Kutongoza ni Haki ya Kiumbe wa Kiume tu?

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Jana ktk EATV "Strictly Kenyan" kulikuwa na mada kuhusu wanawake wa Kenya kuanza kwa kasi ya ajabu kutongoza wanaume. Wahojiwa walikuwa wanaume na wanawake; na wote waliliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa na kuliunga mkono. Lakini miye BAZAZI nina wasiwasi kama huo ni mpango wa YEHOVA Mungu. Ukiangalia wanyama na ndege wote utaona kuwa watongozaji ni wakiume. Kwa sababu hiyo ndio maana kwa Binadamu wanawake ni wazuri ili wawavutie wanaume lakini wanyama/ndege kwa vile hawana uwezo wa kuongea Mungu aliwafanya wa Kiume kuwa wazuri ili kuwafutia wanawake. Naomba kukosolewa kwa haki. Nawakilisha
 
Mwanamke kupewa haki au kujichukulia haki ya kutongoza ni tishio kubwa kwa wanaume maana nina uhakika hakuna mwanaume atakayekataa atongozwapo. Shida ni pale mshikaji unapohisi kuwa hata mkeo anaweza kutongoza washkaji zako, na una uhakika hawatakataa! Wanawake wasitongoze, sio poa hata kidogo, watulie tu kama mambo ya shepu nk yanalipa watatongozwa tu.
 
Kama mtu umemzimia mtu basi mwoneshe kuwa umemzimia....usisubiri aanze yeye la sivyo unaweza ukasubiri milele na kuishia kutokujua kile ambacho kingetokea laiti ungemwonesha au kumweleza hisia zako....sio lazima kumwambia kwa maneno.....matendo nayo yana sauti kubwa tu inayoweza kueleweka bila utata.
 
jana ktk eatv "strictly kenyan" kulikuwa na mada kuhusu wanawake wa kenya kuanza kwa kasi ya ajabu kutongoza wanaume. Wahojiwa walikuwa wanaume na wanawake; na wote waliliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa na kuliunga mkono. Lakini miye bazazi nina wasiwasi kama huo ni mpango wa yehova mungu. Ukiangalia wanyama na ndege wote utaona kuwa watongozaji ni wakiume. Kwa sababu hiyo ndio maana kwa binadamu wanawake ni wazuri ili wawavutie wanaume lakini wanyama/ndege kwa vile hawana uwezo wa kuongea mungu aliwafanya wa kiume kuwa wazuri ili kuwafutia wanawake. Naomba kukosolewa kwa haki. Nawakilisha
mimi kama mwanamme sioni kwanini mwanamke asitongoze kama akipenda.tatizo letu ni baadhi ya sisi wanaume sijui kutojiamini au ushamba.utakuta baada ya kutongozwa unatangaza mtaa mzima fulani ananitaka,sijui ili iweje?kumbuka ni bora uwe na mpenzi ulie na uhakika kuwa anakupenda.mimi nasema kumtangaza ni ushamba wa hali ya juu.....akina mama kutongoza mi naona ruhsa.
 
tupeni basi mistari ya kuwatokea wakaka!...:behindsofa:
 
tupeni basi mistari ya kuwatokea wakaka!...:behindsofa:

Wala hamhitaji mistari....kwa yule unayemzimia wewe tabasamu, kuwa mchangamfu kuliko kawaida...nk.....utaona mwenyewe anakuanza....
 
tupeni basi mistari ya kuwatokea wakaka!...:behindsofa:

Bahati ya mtende hii huwa naililia sana.
Hapa mm naweza kuchomoka na kilo 2 maana nitakuwa nafagia tu hasa hasa manyambizi.
 
mimi kama mwanamme sioni kwanini mwanamke asitongoze kama akipenda.tatizo letu ni baadhi ya sisi wanaume sijui kutojiamini au ushamba.utakuta baada ya kutongozwa unatangaza mtaa mzima fulani ananitaka,sijui ili iweje?kumbuka ni bora uwe na mpenzi ulie na uhakika kuwa anakupenda.mimi nasema kumtangaza ni ushamba wa hali ya juu.....akina mama kutongoza mi naona ruhsa.

hapo ndo panakuwa tatizo, tena unamkubali unamtumia ipasavyo na unamtosa maana unamuona ni 'cheap stuff'

sijui kuna ubaya gani kama mwanamke atamwambia au kumwonesha mwanume anavyojisikia juu yake (may be its not african).....

nikishindwa kusema kwa maneno ntamwonesha kwa vitendo kwa kweli

hakuna ubaya kumpenda mwanaume....(nazungumzia true love na kumtamani hapa)
 
Mimi naona wachwe wajaribu ili waona kesheshe ambayo huwa tunakumbana nayo. Ni kawaida kutamani cha mwenzio ila ukikipata ndo unagundua kuwa labda si mali sana kama ulivyodhania. Experience is the best teacher. Naona akina dada waachwe wajaribu bahati zao life, badala ya kusubiri na wakati mwingine kufa na kihoro.
 
mimi kama mwanamme sioni kwanini mwanamke asitongoze kama akipenda.tatizo letu ni baadhi ya sisi wanaume sijui kutojiamini au ushamba.utakuta baada ya kutongozwa unatangaza mtaa mzima fulani ananitaka,sijui ili iweje?kumbuka ni bora uwe na mpenzi ulie na uhakika kuwa anakupenda.mimi nasema kumtangaza ni ushamba wa hali ya juu.....akina mama kutongoza mi naona ruhsa.

Hapo (red) ndo panapokuwa patamu ili waone kwamba mkuki ni kwa nguruwe...! Ukiacha mitaani, tabia ya kutangaza ipo sana kwenye hostels za vyuo. Sasa waache watangazwe ili na wao waweza kujua ni kwa kiasi gani inauma. Hiyo kitu ya kutangaza ilinifanya niwachukie sana wadada wa chuoni.
 
Mimi naona wachwe wajaribu ili waona kesheshe ambayo huwa tunakumbana nayo. Ni kawaida kutamani cha mwenzio ila ukikipata ndo unagundua kuwa labda si mali sana kama ulivyodhania. Experience is the best teacher. Naona akina dada waachwe wajaribu bahati zao life, badala ya kusubiri na wakati mwingine kufa na kihoro.

Mkuu!! waache waje tuwatwange vibuti wapate akili!
 
Mkuu!! waache waje tuwatwange vibuti wapate akili!

Kweli mkuu. Najua wapo wanawake wengi wanaona wivu kwamba hawana nafasi hiyo. Mimi naona wapewe tu. Najua kuna wengine baada ya hapo watatamani kurudi kama zamani na sina hakika kama kutakuwa na hiyo nafasi.

I wish this happened during my time. Si ajabu nilipoteza bahati nyingi kwa kutogundua dalili. Sasa ni direct attack, mdada anarusha missiles na AK47. Waliopo uwanjani kazi kwao. Naamni kelele za baadhi ya wanaume kwamba wanawake wengi wanaringa zitapungua, kwani yeyote (either mwanamke au mwanamume) anayeuona mchuma wa maana anawahi seat. Hii itakuwa movie nzuri sana kuitazama especially kwetu sisi vibogoyo!!
 
nikishindwa kusema kwa maneno ntamwonesha kwa vitendo kwa kweli

hakuna ubaya kumpenda mwanaume....(nazungumzia true love na kumtamani hapa)

Jaribu siku moja uone negative effect kudadadadeki.
 
Back
Top Bottom