Kutoka ITV: Mjadala kuhusu DOWANS; wachangiaji wataka maandamano nchi nzima

sheria??????? to hell with it.kama inatukandamiza haina msaada wowote,jamani tuandamane tupinge hii hukumu na pia waliotusababishia hayo wapelekwe mahakamani na wafungwe...
nchi yetu inaliwa jamani,watoto wetu tutawapa nini? tumekaa tunaangalia wachache wanaifilisi inchi yetu? wanawekeza kwa ajili ya watoto wao wa kwako atakula nini? jamani chonde chode tuamke wapendwa.
this is too much,it is intolerable and i we should not take it any longer.
 
hata wakati wa wakoloni kulikuwepo na sheria lakini leo hii sheria zingine tunazipinga iwe mahakamani au kwa kutumia nguvu ndio maana leo hii angola ipo huru, zimbabwe, Mandela licha ya uhaini wake akawa Raisi nk nk, so tusikubali nyimbo za wanao fikiria kwa masaburi yao kuwa ndio maamuzi yetu sote. sauti ya wengi ni sauti ya Mungu

Mkuu umesema kwlikabisa, lakini enzi za ukoloni huko ni mbali sana; Kumbuka miaka michache tu iliyopita baada ya Mch. Mtikila kushinda kesi ya mgombea binafsi, serikali ikabadili sheria bungeni ilimradi tu mgombea binafsi asiwepo lakini ilikuwa baada ya hukumuya mahakama. Kama hivi ndivyo kwa nini bunge hilo hilo lisitunge sheria ya kutoridhia kusajiliwa nchini tozo zinazoshinda kampuni zilizopata zabuni kwa utata kama Richmond?
Nasema inawezekana.
 
Maandamano yanatumika pale sheria inapokiukwa. Yana lengo la kuhamasisha sheria ifuatwe.
Je! Mahakama wamevunja sheria ktk kuibariki tuzo?

Si lazima 'sheria zikiukwe' ndo tufanye maandamano. Hata kupinga sheria kandamizi zinazokwenda kinyume na katiba ni haki ya Raia. Kwa hili la Dowans waheshimiwa waliamua makusudi kuweka vipengele vitakavyolinda wizi huu. Sisi ndo wenye mali, tukatae kuhalalisha wizi huu!

Maandamano ya AMANI nchi nzima, tena iwe siku ya Nyerere, ili tumuenzi vizuri kwa kupigania haki na uhuru wa Mtanzania.
 
Maandamano yanatumika pale sheria inapokiukwa. Yana lengo la kuhamasisha sheria ifuatwe.
Je! Mahakama wamevunja sheria ktk kuibariki tuzo?

Mkuu, mimi naamini maandamano ni muhimu sana kwenye hili lakini nahisi tunachotofautiana wengi ni lengo/ujumbe wa maandamano ni upi?
1)Hatutaki DOWANS ilipwe or;
2)Tunalaani na ku-demand accountability kutoka kwa viongozi wetu specifically JK, Rostam (kiongozi wakati huo, na master mind), Lowassa, Uongozi Tanesco etc or;
3)Tuna-heshimu maamuzi ya mahakama lakini tunasema hatutalipa deni (since ni kampuni hewa na haina owner than deni linabakia kuwa hewa i.e. the deal was fake and so is the outcome)
or;
4) Both

Naamini wanasheria tulionao watatusaidia kujua if no. 1 is even legally possible. Lakini naamini kabisa we can strongly push on the number two agenda whether no 1 is possible or not. Regardless ya outcome ya hii kesi; kwa mtizamo wangu ni muhimu kuwe na out cry ya vitendo kutoka kwetu wananchi. Kuwaacha wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kulivalia njuga swala hili kuna send bad signal (itakuwa easy kwa maadui kuwasambaratisha wao wakiwa wachache. Lakini wakipata support ya vitendo kutoka kwa wananchi walio wengi inawapa moyo kuendelea kufichua na mengine tusiyoyajua. Mfano, naona watu wa LHRC wamepata nguvu yakuja na report ya Igunga kutokana na mwamko walioonyesha watu wa Igunga. Vinginevyo ingekuwa the same old stories.
 
Ni bahati kubwa sana jana Wife amepata nakala ya hukumu hiyo ambayo ina kurasa takriban 84. Lakini all in all since imesajiliwa tuzo hiyo na mahakama kuu ya huko Tanzania basi Tanesco lazima walipe hilo deni hata watu mkiandamana namna gani lakini deni litalipwa kisheria.

