Kutoka Dodoma!


Kasheshe,

Wenye kuamua hapo kama ni uchawi au sumu ni wataalamu na wala sio wanasiasa.

Ilikuwa lazima kuhusisha polisi ili wao ndio waamue kama kulikuwa na sumu au ni imani tu za kijinga.

Makosa tunayofanya nyumbani ni kudharau mambo madogo, dunia ya sasa hakuna jambo dogo, linakuwa dogo baada tu ya wataalamu kutuhakikishia kwamba ni dogo.
 

kwi kwi kwi kwi.............

Mbavu zangu kasheshe duh, kaazi kweli kweli.

You made my day kasheshe lol.
 
Shivji aliwahi kuniambia kitu kimoja, doubt everything! Siamini kama suala la bungeni ni uchawi. Ninaamini kuwa uchawi unatumika kutuzuga tu. Kwa nini sio radioactive materials?

Tufukiri kwa mapana
 
Shivji aliwahi kuniambia kitu kimoja, doubt everything! Siamini kama suala la bungeni ni uchawi. Ninaamini kuwa uchawi unatumika kutuzuga tu. Kwa nini sio radioactive materials?

Tufukiri kwa mapana

Mheshimiwa Zitto,

Mimi sio mtaalam wa radio active materials lakini I doubt kama unaweza kusambaza radio active materials kwa njia ambayo mhusika alitumia.

Unless kama lengo lake lilikuwa ni kujenga hofu, lakini kama ni kuleta madhara kwa wahusika, basi huwezi kufanikiwa kwa njia iliyotumika.Ingelikuwa rahisi hivyo basi akina Osama tayari wangeshatumia.

Kwa case ya bunge, basi hiyo material ingemdhuru Chenge zaidi ya mtu mwingine yeyote.
 

jamii naomba ikubali kwamba uchawi upo na hata misahafu imeandika kwa hiyo bwana chenge awajibishwe kwa hili na asionewe haya kwa sababu alikuwa kigogo serikalini
 

Mkuu Mtanzania, hakuna anayejua kwa hakika njia aliyotumia Chenge. Ndio maana uchunguzi lazima ufanyike kwanza. Wale waliokuwapo ukumbi wa Bunge (wa Star TV) hadi sasa hawajaitwa wala kuulizwa, Chenge na Sagasii wanaotajwa kuingia ndani hawajaulizwa na ofisi ya Bunge hadi sasa. Kuna contradiction statement kutoka ofisi ya Bunge. Kwanza Sitta anasema wanapeleka polisi (which is fact) lakini maofisa wake wanasema kwanza wanasema hawawezi kuwauliza Chenge na mwenzake kwa kuwa hawajapata ushahidi, na pia wanasema kamera zao zilikua zimezimwa wakati Sitta anasema zilizimwa zote ila moja ilibaki ON. Baadaye maofisa wa Bunge wanawaambia waandishi Kamera zao zote huwa ON saa 24 na hakuna ushahidi wa kumuona Chenge bali zinaona watu wengi mbalimbali. Hapo inachanganya kuona kauli za maofisa wa bunge zina kigeugeu, kwanza kamera zilizimwa pili zinafanya kazi 24hrs lakini Chenge hakuonekana. Nadhani wanabadili statement kila wanapoona walichosema hakisaidii kupoteza ushahidi. Hili suala ni serious tokea siku ya kwanza kujulikana. Yeyote anaweza kuwa mwoga hata akiwa shujaa wa aina gani, na si woga wakushindwa kupambana bali woga wa kujipanga na kuchukua tahadhari. Hata Vitani majeshi yenye nguvu hayapiani kiholela, hata kama wanapigana na kijeshi kidogo, lazima ujipange na kuwa na hadhari wakati wote. WAANDISHI WA HABARI WANAAMBIWA HAKUNA HABARI YENYE THAMANI YA MAISHA YAKO
 
nashindwa kuelewa kuna gazeti hapa linasema kilichofanyika ni tambiko, mjue tambiko no tofauti na uchawi , tambiko ni kama sala ya asili ya kumuombea dhahama adiu yako

kwa vyovyote vile, taifa letu lionapoteza dira, watu wanazungumzia uchawi na matambiko vitu vya karne ya 12.

