wa ccm inadhihirisha ukweli kwamba serikali inayotumia dola ili iweze kubaki madarakani, basi imeishiwa na hoja za kuwashawishi watanzania kuweza kuwachagua.
Dola kazi yake kwenye demokrasia, ni kusimamia uwanja sawa wa kila upande uweze kuziwakilisha hoja zake kwa wananchi bila bughudha yoyote ile! Na siyo kutumika na chama kimoja. Hilo likitokea, tunaweza kusema ni udikteta!
Pia nashauri kuwepo na midahalo ili wananchi tuweze kujiridhisha na siyo kupachikiwa viongozi tu bila kusikia uwezo wao wa kusimamia hoja.
Rais ni nembo ya kwanza na mwakilishi wa kwanza kwa Taifa hata nje ya nchi.
Ukimpata rais ambaye hajui mdahalo, kuna uwezekano akawa katili. Ndo maana hatuoni mijadala ya bunge live ili wananchi tuwe proud kuhusu demokrasia yetu na kuona mchango wetu kwa Taifa kupitia wawakilishi wetu nk.
Tungekuwa na midahalo ya wazi na mfumo mzuri, aliyoyahoji Ben Saanane yangeshapatiwa majibu kabla ya mtu kuingia ikulu na Ben kutekwa na kupoteza maisha yake.