Ushimen
Platinum Member
- Oct 24, 2012
- 44,112
- 110,859
Mmh,afu hiyo avatar yako inatisha bhana
Mkuu, hiyo ndompango mzima maana hata umri unaelekea giza
Mmh,afu hiyo avatar yako inatisha bhana
Haya mambo ya kung'ang'ania sehemu moja ni hatar sana,huyo jamaa mpuuze tu hana jipya
Ukweli mapenzi yakigeuka inauma sana hasa Kama ulimpenda ukamthamini unaweza kuapa kutopenda tena msamehe ila uwe makini ht mm yalishawahi kunikuta nililia Sana japo naishi nae lkn kuna kitu kimeingia kwenye roho ambacho hata anitendee zuri cwz kumuamini tena
Mkuu wewe si ndio muasisi wa infidelityNarudia tena, usithubutu kumrudia. Wanaume kucheat ni jadi yetu, lakini huwa tunacheat kwa kuiba kama kweli tumependa. Ukiona mwanaume anakucheat mchana kweupe tena kwa shosti wako ujue hakupendi.
Kwa taarifa yako kakuponda sana kwa shosti yako. Na ukimrudia ujue atakuponda tena kwa mwingine atakayekucheat naye.
Kifupi ni kuwa HAKUPENDI.
Wapendwa ni matumaini yangu mu wazima na mko vizuri katika majukumu yenu:
Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu....
Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza ku........
Nae kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa,Kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.
Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini gafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio. Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake,nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu,rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.
Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake. Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo,nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia,nimetokea kumchukia.
Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendlea mbele,hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe mana natumia cm.
Ni muda mrf lkn hta akinita mke wangu cjickii furaha wala akinieleza habari zake cmwamini tena ukweli nilimwamini Sana hata cku nilivyomfuma nilipoteza amani mpk leo nimeathirika akili nipo nipo hata yeye hanielewi inauma unamlindia heshma halafu anakufanya mjinga
Asante imebaki kwake anakosa raha Niko bize na yangu hekaheka zakujipendekeza zimekwisha nilimaliza ufundi wote nikadhani ndo namtuliza akanilipa majuto cna ham
Mkuu, hiyo ndompango mzima maana hata umri unaelekea giza
Asante best,kusuffer sawa kupo ila jamani muwe mnaangalia mengine ya kukwepa jamani. Heri ya mwaka lakini
mara ya tani atacheat na yeye mwenyewe!Uije ukathubutu kurudiana naye kama unataka usife kwa presha.
Mara ya kwanza kakucheat na rafiki yako.
Mara ya pili atakucheat na ndugu yako.
mara ya tatu atakucheat na dada yako.
Mara ya nne atakucheat na mwanao. Na listi itaendelea.
Jasiri huwa haachi asili. Niamini nakuapia.