Kutoka Mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka Mtwara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, Sep 27, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakuu kwa wiki mbili zilizopita nimekuwa sipo jf kwani nilikuwa safarini Mtwara kwa shughuli maalum na bahati mbaya sikupata hata nafasi ya kuingia internet cafe. Kila nilipojaribu kutafuta zilipo sikupata na muda wa shughuli yangu haukuniruhusu kupata wasaa huo.

  Nilijisikia kweli kumiss corner hii ya jf niliyoizoea.

  Niliwamiss members wengi wa jf kama akina NN na yoyo, mkandala, omutwale, lunyungu. invisible, junius, ngekewa, na siwezi kumaliza orodha yote hapa............

  Ninayo mengi ya kusema kuhusu Mtwara na picha kiasi za kuvutia za Mtwara.

  Mji ulio pembezoni mwa bahari ulio na beaches nyingi sana tena nzuri hata kupita hizi chafu zilizojaa harufu za Dar lakini zikiwa na wananchi maskini kweli kweli.

  Kwa kuwa sijapata muda mzuri nitakuja siku ingine kuelezea zaidi na kuweka picha.

  Sasa hivi niko safarini so stay tuned.
  MF
   
 2. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  ok ok thanx mkuu afadhali na hizo picha tutakumbuka mbali sana,nilifika pale mwaka 1998 kipindi mkuu wa mkoa aliitwa musa kaisi,ni kweli beach safi sana na hotel kubwa iliitwa tingatinga sijui bado ipo au?na kuna baa ya vigogo wa huko inaitwa mk bado ipo?na pale mikindani beach wale wenyeji wameacha tabia ya kukimbilia bichi kupata haja kubwa badala ya kujenga vyoo?usisahau picha ya ule mlango wa barabarani wakati unaingia lindi,pia daraja la mkapa
   
 3. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,575
  Likes Received: 923
  Trophy Points: 280
  Huyo mkuu wa mkoa sio Musa Kaisi ni Nsa Kaisi.Majina ya Kyela hayo mdau matamshi yake ndo yanapelekea mtu afikiri ni MUSA!Huyo jamaa ni komandoo kamili alisoma Cuba na kufuzu with flying colors akaja na personal letter toka kwa Rais Castro akimueleza Nyerere jinsi Nsa alivyo extraodinary!
   
 4. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  yaah asante kwa masahihisho mkuu na yule jamaa hata maamuzi yake yalikua ya kikomando tu maana nakumbuka tulienda kwaajili ya mkapa na muluzi walikua wanakabidhiana bandari ile muluzi atumie,jamaa akapiga mkwara kwamba hakuna kupika pale ikulu ndogo wakati lunch inahitajika sasaba kamili kwa waheshimiwa,ilibidi aje mbabe mwingine kutoka ikulu kutwambia lunch iwe tayari mda huo huyo kaisi ataongea nae yeye ndo kazi ikafanyika,namkumbuka sana huyo komandoo
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Unachosema una uhakika nacho?. Mimi nimefanya kazi na NSA Kaisi Singida wakati huo akiwa LT col.

  Ninavyoojua Nsa Kaisi sio Graduate na hata maamuzi yake ni ya moja kwa moja (Amri) kama walivyokuwa wanajeshi wengine. Sifa ninayompa na nilimpenda ni mtu anayejali sana muda hana mchezo katika time.

  Kama kuna mtu yoyote atamuona basi mpe jina Hamza Yousuf ( alizoea kuniita Mwarabu wa Zanzibar) mimi nilikuwa namwita Malafyale
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakuu niliahidi hapa kuwaletea habari na picha toka Mtwara na nimeanza kuziweka kule kwenye jukwaa la Jamii pichaz. Bado nakumbuka ahadi yangu.
   
 7. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35

  Jina kamili la huyo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa ni Nsajigwa Mwakaisi,naye akalifupisha kwa kujiita Nsa Kaisi. Amekwishastaafu Utumishi serikalini.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...