Kutoka ITV: Mjadala kuhusu DOWANS; wachangiaji wataka maandamano nchi nzima

kwa mfano kati ya katiba na sheria ya nishati na madini, sheria ya uwekezaji na sheria iwayo yoyote ile, ipi ya kuheshu zaid? kati ya sheria na katiba, kipi kinatakiwa kulinda na kuheshimu chenzake? Je inatakiwa katiba iheshimu sheria au sheria ziheshimu katiba?

Katiba ni mama wa sheria zote na iwapo itatokea sheria mojawapo inakinzana na katiba basi sheria ile inakosa nguvu. Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri unamaanisha kwamba katiba ilikiukwa katika kuingia mkataba ule, sasa ni kipengele kipi /vipi vilikiukwa? lazima tuainishe ile tuwe na pa kusimamia. ili kujiridhisha kwa hili tafuta mkataba wa TANESCO na DOWANS uusome kisha uainishe kama ulikiuka vipengele vya katiba yetu vinginevyo tunarudi palepale
 
Maandamano yanatumika pale sheria inapokiukwa. Yana lengo la kuhamasisha sheria ifuatwe.
Je! Mahakama wamevunja sheria ktk kuibariki tuzo?
 

tume ipi na inaundwaje best? sijui kuhusu hili tafadhali nijuze

utanisamehe kidogo niliposema tume nilimaanisha ile mahakama ya International Chember of Commerce (ICC) ni kuwa mkataba ule unasema pakipotokea mgogoro wa aina yoyote kati yao basi mahakama hii ndio itahusika kuamua na maamuzi yake hayatopingwa wala kutenguliwa popote pale na ndio maana hata ilipoletwa hapa ilikuja kwa ajili ya kusajiliwa tu hivyo na mapingamizi yote yalikuwa ni kwa mahakama kutoisajili kitu ambacho kimeshindwa mahakama kuu na kinapelekwa mahakama ya rufaa. na wao wakipitisha hamna namna tutalipa tu. Hapa tuwabane wale waliongia mkataba huu wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kuwavua madaraka yao
 
Kimsingi nakubaliana nawe kabisa...... Wasiwasi wangu ni juu ya uwajibishwaji wa hawa waliohusika kwa maana ni wengi na pengine hata mwajibishaji mwenyewe atakuwepo. Sasa kwa utawala huu wa sheria unaobagua nani awajibishwe na nani asiwajibishwe unatutia mashaka. Hebu angalia watu waliowahi kufanya madudu ktk serikali hii lakini inafikia eti wanaombwa wajitafakari.......mwisho wa siku wameamua kukaa kimya na hamna wa kuwahoji...........

maneno yako kany yanaelekea kwenye suluhisho. nionavyo mimi hapa ndipo tunatakiwa kuwaondoa madarakani na kuwapa tunaowaona wanafaa kutuongoza. hili linaweza kufanyika kwa kuiga wenzetu wa Misri na Tunisia na wanachoendelea kufanya wa-yemen na wa-syria maana nchi ni yetu sote, serikali ni yetu sote na rasilimali ni zetu sote hivyo sote tuna wajibu wa kukemea na kuzitunza kwa maslahi ya kizazi kijacho
 
Mkinga is attempting to pave her way towards 2015 elections. His vitriol and caustic remarks against CCM are largely fictitious and utterly spurious. His trend has normally been followed by a lot of knavish protagonists who manipulate their platforms just to find their way into politics. So I don't see any genuine willingness inside this loquacious crusader but only a desire to leadership.

So what is your take? Leaders who pave their way through lies and corruptions or those who stands for truths? Whichever way you chose Dowans saga is scam, something need to done to protect our national resources. Wake up this has nothing to do with our political affiliation, I am a CCM aspirant but for Dowans issue no way I stand for our country intrests

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kwani, kwa kuwa sisi, raia ndio Wenye Nchi, na kwa mujibu wa Katiba, Serikali inapata ridhaa ya kutawala kutoka kwa Wananchi, na kwa kuwa sisi ndio tunaounda Katiba (kwa hiyo tuko JUU ya Katiba, kwa kuwa sisi ni ZAIDI ya katiba), tukiamua kwamba hizo pesa HAZILIPWI, na hao DOWANS walie tu, nani mwenye uwezo wa KUTUZUIA?

Nchi ni ya Watanzania, sio ya DOWANS! Kwa nini, (a) kampuni ambayo inatokana na kampuni hewa, (b) kwa nini kampuni ambayo ni hewa, iingie mikataba ya KIZUSHI na hawa TANESCO, kinyume cha sheria?

Isitoshe, kwa mujibu wa Sheria, huo mkataba ulikuwa batili pale ambapo Richmond waliuhamishia kwa hiyo DOWANS, bila kuishirikisha Serikali (TANESCO)! Breach of contract!

