Kutoka Dodoma!

Mchawi ni mchawi tuu haiwezekani kama alikuwa anatafuta viti na spika leo atoe tangazo kuwa ukumbi uko shwari na pia Bunge haliamini kwenye ushirikina.

Tamko la Spika la leo asubuhi ni kuwa kulikuwa na jambo la kishirikina ila Bunge haliamini kwenye ushirikina hivyo ni kweli kuwa kulikuwa na mambo ya Teknologia ya made from Bariadi ,huku si ndio kule maalibino wanapotea sana ?

Kuna Mbunge mmoja kaniambia kuwa waganga wanaakili sana kwani wanaweza kumwambia mtu atembee uchi na hakuna atakayeweza kumwona na mtu huyo akaamini hata kama ni mwanasheria aliyesoma Havard, mbele ya mganga hakuna akili ..
 
Sikonge ,

Tatizo ni kuwa by the time tunapata hicho "kikombe kisafi" breakfast time imeisha na ni lunch-time au pengine dinner-time! Sasa kwanini tusitumie kifuu kuinywa hii chai kabla time haija elapse?

Masatu,
Hapa ndipo kitendawili. Wazungu wamekuwa wakifa kwa ajili ya manufaa ya WANAO au taifa la kesho. Tatizo la kutumia kikombe kichafu ni kuwa wewe, utakiacha kikiwa kichafu zaidi. Wanao wakija watakuta uchafu mara mbili. Wajukuu ndiyo kasheshe. Uzuri wa KUGOMA ni kuwa "unapeleka ujumbe kwa FISADI" kuwa ehhh, NIMEKUSHTUKIA. Kutumia KIFUU badala ya KIKOMBE ndiko sisi hapa tunafanya. Sasa wee mwanzo uliandika kuwa "unatushangaa tunajadili UFISADI badala ya BAJETI. Sisi Bajeti hatuna shida nayo kwa sasa. Muda ukifika basi tutajakuja KUINYWA kwa kutumia KIKOMBE ambacho i hope by the time kitakuwa safi tayari. Mungu WAFUNUE WADANGANYIKA.
 

huu sio uchawi hapa jamani msimuonee chenge. wewe unategemea msomi wa Harvad anaweza kufanya uchawi? watu wamezidi kuchonga kweli, Kikwete alipoanguka mara mbili kwenye kampeni watu wakasema uchawi. Wanaccm wakienda bagamoyo kujiliwaza baada ya kazi ngumu ya kujenga nchi watu wanasema uchawi.

Mwacheni Chenge ajenge jimbo la bariadi na kuwasaidia wananchi wake.
 
Jamani mwacheni Andy!jalini mambo yenu!Mambo ya Andy mwachie yeye mwenyewe!Yaani maneno mengine kweli ni ya kusadikika!yaani conditional kibao!
yaani hilo wazo ulilotoa hapo halitakaa litokee!
Asante
Hollo

Hollo,
Mtoto wa NYOKA na yeye ni NYOKA. Kuna ujumbe nimesoma kuwa Dr. Mwinyi alikuwa akicheka wakati MAFISADI wakipewa UPPER-CUT kama zile za TYSON. Sasa kwa maana hiyo inaonekana mtoto wa MWINYI ni mpinzani wa UFISADI. Na kama ni hivyo basi kama BABA mtu alifanya na sasa hawezi, si tumpe mwanae? Tena ma-DR mara nyingi kutoa ROHO ya mtu kwao si shida sana. Wanaweza kukutoa kwa muda na kukupa tena. Ukiwatibua wanakutoa moja kwa moja. Mie napendekeza KAZI hii ya KUMKONGWE ANDEREYA aifanye mtoto wa Mzee Ruksa.
 
