Kutoka Kikao cha UKAWA

Kutoka Kikao cha UKAWA

Siku za mwanzo nilidhani una undugu na Mwalimu Nyerere (hivyo utasema ukweli daima bila woga), Lakini sasa hivi nikfungua post yako huwa ni kama napitia katuni za sani

Tatizo lako unapenda kusikia mambo matamu yenye uchungu ndani yake!Pole mwanachichiem! Watanzania sasa hatukubali tena khanga na tshirt!
 
Kinachowaunganisha wanaukawa wote kwa sasa ni slogan, sio itikadi mkuu.

Slogan yetu ni utaifa tu sio uzalendo wala ubwanyenye wa Lumumba

Utaifa bila uzalendo unakamilika kweli mkuu? au kwa kuwa uzalendo ni slogani ya ACT ndo maana unaipangua?....pia ukumbuke chama bila itikadi ni sawa na mtu bila kichwa.
 
Ukawa ni chadema,unategemea mgombea atoke CUF?

Independent-mind;
Mbona jina zuri saana hili halafu linakuwa ka limewekwa juu ya mti mchafu?? Kwenye kichwa chenyu mmejaa mawazo ya mgombea urais tuuu baasi.
Tunajua kuwa hata angetokea LND au NLD bado kubeza kwenyu kungekuwepo tu. Sawa jamani. Tunachokisema, si mabezo yenu yataacha kumchagua wa kupeperusha bendera ya UKAWA kama atatimiza masharti tuliyo kubaliana.
Mtanzania litangoja saana kitu cha kutusambaratisha nacho lakini halitakipata. Unaonaje, tukikubaliana kwamba, chama kitakachotoa mgombea urais kisiwe na majority ya wagombea ubunge, nyiye mkabaki kuangalia urais tukapeta kwa wabunge si hilo nalo ni bao??
Endeleeni na utoto wenyu, huku mwaliwaaaa:boxing::boxing:
 
mtanzania litangazwe rasmi kuwa adui namba moja wa chadema na ukawa, wanatunga mno!
Adui namba moja wa CHADEMA siyo ZITTO tena? Na kwa nini Mtanzania liwe adui namba moja wa CHADEMA na siyo UKAWA kwa sababu taarifa hii inahusu UKAWA na siyo CHADEMA? hapa kuna walakini.
 
Utaifa bila uzalendo unakamilika kweli mkuu? au kwa kuwa uzalendo ni slogani ya ACT ndo maana unaipangua?....pia ukumbuke chama bila itikadi ni sawa na mtu bila kichwa.

Huwezi kuwa na uzalendo kabla ya utaifa,

Kumbuka kuwa UKAWA sio chama, ndiomaana hawana itikadi moja,

Kinachowaunganisha ni kaulimbiu tua ama kwa lugha ya kigeni huitwa slogan.

Utaifa ndio jicho leo, utaifa wa Tanganyika, Utaifa wa Zanzibar na Utaifa wa Tanzania.

Serikali tatu nilazima sio ombi
 
Wakuu wanamageuzi,

Poleni kwa propaganda za ccm kupitia magazeti yao ya Mtanzania nk.

Napenda kuwajuza kuwa kikao cha wakuu wa UKAWA bado kinaendelea vema kabisa, na mambo makubwa yote yameshapatiwa ufumbuzi ikiwemo taratibu za kumpata mgombea wa Urais na changamoto za vifungu vya katiba juu ya wagombea hao.

Vuteni subira wakuu wa ukawa watatoa tamko rasmi baada ya kumaliza kikao chao.
Asante kwa taarifa, tunavuta subira huku tukisubiria taarifa kamili.

Endapo wewe ndie ofisa habari wa UKAWA, hongera sana, maana UKAWA imepata mtu!.

Pasco
 
Hivi umejisoma vizuri mkuu wangu. Kama tume imerasimisha utengano ulokuwepo utasemaje tume hiyo imeunda serikali 3 za Muungano wa kweli na sio Utengano wa kweli? Mimi nawashangaa sana mnapotumia ati S3 ni kuudumisha muungano ilihali mnajua mnachokifanya ni kutenganisha kile mnachoamini kimesha kuwa na Utengano basi bora Tutengane. Na ndivyo navyowasoma miye siku zote..