wakti tutakapozinduka toka kwenye hili blanketi la uchawi na matambiko , akina barricks siyo tu watakuwa pale buzwagi, bali pia watakuwa pale magogoni au ikulu.
 
ukweli uliotolewa na jf mimi ninaukubali ila tu nasubili hao polisi dodoma watudanganye ndiyo tuwaumbue tena hatutawaonea aibu. chenge alitumwa na wananchi wake kuwasaidia matatizo yao na si kupeleka uchawi bungeni. ha ha haaaa sijui atawajibu nini wapiga kura wake kazi anayo.habari ndiyo hiyo.
 
jamii naomba ikubali kwamba uchawi upo na hata misahafu imeandika kwa hiyo bwana chenge awajibishwe kwa hili na asionewe haya kwa sababu alikuwa kigogo serikalini

tusiendelee kujitumbukiza kwenye imani za kiza, bali hatua kali zichukuliwe dhidi ya chenge kwa kuipotosha jamii dhidi ya mila potofu, au kwa kukusudia kutenda jambo la hatari dhidi ya wengine

pili, wanachi wa bariadi wasikubali kuongozwa na jambazi, fisadi, mwongo, na sasa mshirikina
 
********Kwanza, Naamini hili suala linajadiliwa KINAFIKI. Naomba niishie hapo bila kufafanua lakini ujumbe umefika.

*********Pili nakumbuka wakati habari za yule mtoto (kijana) aliyekamatwa eti akinyonya damu ya kichwa cha mtu, nilikutana na mtu mmoja muhimu katika jamii, akaniambia maneno yafuatayo, "Waandishi wa Tanzania na Watanzania ni wepesi kuvurugwa mawazo. Hawashangai kuona polisi na vyombo vya habari vimekua vikishabikia hili suala la ushirikina? Hawajui kwamba nchi imegubikwa na wimbi la UFISADI na Msamiati wa UFISADI umekaa hata katika vichwa vya watoto wadogo ambao, utakuta wanakwambia 'baba nataka nikifika shule wajue na mimi nina fedha za kifisadi wasinione lofa' na wahusika wanaona hilo ni tishio na sasa badala ya kujadili mambo ya maana wanawatengeneze ajenda za kijinga ili musahau UFISADI japo kwa muda wapate kujipanga" kauli ya mzee huyo sasa naiona tena humu JF, mahali ambapo sasa mada nyingine zote muhimu zimepotea na mada hii inapata wachangiaji wengi tena kwa mwelekeo wa UCHAWI zaidi.

Nafahamu wakati watu waliweka mada inayohusu NGONO ilipata wachangiaji wengi pia na wote wanalaani na kukemea, lakini ASILIMIA 90 ya wachangiaji walikua ni WANAFIKI kama walivyo wachangiaji wa mada hii ya VIJISENTI. Tufumbue macho na tuwe WAKWELI
 