Why do we have to pay a NON-EXISTENT company? DOWANS ni NANI haswa? Mie nasema hizo pesa HAZILIPWI NG'O!

hapo kwenye red:

tunaweza kuamua tusiwalipe kibabe sawa tunaweza (ingawa sijawahi kusikia katika dunia hii mtu kaamriwa kulipa na mahakama halafu akakataa kwani kuna hata njia za lazima ikibidi) lakini tujue tunafukuza wawekezejai pamoja na biashara za aina zote na watu wa nje ikiwamo hata hawa jirani zetu kwani wataogopa kushirikiana na sisi wababe wa kutolipa madeni pia kuna wasiwasi wa hata kutengwa kimahusiano/kiushirikiano na nchi marafiki hasa kibiashara.

kampuni hii inasemekana ipo hapahapa Tanzania na wamiliki wake wapo na wanajulikana na nadhani hii ndio sababu tunathubutu kusema kwamba hatuilipa DOWANS hayo mabilioni kwani wamiliki wake wameshajulikana na inasemwa ingawa sina hakika kuwa ni watanzania
 
deni lina lipika. Jamani tusitake tutafute mchawi. Acheni tu tulipe hli deni yaishe. Tena si inasemekana hao wababe wa richmond ndo haohao wazee wa dowans, bas acha tu watanzania wenzetu wachukue hicho kiasi watawekeza then na sisi wengine tutapata ajira.

Wewe Tanganyika gani una akili za kitoto....UNARIZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIKA?
 
When the RICH rob the poor it called business and when the poor fight back its called VIOLENCE,i think the time of doing business with rich is over...let us fight back
 
Nakubaliana na Dr Nkya kutokubaliana na dhana kwamba uamzi wa mahakama ni wa mwisho hata kama
unanyonga watanzania.
Sisi ndio tuliowapa mahakama mamlaka waliyonayo,na tunaweza kuyachukua!
 
hata wakati wa wakoloni kulikuwepo na sheria lakini leo hii sheria zingine tunazipinga iwe mahakamani au kwa kutumia nguvu ndio maana leo hii angola ipo huru, zimbabwe, Mandela licha ya uhaini wake akawa Raisi nk nk, so tusikubali nyimbo za wanao fikiria kwa masaburi yao kuwa ndio maamuzi yetu sote. sauti ya wengi ni sauti ya Mungu
 
Sasa tuandamane kukataa kulipa deni au kushinikiza kuwaadabisha mahakamani hawa mabazazi walotufikisha hapa? Mi nafkir Wa'tz' wengi tunaendeshwa kwa hisia zaidi bila kufikiri

Nadhani si sahihi kuandamana kuzuia malipo kwa Dowans, wacha walipwe kwani kwenye sheria tumeshindwa, lakini tuandamane kuiondoa serikali hii iliyotufikisha hapa. Mimi sisemi waadhibiwe waliotufikisha hapa kwani huu ni udhaifu wa serikali yote. Wote waondoke. Tufanye kama Misri waondoke wote Jeshi litawale kipindi cha mpito, tuandae katiba mpya kisha twende kwenye uchaguzi. NO! NO! Kikwete and his fellows must go now.
 
Tanesco ikae kitako na dowans ipi hali ya kuwa hawajulikani.? HAKUNAGA .......
Yupo mwakilishi wao ambaye ananguvu za kisheria za kufuatilia deni hilo, naye ni mheshimiwa mtukufu sana Rostam Azizi. Alikili wazi kwamba yeye ndie mwakilishi wa Dowans. Kwa hiyo sio sahihi kusema Dowans hawajulikani.
 
Kwa hiyo hizi mahakama za kimataifa zikisema watz tutembee uchi, itabidi tufanye hivyo kwa madai kuwa hakuna jinsi? Mbona tunawapa kiburi sana mabeberu. Na hii ni gharama ya kujipendekeza kwao. Kitu kama hakiwezi kubalika katika taifa la watu makini. Kamwe!
 
Watanzania ni waoga,waongo,wanafiki,malimbukeni walio lala.mungu atkuja kutufufua siku ya mwisho
 
Nadhani si sahihi kuandamana kuzuia malipo kwa Dowans, wacha walipwe kwani kwenye sheria tumeshindwa, lakini tuandamane kuiondoa serikali hii iliyotufikisha hapa. Mimi sisemi waadhibiwe waliotufikisha hapa kwani huu ni udhaifu wa serikali yote. Wote waondoke. Tufanye kama Misri waondoke wote Jeshi litawale kipindi cha mpito, tuandae katiba mpya kisha twende kwenye uchaguzi. NO! NO! Kikwete and his fellows must go now.
Tafadhari usiliombee hilo kwani itakuwa sawa na kumuonjesha paka maziwa akinogewa utajuta.
 
Wezi wengine ndio hao wanaotetewa na mamruki humu ndani ya JF ,eti ndoto zao ni kugombea urais,uelewa wa baadhi ya watanzania au kutumika kwetu na wanasiasa kunatia shaka,tuangalie maslahi ya nchi ,waliohusika na RICHMOND watoswe
 
Hapa ni kuandamana mpaka kieleweke,make serikali nzima wameshindwa kazi,bora tuondoe uchafu wote kuanzia kwa mkuu
 
Kwa kuuchonga mdogo watanzania tumejaliwa, lakini kufanya maamuzi magumu hapo ndipo kila mtu kaufyata mkia!
 
Mkinga is attempting to pave her way towards 2015 elections. His vitriol and caustic remarks against CCM are largely fictitious and utterly spurious. His trend has normally been followed by a lot of knavish protagonists who manipulate their platforms just to find their way into politics. So I don't see any genuine willingness inside this loquacious crusader but only a desire to leadership.

yaani wewe ndio(neno baya) mara she mara he which is which.acha kukurupuka ndugu.kama lugha ya malkia inakusumbua andika kiswahili 2 tata.
 
wanaJF hamna mwenye hukumu ya kesi ya DOWANS iliyoamriwa juzi na mahakama kuu, upload hapa tusisome na yenyewe
 
Back
Top Bottom