Ushauri wangu kwa wa Tz.
1. Tanesco kukaa kitako na hao Dowans na kuangalia namna watakavyoweza kulipa deni hilo. Kwani hilo ni deni la kisheria na si la kisiasa.
2. Tanzania kukuwajibisha kwa adhabu kali kabisa maafisa wake walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mkataba huo wa maangamizi si kwa Tanesco pekee bali kwa wavuja jasho masikini wa Tanzania.

Nafikiri mwenye software yake kama yupo tuuweke kwenye barza yetu ya sheria kuanza kuujadili

Nakubaliana na wewe kama Serikali itakuwa Transparent kuonyesha Mkataba wa Richmond and Dowans, ni namna gani ulihama kutoka upande mmoja kwenda kwingine na ni nani Wakurugenzi halali wa hizo kampuni, kama hawata fanya hivyo Watanzania tunayo haki ya Kuandamana Nchi nzima nami nipo Tayari, tafadhali naomba mniunge Mkono! Nawasilisha
 
hayawi hayawi mwishowe yatakuwa, kuna watu walifikiri na wapo wengine hata leo hufikiri kuwa , ahh mimi no , haiwezekani itokee kwangu no no no , labda kwa wengine, watu wa namna hii ndiyo hufa kihoro yanapokuja watokea na wao mambo yasiyozuilika, watanzania tukiendelea hivi na sisi yatatukuta tu, sisi ni binadamu wale wale wa Tunisia , misri nk. ...
 
Baelezee shosti, maana wansheria kama mh Sita wanahadaa wanchi kuwa dowans haifai kulipwa harafu wanakaa pembeni wanawaacha watanzania wakiumia. Wanasiasa na wansheria kama hawa wanatia kichefuchefu.

Sitta ndio chanzo cha haya matatizo yote ya Dowans, nani asiyejuwa hilo?
 
Nakubaliana na Dr Nkya kutokubaliana na dhana kwamba uamzi wa mahakama ni wa mwisho hata kama
unanyonga watanzania.
Sisi ndio tuliowapa mahakama mamlaka waliyonayo,na tunaweza kuyachukua!

Kwanza lipeni madeni mliyojiingiza kichwa kichwa. Hta Zitto atawasuta. aliwatahadharisha mapema kabla haya hayajatokea> mlimuona msaliti. Na sasa mnaanza tena kukurupuka kutumia maneno ya kugeuzwa geuzwa ya wanasiasa wanaotumia kila njia kuijipatia umaarufu hata kama italiingiza Taifa kwenye majanga, kisa huwa wako ambitious na hawaoni hawasikii zaidi ya kutafuta ukubwa wasiokuwa nao. Kiongozi hatafuti anatafutwa.
 
Kwanza lipeni madeni mliyojiingiza kichwa kichwa. Hta Zitto atawasuta. aliwatahadharisha mapema kabla haya hayajatokea> mlimuona msaliti. Na sasa mnaanza tena kukurupuka kutumia maneno ya kugeuzwa geuzwa ya wanasiasa wanaotumia kila njia kuijipatia umaarufu hata kama italiingiza Taifa kwenye majanga, kisa huwa wako ambitious na hawaoni hawasikii zaidi ya kutafuta ukubwa wasiokuwa nao. Kiongozi hatafuti anatafutwa.
Bibie,
Taifa limeshaingia kwenye majanga. Tangu IPTL ya Mwinyi na Kikwete, Net Solutions ya Mkapa, Richmond ya Kikwete/Rostum/Lowassa, nchi imeshaingia kwenye majanga. Haiingii akilini kuwa Richmond iliyokuwa ya kitapeli ikalipwa na Dowans na Dowans ikachukua mitambo na hata sielewi walitumia hila gani kusainisha mkataba huo wa kitapeli na TANESCO na wewe leo unashabikia kulipwa kwa wizi huu wa mchana. Have some humility.
 
sasa hapo ndio jiulize ww mwananchi ambaye hutaki kupigana unasubiria hadi uuzwe ndio utaona hautendewi haki sasa
lets fight then with one strong arm
ok sasa lini tunaanza kudai chetu
 
Sasa tufanye kweli na tuache maneno mengi, tuandamane kuuondoa uongozi dhalimu unaoinyonya nchi yetu.
 