Wacheni kuhangaika kama unasema hakuna mchawi basi utakuwepo katika lile likundi la akina Ngombale mwiru wa Kingunge ambao hawafungamani na upande wowote.
Kuna vitu viwili inategemea na kideo zenyewe natumai vijana wetu wapo mbioni kuzutafuta.
Jamaa ametumia juju au ametumia chemiko ambazo zipo na zinatumika katika mauaji ya sirisiri na unaweza kuanza kuumwa hata baada ya miezi sita au pia unaweza kuondoka ghafla au kuumwa gafula , inategemea na jinsi mwili wako ulivyozipokea ,kuna yule wa Ukraine ,kuna yule wa Uingereza na kuna hawa akina Balali ,Amina ambao vifo vyao vinatanisha na wengi kati ya hawa wetu walianzia kujisikia kama wana mimba huko huko machinjioni.
So far ikiwa mkono wa kutumia chemikali utakuwepo sidhani kama wachunguzi watakuja na rai ya kuumbua jambo hilo maana linaweza kuja kuzua mengine mapya ikiwa tu wale wenzetu walikufa kwa njia hii ya spray the sit and table kama yule wa Uingereza ambae inasemekana majasusi wa Kirusi walispray ndani ya ndege.Hivyo chain ya mauaji inaweza ikaja juu kama wahusika wa sakata hili la Mwakyembe walihusika na yaliopita ,watu itabidi wataje tokea walipoanzia ,hapo utaona walioko pembeni wanaweza kabisa kuukwepesha ukweli na kwa nini wasiitwe wataalam kutoka nchi za nje ?
Haya tukiingia kwenye juju wandugu juju lipo tena bado linanguvu za giza ,amini unachokiamini nguvu za kichawi zinaweza kukudhuru na ukadhurika ,ila kama na wewe ni mzito kwa lugha ya pwani kwamba na wewe umefungwa au umejifunga pengine mwakyembe amejifunga sana sasa ile kosakosa ndio amekuwa akipepesuka na kuyumba yumba huku akipita akipapasa ,hivyo baada ya kumaliza kiliniki na kutembezwa Muhimbili namtaka arudi kijijini kwenda kuongeza power.
aidha kuhusu wahusika sijui kama wameshachukuliwa hatua au bado wako mitaani wakitafuta jengine jipya ,tukumbuke tu hawa wengine walisikika kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa watafanya juu chini na wao kuondoka na watu ,hili wa kulaumiwa ni Mh.Kikwete na hata haya yanayotokea Bungeni Mh.Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kuwaachia wahuni hawa kutembea kifua mbele na sasa wanakuja maungoni hata hawaoni haya maana si kweli kuwa mhusika hatambui kama kuna security camera zinafanya kazi lakini kiburi ndicho kilichompa nguvu na kudharau Serikali nzima , kwamba hata zikimchukua hawatakuwa na cha kumfanya zaidi ya makelele ya siku mbili tatu ,mtu huyu alitakiwa akamatwe mara tu baada ya kumaliza ushirikina wake na kupata usimgizi katika vituo vya Polisi pale Dodoma.
Je mlioko Dodoma huyu mtu ametiwa nguvuni au hakuna wa kumkamata maana si ajabu ukaambiwa hakuna ushahidi.
 
Na sie wenye imani za kiafrika tutaweza kuukemea uchawi kwa jina gani?
Naona mwenzangu wewe mwenye dini ya kizungu umemtumia mnazareti......

kinjeketile Ngwale, milambo, mkwawa, chabruma,Kibanga,kambarage,Pazi,Kingalu,Mazengo,..... kemea kwa majina hayo kila kitu kitakuwa mswano, mafisadi wote watasambaritikia mbali!!!!!!!
 

Spika Sita alisema amewapatia wao vielelezo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wakishirikiana na uwt. Ndo tungoje tuwasikie watasema nini na wakae wakijua kuwa wakileta taarifa za ubabaishaji tu, mzigo utakuwa juu ya vichwa vyao
 
FMES,
Mkuu Mwaga vitu.....
Unajua inachekesha sana kuona watu wakijaribu kutetea mtu ati kwa sababu tu ana elimu ya Havard hivyo haiwezekani kuwa huyu mtu kasukumwa na imani ya Uchawi...Mngefahamu tu ya kwamba viongozi karibu wote duniani wanaamini rituals na huzifuata msingempa daraja huyu bwana...Nina hakika kabisa angekuwa Mkandara hapa mngesema kweli inawezekana kuwa anatumia uchawi!.. all this ni kwa sababu mtuhumiwa ni Chenge mwenye elimu ya KIDHUNGU (elimu ya kuiga)

