Kutengeneza vioja kwa lengo la kulichafua Kanisa Katoliki kunadhihirisha uwezo mdogo wa akili wa wapanga huo uovu

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,096
Wadhulumu haki na wauaji wanaumia sana na kufadhaika wakisikia yeyote ama akiongelea au kulaani udhulumati na ushetani wao walioufanya ile Oktoba 29. Kila anayechukizwa na dhuluma zao, huwa ni adui yao mkubwa. Na hasa kama wanaamini kuwa huyo anayechukizwa na uovu wao ana influence. Na kwenye hilo, wanaamini kuwa Kanisa Katoliki lina influence kubwa kwa waumini wake na wapenda haki wote, hivyo wanahangaika, huku kwa kutumia uwezo wao mdogo wa akili, wakiamini wana uwezo wa kulidhoofisha Kanisa kwa mbinu za hadaa na maigizo.

Kanisa Katoliki, kudhihirisha dhamira yake njema, hata kabla ya ule uchaguzi bandia, liliwashauri watawala kukutana na wadau na kufanya marekebisho muhimu ya kishetia na kikanuni ili uchaguzi uwe wa haki, na watanzania waingie kwenye uchaguzi wakiwa wamoja, kwani uchaguzi wa Serikali za mitaa, ulikwishaonesha wazi kuwa mamlaka za kiutawala zimeweka taratibu za kidhalimu kwenye michakato ya uchaguzi ili kubakia madarakani bila ya matakwa ya wananchi.

Viongozi wote wa dini, wakafanya kikao na kuweka maazimio ambayo wangeyafikisha kwa Samia kama kiongozi mkuu wa nchi, wakati ule. Kwenye kikao kile Fr. Kitima alikuwa katibu. Habari zilipowafikia watawala, hawakusubiri hata kufikishiwa hayo maazimio ya kikao cha viongozi wa dini, badala yake walifanya kikao cha haraka ambacho Bshungwa alishiriki, na wakaishia na maazimio kuwa wale viongozi wengine wote wa dini wanawamudu, ambaye ni vigumu kumhadaa kwa namna yoyote ni Fr. Kitima, hivyo wakaazimia kuwa adhibitiwe mara moja. Huko kumdhibiti ndiyo kukaishia kwenye mipango ya haraka ya kumwua! Mungu alimnusuru Fr. Kitima.

Oct 29 wakatekeleza ushetani wao wa kujipachika madarakani, na kisha kuua watu kwa maelfu. Father Kitima hakusita kueleza wazi kilichoshuhudiwa kwenye hospitali za Kanisa, ikiwemo kuwapeleka majeruhi mortuary badala ya kuwaruhusu wapate matibabu!

Watawala dhalimu wamejitahidi kufanya hadaa nyingi kwa Kanisa ili litumike kuwasafisha kwenye uovu wao, mojawapo ni kupiga picha na Fr. Kitima, lakini Fr. Kitima akaweka msimamo wake wazi. Wamebakia wamechanganyikiwa.

Mwiglu akaamua kumwomba Ldovik ashughulike na kazi ya kulipotezea kuaminika Kanisa Katoliki kwa waumini wake na wapenda haki, wakaanza na maigizo ya kuandika barua Roma, wakafeli; wakatengeneza maandamano bandia, yakafeli; juzi wakaja na pongezi kwa muuaji kupitia upandaji miti, nayo imefeli vibaya; na kisha kuzidi kuuanika uovu wao.

Mbinu zao zinadhihirisha uwezo mdogo wa akili walio nao, maana wanafanya hadaa ambazo kila mtu anajua kuwa ni upuuzi.

Eti watu wanajitangaza kuwa ni jumuiya ya Kanisa Katoliki, inafanya kazi ya kumpongeza Samia! Ni lini jumuiya ya Kanisa Katoliki au hata vyama vya kitume vilifanya kazi ya kumpongeza mtawala yeyote wa kisiasa? Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, hakuna mtu yeyote anayeweza kutoka na kufanya kitu chochote kwa jina la Kanisa bila ya mtu huyo kupewa kibali hicho na Paroko wake (kama ni jambo linaloishia ndani ya parokia), au Askofu (kama jambo linagusa level ya jimbo. Na huyo muumini hawezi kwenda kwa Askofu kuomba kibali hicho, bali paroko wake ndiyo atamwombea). Sasa hao mawakala wa uovu, eti jumuia, mkatoe tamko kuhusiana na utendaji kazi wa mtawala wa nchi, halafu mkilitaja Kanisa Katoliki, si uwendawazimu wa ajabu!!

Kama dhamira ni kutaka Samia awaone, kwa nini hata wasingesema kuwa "Sisi walevi wa Yombo Dovya, tunakuunga mkono kwa kupanda miti"?, wakapewa hela yao, wakaenda kulewa, wakisubiria usanii mwingine, mradi matumbo yao yajae?

