Kutoka NACTE: Maombi ya Uhamisho kwa wanafunzi wanaoendelea

Humilis

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
881
1,034
Tafadhali soma kwa umakini taarifa na mahitaji muhimu ya kuhama kabla hujaanza kufanya maombi ya uhamisho.

Tarehe ya mwisho ya kuomba uhamisho ni 30-04-2022.

Masharti na Sifa kwa Waombaji, Taarifa kwa Waombaji:

1. Mwanafunzi anashauriwa kuhakiki na kufahamu taarifa za msingi za chuo anachotaka kuhamia kama vile, mahali chuo kilipo, hali ya hewa, ada na michango mingine. Kwa taarifa zaidi angalia kitabu cha muongozo wa udahili (Admission Guidebook) kupitia www.nacte.go.tz

2. Uhamisho unawahusu wanafunzi waliopo katika mwaka wa masomo 2023/2024 kwa mkupuo wa MACHI na 2022/2023 kwa mkupuo wa SEPTEMBA.

3. Mwanafunzi ataruhusiwa kuhama chuo kimoja kwenda kingine chenye kozi inayofanana
Mwanafunzi ambaye hajafaulu au kuwa na mtihani wa marudio hahusiki na uhamisho huu
Uhamisho utakubalika pale tu chuo unachotoka na unachotaka kuhamia vimedhiridhia.

4. Tarehe ya mwisho ya kuomba uhamisho ni 30-04-2022

Malipo

Gharama za mchakato wa uhamisho ni Tsh 10,000/=, Malipo yaliyopokelewa hayatarejeshwa.
 
Back
Top Bottom