Hee! Mpaka kieleweke mwaka huu.Ufisadi hautavumilika wananchi tumechoka.Kuhusu kuchagua kiti hilo halipo hata Lowassa alijiuzulu uPM alirudi kwenye nafasi yake ya zamani.Na Mawaziri huwa wanaviti vyao spesheli pale wakijiuzulu au kupigwa chini wanarudi kwenye nafasi zao za zamani.
After all na kuchagua kiti mpaka akavuka koooooote akaenda mpaka kwa Spika???
WanaJF tusimame imara
 

MKuu masaka

Naona ya CHenge muachie Chenge. Chenge Mbunge wa bariadi yeye anajua alikuwa anafanya nini? Labda kama una data kuwa waliomuona alikuwa kweli asilimia mia anatafuta kiti tuwekee Mkuu.

Unajua wamesema alikuwa anakalia kiti chake cha uwaziri, tayari data ziko hapa za kuonyesha chenge alikuwa anakaa wapi.

Kuna tetesi kuwa hata alifika karibu na kiti cha Spika, bado hatukupata ufafanuzi alikuwa anatafuta nini hata huko.

Halafu kwa akili tu ya kawaida mbona kama alikuwa tu anatafuta kiti hawakutoa majibu mapema hata mpaka ikalazimu Spika kupeleka Ishue Polisi?

Mkuu Masaka najua wewe ni Mkataji wa Ishue vizuri sana na najua unajua sana hila kwa hili nasema ya Chenge muachie Chenge
 
ok asante kwa mawazo yako!ila haiwezekani kumuondoa duniani Andy!ni mpaka MUNGU mwenyewe aliyemuumba aamue!
Asante.
Hollo
 

Kama sio uchawi ni kitu gani?
Spika leo kasema kuwa Bunge haliamini kwenye uchawi ,na pia uchunguzi unaendelea ili kujua ni kitu gani kama ni sumu ya kisasa ama laa hivyo kuna haja ya kuamini yote mawili.

Huyu alitoka wapi kwenda mpaka kwenye kiti cha Spika ?kwani hapo napo alikuwa anatafuta sehemu ya kuketi?

Hata kama ni msomi ,kama anaimani za kichawi ni mchawi tuu ,mbona kuna maprofesas wanaenda kwa waganga ili wapandishwe vyeo?
 
Taarifa ya Spika inasema kuwa alionekana kwenye kamera hizo majira ya saa 2 na dk 38 usikuje?huko nako ni kutafuta kiti tuu ?

Aliposimama Spika leo cha kwanza ilikuwa ni kutoa taarifa kuwa usalama upo wa kutosha ndani ya Bunge, ili wabunge wasiogope kukaa mule ndani na kama hali ni hiyo huyu Anderea alitoka wapi kuonekana humo usiku wakati Bunge lilikuwa limefunwa?


Nataka wale wote wanaobisha wavute subira kwanza kwani kuna ukweli mkubwa kwenye hili na utadhihirika soon,
 
sasa yeye Chenge ameulizwa na waandishi kuhusu suala hili au ndio wote wanagwaya wakimdhani "kigagula"?
 
sasa yeye Chenge ameulizwa na waandishi kuhusu suala hili au ndio wote wanagwaya wakimdhani "kigagula"?

Mkuu

Mtu wameisha sema ana maskadi unafikiri hapo kuna wa kumsogelea? nafikiri si ajabu ukasikia hata waheshimiwa wanaokaa karibu naye wakiomba kubadilishiwa viti.
 
Thubutu! watu wameogopwa kugeuzwa msukule......itajulikana tu

Ya kweli hayo?????????na wewe sema tu!tutakupeleka "GAMBOSHI" shauri yako!
kwi kwi kwi!im joking!
Hollo
 
Mkuu

Mtu wameisha sema ana maskadi unafikiri hapo kuna wa kumsogelea? nafikiri si ajabu ukasikia hata waheshimiwa wanaokaa karibu naye wakiomba kubadilishiwa viti.
Tehe tehe tehe hayo ndiyo ya Andrea ndugu yake na Yakobo
 
Leo asubuhi wakati Kiongozi wa Upinzani akiwasilisha hotuba mbadala ya kambi ya upinzani wabunge wengi walionekana kuwa kimya na tulivu.

Anderea alikuwepo ila katoka mapema kuhusu waandishi kumuuliza hilo sijalijua nimejaribu kuwauliza baadhi ila wanasema kuwa haonekani yaani hawawezi kmpata .

