Kutoka magazetini: kifo cha Mandela chafunika sherehe za uhuru..

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Nilikuwa nafatilia habari toka magazetini kupitia Channel Ten, nimesikitika sana kwamba kati ya magazeti makuu yote kama nitakavyoyaorodhesha, hakuna lililoweka habari ya siku ya uhuru wa Tanganyika kwenye ukurasa wa mbele (front page), achana na kuifanya habari kuu, badala yake habari kuu (main story) imeonekana kuwa kifo cha Mandela.. Magazeti hayo ni:-
NIPASHE
TANZANIA DAIMA
DAILY NEWS
THE GUARDIAN
RAI
JAMBO LEO
HABARI LEO
ZANZIBAR LEO na
UHURU

SWALI: Mandela ni zaidi ya uhuru wetu??
 
Ukiona hivyo jua Uhuru wetu unaonekana ni utamaduni usio na tija kwa wananchi zaidi ya mbwembwe za gwaride na hutuba ya rais.
 
Ni bora hata tarehe hii isingekuwepo katika kalenda kwani tangu nizaliwe sijawahi ona faida yake zaidi ya kusikia ya kwmb serikali ime2mia mabilioni katika sehere hiyo ingali mambo ya kijamii bado ni kedekede!
 
Naona maadhimisho ya sherehe za uhuru yamechuja sana kwa sasa.. Ndo maana cdm na wenyewe wameandaa kongamano la vijana siku hii hii ya leo.. Ni kama kugombania wahudhuriaji!
 
Ukiona hivyo jua Uhuru wetu unaonekana ni utamaduni usio na tija kwa wananchi zaidi ya mbwembwe za gwaride na hutuba ya rais.

Well said mkuu mtanganyika aliyepo kule Kazuramimba hana hata habari na sherehe hizi yeye anawaza atapataje ugali wake mchana. Uhuru bila vitendo kwa maana ya hali ya mtanganyika kiuchumi kuwa bora haina maana.
 
Back
Top Bottom