Na kama kweli wapo viongozi ndani ya serikali yetu wasioogopa Uchawi inakuwaje kina Lowassa, Chenge, Karamagi, na kadhalika wanaendelea kutamba?...
Inakuwaje serikali inafikia kuwambia wananchi ati msiilaumu serikali ama chama kwa matendo ya watu wachache... wakati serikali na chama hicho bado kinawapa nafasi watu hao kushiriki kikamilifu katika maswala mengi ya serikali na chama?..kifupi sielewi kwa nini wapo bungeni ikiwa serikali hiyo ya Pinda inaamini hawa ni wakosefu na wanatakiwa kulaumiwa wao sio serikali. Why mnawapa hifadhi mafisadi!..Then tunaambiwa tusiilaumu serikali na chama wakati ni hizo serikali na chama ambazo zinatakiwa kuwakata kabisa ktk timu..
Ni sawa na mchezaji ambaye alikula njama na kusababisha timu yetu iwe Yanga/Simba/au Taifa Stars sio tu itufungwe goli bali ishindwe ktk mashindano tumlaumu mchezaji huyo na sio timu nzima!..hasa tukiangalia kuwa kilichofanyika ati mtu huyo anaondolewa ktk kundi la wachezaji 11 wanaoanza )1st eleven) lakini bado uongozi wa timu unamshirikisha ktk mazoezi, maandalizi ya timu na bado anachukuliwa mchezaji wa kulipwa..Tunategemea kitu gani hasa toka kwa mtu kama huyu ambaye aliweza kuiuza timu?..Watu kama hawa watajaribu kila kinachowezekana iwe imani za uchawi ama kisayansi kudhuru ama kuondoa wale wote wanaojaribu kuwa against maslahi yao. Chenge pamoja na elimu yake bado ni mwafrika deep ndani ya roho yake ataweza kuamini uchawi ikiwa umeweza kufanya kazi hadi sasa hivi... Kwa waliyoyafanya kina Lowassa, Karamagina wengine wote wameweza kulituliza taifa zima kutofukuzwa ama kufikishwa mahakamani. Ujinga huu usingeweza kuwepo ktk timu yoyote ile Yanga/Simba ama Faru ya Tandale.. wahusika wangefukuzwa kabisa wakacheze timu nyinginezo..
CCM na hiyo NEC wao wote waoga kama alivyo JK na woga huo unatokana na imani za kichawi! imani ambazo hadi sasa hivi zinaonyesha mafanikio makubwa!

Kifupi hadi sasa hivi mshindi ni CHENGE... yaani sasa hivi ndio watamwogopa zaidi! mtakuja nambia wenyewe mnacheza na Mgobogobo!
 
Dah..ndugu yetu chenge..kumbe hata wewe ni mtambikaji????!! kweli dunia ina mambo...!!!! sijui kama sheria za nchi zinatamka lolote kuhusu uchawi..ila ningependa sana ikithibitishwa kuwa ni yeye..hatua kali mnoo zichukuliwe juu yake ili iwe ni tishio kwa wale wote wanaojaribu kuliweka bunge katika hali ya wasi kwa vitendo ivyo......
 

UJINGA MTUPU, kila mtu anajua ni CHENGE lakini WOTE WANAMUOGOPA hata SPIKA mwenyewe na WAANDISHI WA HABARI, kwanini wasimtaje JINA?
 
Wakuu Wote ndugu zangu wa JF, heshima mbele in the next 15 minutes tutawamwagia yailiyojiri jana Dodoma na NEC,

Mbunge wetu Shujaa Mwakyembe bado yupo Dar kwa medical check zaidi, na tunamuombea sana kwa Mungu kuwa awe salama na aweze kurudi bungeni sasa maana tunamuhitaji huko sasa as anation kuliko wakati wowote wa uhuru wa taifa hili.

Ashante Wakuu nitarudi in 15 minutes na more Big Dataz kutoka Dodoma!
 
Kuna mambo hayaendi sawa bina sawia, hasa baada ya kusoma posts za watu ambao nina amini kwamba wanatoa maelezo ya kina kuhusu hili sakata.

Kwanza nimeshangazwa na jinsi Bunge kama Taasisi jinsi ambavyo linashughulikia hili swala. Kuna mambo mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na watendaji wakuu wa Bunge pamoja na wasaidizi wao na watunza usalama wa hilo jengo.

Iwapo camera za usalama za jengo lote zilikuwa zimezimwa, hiyo picha ya Mbunge na Katibu wa Bunge inayowaonyesha wakipita kwenye viti vya waheshimiwa wakimwaga vitu ilitoka kwenye camera ya chombo gani cha habari?

Kwanini kuna contradictions kwenye maelezo yao? Kwamba camera zilikuwa off, mara camera zilikuwa ON na Chenge haonekani? Hapa ninanusa harufu mbaya sana ya ufisadi uliopea. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Bunge kama Taasisi ilitumiwa na mafisadi ili kufanya hayo waliyoyafanya kwa faida ya mafisadi lakini wameumbuka baada ya picha kutoka nje camera za usalama kumuonyesha Mbunge na Katibu wa Bunge. Kwa hiyo kuna vigogo wa Bunge walijua nini kinafanyika na walitoa baraka zote, may be Sitta na Mama Makinda na some othe Big Shots hawakujua, lakini kuna watu very senior walikuwa involved. Hili swala linahitaji kuwahoji vigogo wote wa Bunge kuanzia Katibu wa Bunge mpaka wanaolinda.

