bibikuku
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 832
- 495
Kutoka Bungeni jioni ya leo Wabunge wa CCM, Mh. Serukamba na Mh. Olesendeka wamepigania vikali hoja ya kupunguza muda wa awali kwa kodi ya uchakavu wa magari toka nje ya nchi toka miaka 10 iliyokuwa awali na kuwa miaka 8.
Wakitoa mapendekezo yao Mh. Olesendeka alisisitiza kwa kubakisha ongezeko hili Serikali itakuwa haijawatendea haki wananchi wake, kwa maana hiyo alikua anamuunga mkono moja kwa moja Mh. Serukamba hata ikampasa Mh. PM kusimama na kuondoa utata uliopo hata naye kuikubali hoja hiyo.
Nawasilisha!
mkuu wabunge wamekubalianaje katika hilo? wamerejesha miaka kumi au??