hayacola

New Member
Nov 3, 2023
2
2
Habari wana JF
Naomba uzoefu Kwa mtu ambaye amekuwa akisafiri kwenda Kenya na ana akaunti NMB je akiwa Kenya aliweza kutumia huduma za kwenye app ya NMB mfano kutuma pesa kwenda mitandao ya simu?

Kwa kifupi issue yangu iko hivi nina akaunti NMB nitaenda Kenya hivi karibuni nikiwa huko nitakuwa na miamala ya kutuma pesa kwa namba za simu zilizo mitandao ya Tanzania kwa kutumia app ya NMB. Sasa wasiwasi wangu ni kuwa isije kuwa app ya NMB haifanyi kazi nje ya nchi, japo nmb wanadai ukifanya roaming sometime huwa app inafanya kazi. Sasa nataka nipate nipate uzoefu wa mtu ili malipo yasikwame. Kingine NMB app nilijisajili kwa line ya halotel sasa hapa bongo tu wakati mwingine inasumbua sasa najiuliza je nikiwa Kenya na nikitaka kufanya roaming itakuwa rahisi kweli?

Au kama kuna mtu amekuwa akitumia huduma za KCB bank na Equity bank na kama ni rahisi zaidi kwa benk hizi naomba anipe uzoefu pia maana mahitaji yangu ni kutuma pesa mitandao ya simu ya Tanzania nikiwa kenya lakini vilevile niweze toa pesa nikiwa hukohuko Kenya kwa maana ya aidha kwenye tawi au ATM na hata kwa wakala ikiwezekana.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa watakaonisaidia

Ahsanteni

Hayacola
 
Mkuu tumia internet banking,,
Utatoa pesa popote ulipo na kwa mtandao wowote wa simu.

Waambiye bank wakuunganishe na huduma ya internet banking system.
 
Mkuu tumia internet banking,,
Utatoa pesa popote ulipo na kwa mtandao wowote wa simu.

Waambiye bank wakuunganishe na huduma ya internet banking system.
Mkuu hv ninaweza kutumia laini yangu ya tigopesa nika access tigopesa menu nikiwa Lebanon? Ntakua huko soon. Nna bank account na dtb na nna internet banking sema kuna miamala lazima nitumie hii laini ya tigo maana ake nihamishe from bank to tigopesa kisha nifanye hyo miamala
 
Back
Top Bottom