Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Sitta ndio chanzo cha haya matatizo yote ya Dowans, nani asiyejuwa hilo?
Samwel Sitta si ndiye aliyeshauri/amua kwamba mkataba uvunjwe? Alikuwa hajui sheria ama ilikuwa ubabe tu wa kisiasa? Hapa kwa kweli tusilaumu mahakama yetu inabidi Sitta awaelezee Watanzania ilikuwa aamuru mkataba uvunjwe? Alikuwa ana backing gani ya kisheria hadi kuamuru mkataba wa kisheria kuvunjwa? Watu wanshindwa kuelewa kitu kimoja kwamba tatizo lilikuwa kwenye procurementt process ambayo ilifanywa na serikali/TANESCO Baad ya serikali kufanya procurement process na kumpata mzabuni waliyemtaka ndipo Richmond/DOWANS waliingia mkataba. Kwa hiyo mkataba ulioingiwa ulikuwa halali na walitakiwa kuwajibishwa ni wale waliofanya hayo manunuzi.