Taarifa za kiongozi mwandamizi wa Bunge aliyekuwa naye ni kuwa ni miongoni mwa mwanasheria wa huko Bungeni na inasemekana aliwahi kusoma na Anderea na alifanya naye kazi sana za kutengeneza miswada ya kupelekwa Bungeni kwa kipindi chote akiwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Huyu naye ni miongoni mwa wanaoutaka ukatibu wa Bunge....
 

kusoma harvard sio kigezo wangapi matajiri wasomi wanajulikana lakini hawawezi lala kwenye vitanda au kutembea na viatu kisa ni condition za kichawi??nao hao unataka sema hawajasoma??sasa hebu tuambie saa mbili usiku alikua anafanya nin ndani ya bunge huyo msomi wako??
 
sasa yeye Chenge ameulizwa na waandishi kuhusu suala hili au ndio wote wanagwaya wakimdhani "kigagula"?
Sasa hivi Chenge amekuwa kama Mgonjwa wa UKOMA. Kama siyo JF sidhani kama watu wangelifahamu hili. Hii inanikumbusha story moja pale Ilala. nasikia gari la maji machafu likiwa kazini mara mpira ulifyatuka na jamaa mmoja akarushiwa choo na kulowa mwili mzima. Sasa jamaa akaanza kuwakimbiza wafanyakazi wa gari hilo ili awafunde. Jamaa si tu kuwa walimgwaya ingawa inasemekana alikuwa anatembeza masumbwi vizuri sana, ila tatizo ni kuwa kila sumbwi lake moja au teke ni kwamba anakupaka na choo. Jamaa alikuwa kama gari kwenye barabara la vumbi, ukiliona linakuja unalipishia mbali. Kuna haja ya kusikiliza ule wimbo wa "Masoud, amekuwa jambazi, ukikutana naye usiku mpishie mbali, ama si hivyo atakudhuru baba..." By the way mwuulizeni Mkwanyembe kama hakukutana naye hivi karibuni kabla hajaugua.
 
Jamani mwacheni Andy!jalini mambo yenu!Mambo ya Andy mwachie yeye mwenyewe!Yaani maneno mengine kweli ni ya kusadikika!yaani conditional kibao!
yaani hilo wazo ulilotoa hapo halitakaa litokee!
Asante
Hollo

angekua huo uchawi wake kaufanyia nyumbani mwake kwa mkewe na wanawa,sidhani kama tungeieven fungua thread kudiscuss mambo yake,ukumbuke uchawi huo kaufanya ndani ya bunge ambapo wawakilishi wetu sie wa tz wanago ku discuss mambo ambayo ni kwa manufaa yetu dats why yatubidi tudiscuss as its among our bnez n we shud b concerned abt them...

holllo if ur not chenge mwenyewe,his wife,mwanawe au punga lake kama sio huyo mganga wake (i doubt it if wanatumiaga internet),plz u better sometimes not bisha hata mambo yasiyofaa kubisha maana inafikia stage yakera kupita maelezo ila we hujui tu weye waona raha!!
 
Ya kweli hayo?????????na wewe sema tu!tutakupeleka "GAMBOSHI" shauri yako!
kwi kwi kwi!im joking!
Hollo

Mambo ya GAMBOSHI muulize mzee NYANI NGABU hiyo ndiyo mitaa ya kwao (joke)!!!! Kama kweli AC atakuwa amewaendea GAMBOSHI naona sasa itabidi wajiandae vizuri, usije sikia waganga washaletwa DODOMA kusaidia kusawazzisha mambo!!!
 
Habari iliyopo kwa sasa ni kuwa alikuwa anatafuta nafasi ya kukaa ili kesho yake asubuhi asihangaike!mimi ndivyo ninavyojua!hii ya uchawi mimi siifahamu!hivyo basi siwezi kukaa kimya hapa na kuona Chenge anasingiziwa habari ya uchawi!mlimzushia kifo hiyo haikuwatosha!jamani Give him a break
Sasa mkizidi tutawapeleka "GAMBOSHI" ( im joking)maana mmeng'ang'ania uchawi uchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…