Kwa nini UKAWA msiwe wakweli muwaambie wananchi tunagenganisha - Zanzibar Kivyao na Tanganyika Kivyao halafu tuone kama wananchi watakuwa nanyi katika mbiu hiyo badala ya kutumia lugha za ulaghai..Semeni wazi tunataka UTENGANO maana upo siku zote tunarasimisha hakuna sababu ya kukataa kilichokuwepo.

mkuu, mimi si UKAWA wala si group la (CCM + ACT + TLP, etc). mimi ni mzalendo niliyekuwa miongoni mwa ile majority ambayo kamati iliyoteuliwa na kuaminiwa kukusanya maoni (Warioba Commission) ilisema tulipendekeza muundo wa serikali kama ulivyopendekezwa na tume.

kwa mantiki hiyo, kama utakuwa unawa-attack UKAWA as if wao ndiyo waasisi wa wazo hili "ovu" la S3 utakuwa unawaonea bure. lawama na laana zako zote uzielekeze kwetu sisi Watanzania wazalendo tuliopendekeza hili wazo ambalo obviously ni "haramu" from your point of view.

hilo moja. la pili ni kama baadhi ya wachangiaji wengine walivyosema kuwa federal govt ni kurasimisha the status quo...hapa sihitaji kufafanua kwani kila mtu anashuhudia jinsi ambavyo mambo yamekuwa yakipelekwa pelekwa huko Z'bar these past few years.

mzee wetu sheikh Aboud Jumbe si mjinga. wala mtoto wa mmoja wa waasisi wa muungano, Amani Karume. wala mmoja wa mawaziri waandamizi chini ya serikali ya Mwalimu, mzee Moyo. hawa wote si wajinga. kama ilivyo kwa sisi wazalendo tulio wengi tuliotoa maoni yetu kwa Warioba & co, they know exactly what direction this land should take ili kuondokana na ulaghai na nadharia za hawa opportunistic watawala wa sasa ambao leo wanamwita mmoja wao fisadi ghafla kesho yake wanamnadi kama "mchapakazi anayewajali watu wake". hapo nakuachia wewe upigie mstari na kuunganisha nukta mwenyewe!
 
Yericko Nyerere ni muongo, hata akisema saa hizi nje kuna mvua ingawa nnaisikia lakini mpaka nikatazame.

Anajidai kuandika kama vile yumo ndani ya hicho kikao. Na misukule inashangilia.

Mkuu FaizaFoxy,nakupa like tano za maandishi. Like,Like,Like,Like,Like.
Wajing.a ndio waliwao
 
Last edited by a moderator:
Wakuu wanamageuzi,

Poleni kwa propaganda za ccm kupitia magazeti yao ya Mtanzania nk.

Napenda kuwajuza kuwa kikao cha wakuu wa UKAWA bado kinaendelea vema kabisa, na mambo makubwa yote yameshapatiwa ufumbuzi ikiwemo taratibu za kumpata mgombea wa Urais na changamoto za vifungu vya katiba juu ya wagombea hao.

Pia utaratibu wa majimbo,vyote vimekamilika.

Hakuna chama kilichowasilisha barua yakujitoa wala aina yoyote ya kutokuelewana kunakoweza kupelekea kuvunjika kwa UKAWA kama ambavyo maadui zetu wanavyoeneza propaganda hizo,

Pia niwajuzi tu kuwa UKAWA hawajapokea ombi la mtu ama kikundi chochote kinachotaka kujiunga nao, na kwamba malengo na dhana nzima ya uwepo UKAWA yapo wazi kwa kila Mtanzania kuwa ni UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI, na slogan ya ukawa ni "Utaifa wa Uzanzibar, Utanganyika na Utanzania"

Hivyo kikundi chochote kinachotaka kujiunga na Ukawa ni lazima kikubali kujikana na kuyabeba malengo ya wanaukawa. Sio UKAWA ufuate matakwa ya kikundi hicho.

Vuteni subira wakuu wa ukawa watatoa tamko rasmi baada ya kumaliza kikao chao.

Njaa ya madaraka inawasumbua inshort ukawa hakuna kiongozi ambaye anafaa kuwa rais wa taifa hili zaidi ya ukwel kwamba wote wananjaa ya madaraka
 
Acha ukilaza.Kuna utaifa bila uzalendo sana tu.Mfano mafisadi nyote ni matanzania ila sio mazalendo.
Hamna uzalendo bila utaifa ila utaifa bila uzalendo upo tele.
Utaifa bila uzalendo unakamilika kweli mkuu? au kwa kuwa uzalendo ni slogani ya ACT ndo maana unaipangua?....pia ukumbuke chama bila itikadi ni sawa na mtu bila kichwa.
 