Yupo mwakilishi wao ambaye ananguvu za kisheria za kufuatilia deni hilo, naye ni mheshimiwa mtukufu sana Rostam Azizi. Alikili wazi kwamba yeye ndie mwakilishi wa Dowans. Kwa hiyo sio sahihi kusema Dowans hawajulikani.

Kama malipo yataenda kwa huyu mheshimiwa kwanini tusimpigie magoti atuonee huruma watanzania jamani?? nafikiri nae ni binadamu na nahisi (sina uhakika) atakuwa na chembe ya huruma. Tukienda ni kina mama wajawazito, watoto waishio mazingira magumu, wanafunzi wanaokaa chini kwake huku machozi yakitutoka yawezekana akaionea huruma hii nchi na watanzania kwa ujumla
 
Nilifurahi sana mzee mkinga alivyokuwa anamalizia kwa kusema wanafunzi wa vyuo ni hamnazo et walimchangia pesa jk kwa ajil ya uchaguz alaf kesho yake wakaanza kuandamana kwa kulia njaa.tena wakaita wapinzan ni mavuvuzela
 
Wana JF tuliangalie suala hili kwa makini,na ifike mahali tusimame kwenye ukweli,ambao tunaweza hata kuushuhudia mbele ya imani zetu za kidini na hata kwa wasio na dini za kuletwa na mataifa nao wana miiko yao kwa kufuata maadili ya dini zao za asili,iko hivi sheria ni utaratibu tu uliowekwa na kwa nchi kama ya Tanzania mimi siamini katika sheria kwani sheria nyingi zimetungwa kwa kuwapa favour watu fulani hasa wakubwa tena wakubwa wa kutoka chama cha Mgamba.Nauliza hivi ni kwani nini sheria ziwe tu kwa watanzania walala hoi likini kwa wakubwa wa magambani hakuna sheria,hauna kukubali maamuzi ya sheria kwa wana-CCM.ikumbukwe kwamba mchungaji mtikala alishinda kesi ya mgonbea binafsi mahakama ilisema mtikila yuko right!kwani nini CCM hawakukubali sheria?hicho kisa kimoja lakini,hizo sheria kwa wale wanaosema tumlipe huyo Dowans kwa sababu ya sheria ambazo mara nyingine huwa haziegemei kwenye uhalisia na ukweli ambao tunaweza kuushuhudia hata mbele ya imani zetu,hamjui ya kuwa unaweza ukaiba au ukaua na sheria hizo mnazosema zikakuachia huru,lakini ukweli halisi unabaki pale kwamba umeeua?hizo sheria mnazozisema kwa Tanzania hakuna,kuna dhuluma ngapi zimetendeka kupita huo mgongo wa sheria?na hao mahakama wapo kwa ajili ya nani?nani kawaweka?na tukindelea kufuata mkumbo iko siku basi sheria zitatutaka tuhame nchi ss sio watanzania je tutahama?maana nchi inauzwa kwa mgongo wa sheria ya uwekezaji ss mwisho wa siku tukiambiwa ondokeni itabidi tuondoke?HAPANA,hapa hakuna cha sheria wala nini kwa ujinga huo ulikithiri na dharau mbaya zinzo-impress kutkanwa matusi ya nguoni nasema hapa dawa ni kuunga mkono watanzania wenzetu waliowasha moto wa kukataa malipo ya dowans kuanzia waliokwenda mahakamani na waliokuwa kwenye kipindi cha ITV.
Hapa ni kuweka umoja wetu mbele na kukataa,sasa maandamano hayo yakiunganisha vyote napo sawa kwa maana ya kukataa Dowans na kama vipi na serikali yenyewe.
Hivi kama huna hela ya kutibu watu wako,huna hela ya kulisha watu wako,huna hela ya kusomesha watu wako,huna hela ya kujenga barabara,huna hela ya kujenga na kuimarisha huduma ya nishati-umeme,leo ni kweli unadaiwa tena deni lenye riba utaliipaje?wakati umeshatangaza huna hela,hivi hela za kulipa mafisadi zipo za kuhudumia jamii hakuna,aaah no bwana,hapa ni kuigia barabarani na kukataa.
 
kaka akili yako ni finyu sana, jione tuu huruma. kuna cha uwongo anachosema huyo jamaa.kama huna cha kuandika hapa kwenye JF piga kimya.
 
Back
Top Bottom