Ludo na Mwgli wake, wanazidi kumsiriba vibaya zaidi mama yao kwa mbinu hizi za kipuuzi.

Kanisa Katoliki halikurupuki, na wala halitetereki, linazidi kuwa imara zaidi, na kuzidi kuheshimika zaidi na wapenda haki wote. Kanisa Katoliki halitafuti mamlaka ya kiutawala, bali haki ya watanzania na haki ya wanadamu wote, kwani ndiyo agizo la imani inayoungamwa, Mungu wetu, ni Mungu wa haki, nasi tukitaka kukaribiana naye, lazima tuwe watu wa haki. Kuona mwanadamu mwenzako akidhulumiwa haki yake, mwanadamu mwenzako akiuawa, akitekwa na kupotezwa, na wewe kukaa kimya wakati una nafasi ya kusema, ni kushiriki uovu anaotendewa hiyo mwanadamu mwenzako. Tusiliweke taifa letu chini ya utawala wa shetani, wala mawakala wake, maana wao ni wauaji; bali tulitafutie haki Taifa letu, liongozwe na wapenda haki wenye upendo wa kweli kwa Watanzania wote. Wauaji, watekaji, wabambikiaji wa kesi na waporaji wa mali za nchi, ndiyo maadui wetu wakubwa kwa sasa kuliko adui yeyote aliyewahi kulifikia Taifa letu, ukiwaondoa wale waliowafanya babu zetu kuwa ni punda, hata wakaifanya ndiyo biashara yao kuu, kwa kuwauza.
 
HATA SUALA LA SERIKALI KUTUMA UJUMBE WAKE VATICAN KANISA LIMECHUKIA SANA...WANACHOTAKIWA KUJUA NI KWAMBA SERIKALI INA NGUVU KULIKO WAO,SERIKALI INA ONGEA NA MWENYE MMBWA NA SIYO WAO WANUKA MIKOJO
Punguza kupanic. Mbona una comment wewe tu?

Kweli Wakatoliki wanakulaza na viatu mwaka huu. Na bado😄😄😄
 
Kinachonishangazaga kuhusu hawa wauaji, wamekuwa wakilituhumu kanisa kuhamasisha zile wanazoiita wao ni vurugu...

....halafu ukiwauliza hizo vurugu kanisa limehamasisha vipi? Wanasema eti kupitia matamko yao... haya waambie wakupe ufafanuzi kuhusu hayo matamko kivipi yana hamasisha hizo vurugu, hakuna maelezo ya maana watakayokupa zaidi ya hisia zao tu ambazo zimechanganyikana na ujinga mwingi pamoja na udini...

Walivyo na upeo mfupi hata huwa hawawazi kabisa siku huyu raisi wao haramu akiondoka na akaja mtu mwingine wa imani tofauti kabisa, wataishi maisha gani, yaan akili yao inawaza leo tu wajinga hawa.
 
Wadhulumu haki na wauaji wanaumia sana na kufadhaika wakisikia yeyote ama akiongelea au kulaani udhulumati na ushetani wao walioufanya ile Oktoba 29. Kila anayechukizwa na dhuluma zao, huwa ni adui yao mkubwa. Na hasa kama wanaamini kuwa huyo anayechukizwa na uovu wao ana influence. Na kwenye hilo, wanaamini kuwa Kanisa Katoliki lina influence kubwa kwa waumini wake na wapenda haki wote, hivyo wanahangaika, huku kwa kutumia uwezo wao mdogo wa akili, wakiamini wana uwezo wa kulidhoofisha Kanisa kwa mbinu za hadaa na maigizo.

Kanisa Katoliki, kudhihirisha dhamira yake njema, hata kabla ya ule uchaguzi bandia, liliwashauri watawala kukutana na wadau na kufanya marekebisho muhimu ya kishetia na kikanuni ili uchaguzi uwe wa haki, na watanzania waingie kwenye uchaguzi wakiwa wamoja, kwani uchaguzi wa Serikali za mitaa, ulikwishaonesha wazi kuwa mamlaka za kiutawala zimeweka taratibu za kidhalimu kwenye michakato ya uchaguzi ili kubakia madarakani bila ya matakwa ya wananchi.