Maswala ya mimi kumpenda Zitto hadi nikalale naye unayaona mazuri sana na matamu, wengine wasiseme lolote juu yako wewe. Alaa unapofungua milango anaruhusu mambo haya na wala mimi siandiki kitu kama hujaelekea kuacha hoja unanifuata mimi. Hakuna hoja yako hata moja umezingatia Hoja iliyopo isipokuwa Mkandara na Zittto mbona miye sisemei Freeland na Slaa au Mbowe!

Bila shaka nilichoandika ndicho nilichokisoma ni hoja yangu kwamba mngetumia akili japo kidogo msingeendeleza hizi siasa za Utengano ambazo sisi wengine zimetutoa Chadema na UKAWA sitoiunga mkono hata kwa nini na nipo hapa kuipiga vita. Naamini na nitaendelea kuamini Chadema niloijua mimi baada ya 2010 ingeweza kabisa kuchukua majimbo mengi kuliko UKAWA na ingeweza kuwa chama pinzani kuua vyama vyote vingnevyo kama chama kingekubali mabadiliko ( Changes) kutenganisha Uongozi wa chama na Serikali na kutumikia sheria na kanuni walozweka ili kuonyesha mfano bora.

Udini umewaingia kiasi kwamba mmesahau kuwa Chadema haikuanza hivi mnakuwa kama CUF ya kabla ya uchaguzi wa 2010 mnajitangaza na Ukristu wenu sana halafu mkiambiwa mnakataa, sisi wengine sio mazuzu kiasi hicho. Siasa za separation athari zake ndio hizi na inawabidi muwe tayari kuzipokea..
Unapo ingia kuswali naamini huwa unaacha malapa na ubongo mlangoni mwa hekalu, maamuma unaingia na kushindiliwa mawaidha kwenye empty head, baada ya kumaliza ibada inakubidi urudie malapa yako na ubongo wako ili ukusaidie kudadavua mawaidha kwa weledi. Lakini kwa maandiko yako, unamatatizo..., hayaendani na elimu yako, nakukumbusha rudi pale mlangoni hekaluni, kachukue ubongo wako, nahisi ulikumbuka kuondoka na malapa pekee.Haiwezekani msomi mzima kuendekeza udini namna hii.
 
CUF ni walibelari....siasa zao ni mrengo wa kati....CDM ni mrengo wa kati kulia (Mabepari wenye msimamo usio Mkali) ACT-wazalendo ni demokrasia wajamaa na siasa zao ni mrengo wa kati kushoto.....CCM wao ni wajamaa hasa wa mrengo wa kushoto kinadharia ( mioyoni mwao ni mabepari kabisa mrengo wa kulia kabisa). Itikadi ya NCCR na NLD sizifahamu. Nawauliza mashabiki wa vyama wanapenda vyama vyao kwa misingi ipi? Itikadi au watu?

Sasa hivi ni free style, anayecheza beat za umma ndiye anayefagiliwa regardless chama, ila asije kinafiki na kifisadi.
 
Utaifa bila uzalendo unakamilika kweli mkuu? au kwa kuwa uzalendo ni slogani ya ACT ndo maana unaipangua?....pia ukumbuke chama bila itikadi ni sawa na mtu bila kichwa.

Hamna mzalendo, mzalendo alikuwa ni marehemu Sokoine
 
siasa za Utengano ambazo sisi wengine zimetutoa Chadema na UKAWA sitoiunga mkono hata kwa nini na nipo hapa kuipiga vita...
Lini wewe uliwahi kuwa Chadema? nani hakujui ulivyokuwa unapinga uongozi wa Mbowe ukishirikiana na wasaliti wazi wazi, nakushauri kuliko kupoteza nguvu zako bure kuipiga vita UKAWA vita ambavyo utashindwa tena kama ulivyoshindwa vita vya uenyekiti wa Mbowe, bora hizo nguvu uzitumie kujenga chama chenu kipya cha wasaliti.
 
Adui namba moja wa CHADEMA siyo ZITTO tena? Na kwa nini Mtanzania liwe adui namba moja wa CHADEMA na siyo UKAWA kwa sababu taarifa hii inahusu UKAWA na siyo CHADEMA? hapa kuna walakini.

Umeona shidayao wao likija hili wamefuata
 
Acha ukilaza.Kuna utaifa bila uzalendo sana tu.Mfano mafisadi nyote ni matanzania ila sio mazalendo.
Hamna uzalendo bila utaifa ila utaifa bila uzalendo upo tele.
Huwa sipendelei kuargue na watu wenye akili za kiuendawazimu.
 
Back
Top Bottom