Kuna uzembe fulani katika kushughulikia hili swala. Kwa kawaida mtu akienda kutoa taarifa za mauaji, wizi, na mengineyo huwa anakuwa makini sana kwamba mtu mwingine asiguse chochote ili ushahidi usije ukapotea ama asije akaharibu uchunguzi utakaofanyika. Mfano kuchukua kisu, kushika kitasa cha mlango ama kushika komeo la mlango au zana yoyote iliyotumika kufanya huo uhalifu. Ni polisi ndiyo wanatakiwa kuja kugusa hivyo vitu tena kwa uangalifu na umakini mkubwa ili wasije wakaharibu uchunguzi wao. Swali kwenye hii sakata ni kwamba, je, baada ya kupewa taarifa kwamba kuna madudu yalifanyika kwenye ukumbi kabla ya kikao, walizuia watu wengine kuingia ndani ili kutoharibu uchunguzi? Ni nani alipeleka taarifa kwa Sitta ama Uongozi wa Bunge kuhusu hilo tukio na je alipeleka kwa wakati muafaka? Na ni hatua zipi zilichukuliwa ili kuzuia kupoteza ushahidi?

Kudai kwamba siku ya pili kulikuwa unga unga kwenye kiti cha Mh. Mwakyembe ina maana kwamba wafagizi hakufuta kiti chake? Ama ina maana usafi haukufanywa? Kama kulikuwa na tukio kama hilo, kwanini Spika hakuahirisha kwa muda kikao hicho ili kupisha uchunguzi wa polisi ili kama kuna sample yoyote ya kuchukua wachukue na kwenda kuifanyia uchunguzi? Ina maana Spika hawezi kuahirisha kikao for a day ili kupisha uchunguzi wa kina ufanyike?

Jengo lile limejaa serikali na wawakilishi wa wananchi kwa hiyo nilitarajia kwamba Usalama wa Taifa hawalali na hawawezi kuwaamini wana usalama wa hapo na inawezekana wafanyakazi wengi wa Bunge kuanzia walinzi mpaka hao wasaidizi ndani ya ukumbi na hata wafagizi ni waajiriwa wa usalama wa Taifa maana humo ndani kuna PM ambaye anatakiwa kulindwa kwa ukaribu sana na pia Ukumbi wa Bunge ni jengo muhimu sana ambalo UWT wanatakiwa kuwa makini nalo masaa 24. Hili linanipeleka kwenye signal nyingine kwamba UWT imetekwa na mafisadi na inafanya kazi zake kwa maslahi ya mafisadi na ndiyo maana kuna mambo mengi sana ambayo hayaendi sawa kwenye uchunguzi wa hili sakata na sijui kama tutapta kitu cha maana kwa kuwa UWT wanaweza kuwa wanahusika na walifanya kwa mahesabu makubwa na kuhakikisha kwamba ushahidi unakuwa mgumu kupatikana.

Kwa mtazamo wangu, ni wakati muafaka kwa JK kubadilisha na kuisafisha UWT vinginevyo nchi hii itaendelea kuwa mikononi mwa mafisadi na iko siku watakuja kufanya mambo makubwa sana. Tukio la hapo Bungeni ni la kiusalama zaidi kuliko kisiasa na hivyo RO alitakiwa awe responsible kwa tukio hilo, maana ni aibu na kama hayo madudu yalifanyika na yeye hakujua basi kuna walakini mkubwa kwamba Idara imepoteza mwelekeo na iko siku tunaweza kusikia Waziri Mkuu ama Jengo zima wamekufa kwa kuvuta hewa ya sumu humo ndani na bado watakaokuwa responsible ni hao hao UWT. Hawa UWT ni wepesi kupenyeza watu wao kwenye vyama vya siasa ili kuvimaliza lakini nitashangaa kama RO atakuwa hana wafagizi, wahudumu, makatibu wa Bunge na wengineo ambao wanahusika moja kwa moja na shughuli za Bunge kila siku kwenye lile jengo. Kama ikiwa hivyo basi ina maana kwamba RO kashindwa kazi au sasa anafanya kazi kisiasa zaidi na siyo usalama wa taifa tena. Kweli nchi imetekwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…