Viongozi wote wa dini, wakafanya kikao na kuweka maazimio ambayo wangeyafikisha kwa Samia kama kiongozi mkuu wa nchi, wakati ule. Kwenye kikao kile Fr. Kitima alikuwa katibu. Habari zilipowafikia watawala, hawakusubiri hata kufikishiwa hayo maazimio ya kikao cha viongozi wa dini, badala yake walifanya kikao cha haraka ambacho Bshungwa alishiriki, na wakaishia na maazimio kuwa wale viongozi wengine wote wa dini wanawamudu, ambaye ni vigumu kumhadaa kwa namna yoyote ni Fr. Kitima, hivyo wakaazimia kuwa adhibitiwe mara moja. Huko kumdhibiti ndiyo kukaishia kwenye mipango ya haraka ya kumwua! Mungu alimnusuru Fr. Kitima.

Oct 29 wakatekeleza ushetani wao wa kujipachika madarakani, na kisha kuua watu kwa maelfu. Father Kitima hakusita kueleza wazi kilichoshuhudiwa kwenye hospitali za Kanisa, ikiwemo kuwapeleka majeruhi mortuary badala ya kuwaruhusu wapate matibabu!

Watawala dhalimu wamejitahidi kufanya hadaa nyingi kwa Kanisa ili litumike kuwasafisha kwenye uovu wao, mojawapo ni kupiga picha na Fr. Kitima, lakini Fr. Kitima akaweka msimamo wake wazi. Wamebakia wamechanganyikiwa.

Mwiglu akaamua kumwomba Ldovik ashughulike na kazi ya kulipotezea kuaminika Kanisa Katoliki kwa waumini wake na wapenda haki, wakaanza na maigizo ya kuandika barua Roma, wakafeli; wakatengeneza maandamano bandia, yakafeli; juzi wakaja na pongezi kwa muuaji kupitia upandaji miti, nayo imefeli vibaya; na kisha kuzidi kuuanika uovu wao.

Mbinu zao zinadhihirisha uwezo mdogo wa akili walio nao, maana wanafanya hadaa ambazo kila mtu anajua kuwa ni upuuzi.

Eti watu wanajitangaza kuwa ni jumuiya ya Kanisa Katoliki, inafanya kazi ya kumpongeza Samia! Ni lini jumuiya ya Kanisa Katoliki au hata vyama vya kitume vilifanya kazi ya kumpongeza mtawala yeyote wa kisiasa? Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, hakuna mtu yeyote anayeweza kutoka na kufanya kitu chochote kwa jina la Kanisa bila ya mtu huyo kupewa kibali hicho na Paroko wake (kama ni jambo linaloishia ndani ya parokia), au Askofu (kama jambo linagusa level ya jimbo. Na huyo muumini hawezi kwenda kwa Askofu kuomba kibali hicho, bali paroko wake ndiyo atamwombea). Sasa hao mawakala wa uovu, eti jumuia, mkatoe tamko kuhusiana na utendaji kazi wa mtawala wa nchi, halafu mkilitaja Kanisa Katoliki, si uwendawazimu wa ajabu!!

Kama dhamira ni kutaka Samia awaone, kwa nini hata wasingesema kuwa "Sisi walevi wa Yombo Dovya, tunakuunga mkono kwa kupanda miti"?, wakapewa hela yao, wakaenda kulewa, wakisubiria usanii mwingine, mradi matumbo yao yajae?

Ludo na Mwgli wake, wanazidi kumsiriba vibaya zaidi mama yao kwa mbinu hizi za kipuuzi.

Kanisa Katoliki halikurupuki, na wala halitetereki, linazidi kuwa imara zaidi, na kuzidi kuheshimika zaidi na wapenda haki wote. Kanisa Katoliki halitafuti mamlaka ya kiutawala, bali haki ya watanzania na haki ya wanadamu wote, kwani ndiyo agizo la imani inayoungamwa, Mungu wetu, ni Mungu wa haki, nasi tukitaka kukaribiana naye, lazima tuwe watu wa haki. Kuona mwanadamu mwenzako akidhulumiwa haki yake, mwanadamu mwenzako akiuawa, akitekwa na kupotezwa, na wewe kukaa kimya wakati una nafasi ya kusema, ni kushiriki uovu anaotendewa hiyo mwanadamu mwenzako. Tusiliweke taifa letu chini ya utawala wa shetani, wala mawakala wake, maana wao ni wauaji; bali tulitafutie haki Taifa letu, liongozwe na wapenda haki wenye upendo wa kweli kwa Watanzania wote. Wauaji, watekaji, wabambikiaji wa kesi na waporaji wa mali za nchi, ndiyo maadui wetu wakubwa kwa sasa kuliko adui yeyote aliyewahi kulifikia Taifa letu, ukiwaondoa wale waliowafanya babu zetu kuwa ni punda, hata wakaifanya ndiyo biashara yao kuu, kwa kuwauza.
Inasikitisha sana
 
Mimi naamini walifikiri mauaji waliyofanya wanaweza kuyaficha. Yaani wanahangaika hadi aibu. Ni kama mnara wa Babeli ulivyoanguka.
 
Back
Top Bottom